tuwaombe net za mbu kama vipi
CCM na ushoga ni chanda na pete havitengani hata ukifanikiwa kutenganisha lazima alama ibaki.
Mengine ni porojo tu za kina Membe wasikike magazetini na shabiki wao humu wajaze page za thread.
Na barabara ya nyerere ilivyo mbovu...atajionea mambo ya ajabu prince wa watu.
wamewaalika ili iweje? wanahusika vp na miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania?
Hajaja kuangalia barabara amekuja kuangalia wanyama huko mbugani! Tuwe makini tu asije akaondoka na wanyama wetu haiNa barabara ya nyerere ilivyo mbovu...atajionea mambo ya ajabu prince wa watu.
Jana watu waliishutumu ooh chadema sijui ushoga saa hii sijui ni nini maana hawa jamaa acha tu.jana walisema tunawakataa mashoga, leo hao hao wanawakaribisha wenyewe! Aibu........!
Prince Charles na mkewe Camilla, wanatarajiwa kuwasili nchini jioni ya leo kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete kwa ziara ya siku tatu nchini.
Watakuwa nchini hadi Novemba 9 ambapo atatembelea maeneo mbalimbali, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Uingereza nchini, Mark Polatajko, Prince Charles na mkewe watapokewa na Rais Kikwete na mkewe, Salma Kikwete na kutumbuizwa na vikundi vya ngoma za asili.
My take: Kwa nini ikulu na rais Kikwete wamekubali ziara ya mashoga? tuseme habari wanazotutangazia kina Membe ni unafiki? wanatudanganya wananchi huku wao viongozi wakiukubali ushoga nyuma ya pazia??
nimekusoma mkuu ila nataka kujua jambo moja tu, nalo ni kuwa katika Uingereza nani ni mkuu wa nchi (head of state)? Pili nani ni mkuu wa kanisa la kiangilikana? hivi unajua kwamba anglikana huko uingereza walibariki ushoga hadi askofu shoga akaolewa? Inaweza kutenganisha vipi suala la ushoga, uanglikana wa uingereza na familia ya kifalme?Nachangia humu kwa kuweka tu kumbukumbu sawa. Kwanza, Kwa vyovyote vile, Prince Charles hawezi kuwa amealikwa jana kuja Tanzania. Mwaliko wake utakuwa wa siku nyingi kabla Waziri Mkuu David Cameroon hajatoa msimamo wake Mkutano wa Chama chake cha Conservative na alipokutana na mwandishi wa BBC huko Perth. hivyo, ziara ya Prince Charles ilikuwapo kabla ya tamko hili, naye hajawahi kujitangaza kama ni shoga. OAnajulikana kuwa ni rijali tena mwenye kupenda sugar mummy na ndio maana akazamia kwa Bi. Camila akamuacha Princess Diana.
Pili, ni muhimu pia kuelewa kuwa, ndani ya Uingereza mwenyewe hakuna muafaka juu ya suala hili. Serikali ya Chama cha Conservative inajaribu kuifanya kuwa agenda ya kitaifa na kimataifa. Wameanzia katika kutafuta muafaka kwenye Chama chao na sasa wanataka kutungia Sheria. Miaka miwili tu iliyopita wakati wa Serikali ya Labour Party, jambo hili halikupewa nafasi kabisa ingawa kilio hiki kilikuwamo ndani ya Uingereza. Hivyo, hadi sasa, sio Sera rasmi ya NJE ya Uingereza na kwa vyovyote haihusiani na ziara ya Prince Charles. Balozi wa Uingereza hapa nchini ameshajitokeza Jana kukanusha, jambo ambalo linaashiria kuwa Waziri Mkuu Cameroon aliteleza ulimi kutokana na ugeni wake katika Uongozi wa Nchi.
Tatu, Prince Charles anakuja nchini kama Mwakilishi wa Malkia (Royal Family) na si Serikali ya Uingereza. Katika Siasa za Uingereza, Waziri Mkuu ndio kiongozi wa Serikali. Prince Charles hana mamlaka ya kutoa msaada wala kuingia Mkataba wowote kwa niaba ya Uingereza. Hivyo, si mtu anayeweza kuathiri Sera au kushawishi Sera fulani. Ujio wake Tanzania ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru na hivyo hauhusiani na tamko la Waziri Mkuu wake. Kwa mantiki hiyo huwezi kuhusisha ziara yake na kupromote ushoga.
Hayo ndio maoni yangu ikiwa pengine jambo hili halikufanyiwa utafiti na muanzisha mada. Ila kama mwenye mada aliamua kupotosha kwa makusudi, basi maoni haya yapuuzwe.
a
nimekusoma mkuu ila nataka kujua jambo moja tu, nalo ni kuwa katika Uingereza nani ni mkuu wa nchi (head of state)? Pili nani ni mkuu wa kanisa la kiangilikana? hivi unajua kwamba anglikana huko uingereza walibariki ushoga hadi askofu shoga akaolewa? Inaweza kutenganisha vipi suala la ushoga, uanglikana wa uingereza na familia ya kifalme?