Pro CHADEMA acheni kumdhihaki Kikwete

Pro CHADEMA acheni kumdhihaki Kikwete

Angekuwa na uchungu na wanachi wake,angetibiwa MUHIMBILI ili aone ni namna gani wananchi wake aliosema MAISHA BORA kwa kila Mtanzania yamemfikia kila Mtanzania.

Jamaa yangu akiwa hospitali sidhani kama kuna tofauti na yeye akiwa hospitali,tofauti yao au yetu yeye ameenda kutibiwa UGHAIBUNI siye wengine tunasubiriwa KUFA pale Muhimbili kwa kukosa dawa.

Ukitaka ucheke na upate hasira na nchi hii, utasikia wakati wa propaganda za kipuuzi kwenye maandamano Mbowe aje ana familia yake lakini huwezi kuwasikia wakisema watawala/rais w/akiugua yeye na familia zao watibiwe hapa nchini. Kibaya zaidi hata hao polisi wasiojua sheria za nchi bali kusikiliza matakwa ya watawala wakiugua wanapelekwa kwenye hospitali hizihizi zisizo na dawa na huduma muhimu. Kama wangeruhusu wananchi kuandamana mbona mtu asingethubutu kwenda kutibiwa nje wakati wananchi hata dawa hospitalini hawana.
 
Jina la jk ni tamu sana kila ajisikiaye kuongea lazima alitaje hongera jk kwa kupendwa na watu wako mungu akuponye urudi haraka.
 
Kwani umewahi kumuona huyo mbowe katibiwa tarakea au amana lakini umemuona jk tu.
 
Chadema akili yenu inawatosha wenyewe tu kama mnaweza kuvua nguo mbele za watu sishangai mkifanya haya mnayofanya hapa kamanda wa chadema alikuwa anafanya nini?
View attachment 201179
CCM-Samaki-430x320.jpg
 
Yaani jk kaumwa kipindi kibaya sana hadi namuonea huruma..
_Hakuna dawa kwenye hospital na kisa ni deni la msd lilosababishwa na serekali yake alafu yeye kaumwa kaenda kutibiwa usa...
_Ni kama home kwako unajua kabisa hakuna chakula alafu unawatumia watoto picha ukiwa unakula serena hotel amabo bei ya msosi pale inatosha chakula cha mwezi kwako
_si dhihaka hii???

Watanzania hatuna noma nchi hii ni ya amani bwana. Sisi hata tukifa kwani nini bora rais apone.
 
untitled+of+tz.jpg

elimu.jpg

Maisha bora kwa kila mtanzania!

hii shule ingekuwa enzi zile nilitanua nondo ya darasa ili tu niweze kutoroka, nilibanwa wakati mwingine na mkojao lakini sikuweza kumwomba mwalimu ruhusa lakini hili darsa unachepuka tu pembeni unaingilia popote na kutokea popote
 
Jina la jk ni tamu sana kila ajisikiaye kuongea lazima alitaje hongera jk kwa kupendwa na watu wako mungu akuponye urudi haraka.

Ila ndugu zetu kweli mnapambana lakini hili la rais kwenda kutibiwa nje wakati mahospitali hayana dawa kwa uzembe wake imewakalia vibaya. Hapa inabidi mtumie misemo ya kiswahili kama ile ya Mwandosya jana kabla hujafa hujaumbika!! Ninaweza kupata picha dhamira inavyowasuta katika kipindi hiki kigumu japo ndio kula yenu lakini hili ni dhahama tu.
 
Kwani umewahi kumuona huyo mbowe katibiwa tarakea au amana lakini umemuona jk tu.

Duu leo hata mifano yenu inakuwa ni kama kuzuia risasi na debe. Mbowe ana ufunguo wa hazina. Ndiye aliyesema MSD wasilipwe? Jamani kwenye hili la JK kwenda nje wakati hospitali hazina dawa limekaa vibaya. Kwa ujumla halina picha nzuri hata yeye huko alipo dhamira inamsuta sema anajipa imani kwa sababu ya uzezeta wa watz.
 
Picha ya kwanza si dhihaki. Ni ukweli.

Ya pili ni banter. Get a life.

Let freedom of speech reign.

Noblesse Oblige.

Ukikaa sana marikani lazima uambukizwe ugonjwa unaoitwa freedom of speech, demonkreizi na mengineyo
 
Siasa za kijinga sana mtu anaumwa badala kutoa pole mnamdhihaki mh raisi. Pamoja hukubaliani nae ila wakati wamatatizo tunapaswa kuwa wamoja. Cheki msiba wa sataa wote wapinzani chama tawala walionyesha mshikamano.

Hata hapa akidedi raisi watanzania wote watashirikiana kumzika.. Ila kwenye tiba sasa ndo tofauti kabisa.. Mbingu na ardhi.. Ona sasa yeye busha tu ameenda kupasuliwa Marekani wakati mahospitali hayana dawa hapa kutokana na MSD kutolipwa madeni.
 
Uliyeleta picha/mada wewe ndo mchokozi umtengenza kashifa ya kijinga binafsi mimi nilikuwa sijui saiz nimejua.
 
Ukikaa sana marikani lazima uambukizwe ugonjwa unaoitwa freedom of speech, demonkreizi na mengineyo

Yalikuwepo tangu enzi za Wayunani wa kake hayo.

Ni wewe tu na dongo ulilomo ndo unaona hatari.

Bila ya freedom of speech hata JF ungekuwa unaisikia kwenye ngano tu.
 
Wakuu huyu Simiyu Yetu ana wadhifa gani pale lumumba; maana povu linamtoka kutetea udhalimu
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka ucheke na upate hasira na nchi hii, utasikia wakati wa propaganda za kipuuzi kwenye maandamano Mbowe aje ana familia yake lakini huwezi kuwasikia wakisema watawala/rais w/akiugua yeye na familia zao watibiwe hapa nchini. Kibaya zaidi hata hao polisi wasiojua sheria za nchi bali kusikiliza matakwa ya watawala wakiugua wanapelekwa kwenye hospitali hizihizi zisizo na dawa na huduma muhimu. Kama wangeruhusu wananchi kuandamana mbona mtu asingethubutu kwenda kutibiwa nje wakati wananchi hata dawa hospitalini hawana.

Mh!Ni kweli tido,na hapo wanogopa wanaweza wakakatiwa Internet Bundle.Wanajua wazi hali za hospitali zetu zilivyo na bado wako tayari kuuza nchi kwa vijipesa kidogo wanavyopewa.

Pole zangu nyingi kwa watanzania wenzangu wenye maisha ya kawaida ambayo Muhimbili ndiyo John Hopkins yake.!

Nimeamini UKIWA MCHOYO USIWE MROHO!
 
rais ni mtu mkubwa mbona kuna matajiri,wabunge na watu mbalimbali wanatibiwa nje ya nchi mbona hamsemi?
mwacheni rais wetu
 
Back
Top Bottom