Prince Charles kuwasili leo kwa mwaliko wa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prince Charles kuwasili leo kwa mwaliko wa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Nov 6, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Prince Charles na mkewe Camilla, wanatarajiwa kuwasili nchini jioni ya leo kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete kwa ziara ya siku tatu nchini.

  Watakuwa nchini hadi Novemba 9 ambapo atatembelea maeneo mbalimbali, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Uingereza nchini, Mark Polatajko, Prince Charles na mkewe watapokewa na Rais Kikwete na mkewe, Salma Kikwete na kutumbuizwa na vikundi vya ngoma za asili.

  My take: Kwa nini ikulu na rais Kikwete wamekubali ziara ya mashoga? tuseme habari wanazotutangazia kina Membe ni unafiki? wanatudanganya wananchi huku wao viongozi wakiukubali ushoga nyuma ya pazia??
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hapa ndio tutaona kama wanamaanisha!
   
 3. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  wamewaalika ili iweje? wanahusika vp na miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania?
   
 4. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SI wamekuja kuwathibitishia kuwa tunaunga mkono haki za binadamu na mashoga hivyo chonde chonde msikate misaada.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,939
  Trophy Points: 280
  tuwaombe net za mbu kama vipi
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  CCM na ushoga ni chanda na pete havitengani hata ukifanikiwa kutenganisha lazima alama ibaki.
  Mengine ni porojo tu za kina Membe wasikike magazetini na shabiki wao humu wajaze page za thread.
   
 7. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh ha haaa!
   
 8. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya sasa.
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Na barabara ya nyerere ilivyo mbovu...atajionea mambo ya ajabu prince wa watu.
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana ukarabati pale mtava umeshika kasi.
   
 11. Fang

  Fang Content Manager Staff Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 489
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Only with time will we get the appropriate answers.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ni wao waliotupa uhuru, kwa hiyo wanakuja kukagua namna uhuru huo ulivyotusaidia. Union Jack ilipotelemshwa pale Uwanja wa Taifa, ilikabidhiwa kwa baba yake, yaani Prince Philip; leo hii Prince Charles anamwakilisha baba yake Prince Philip kupima maendeleo yetu.
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,396
  Likes Received: 22,273
  Trophy Points: 280
  JK kaanza kutuletea mijishoga, loh.
  Lijishoga likifika tulivalie kanga za kumnanga, tumwekee na taarab za kumtukana
   
 14. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  jana walisema tunawakataa mashoga, leo hao hao wanawakaribisha wenyewe! Aibu........!
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hajaja kuangalia barabara amekuja kuangalia wanyama huko mbugani! Tuwe makini tu asije akaondoka na wanyama wetu hai
   
 16. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana watu waliishutumu ooh chadema sijui ushoga saa hii sijui ni nini maana hawa jamaa acha tu.
   
 17. S

  Sheba JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nachangia humu kwa kuweka tu kumbukumbu sawa. Kwanza, Kwa vyovyote vile, Prince Charles hawezi kuwa amealikwa jana kuja Tanzania. Mwaliko wake utakuwa wa siku nyingi kabla Waziri Mkuu David Cameroon hajatoa msimamo wake Mkutano wa Chama chake cha Conservative na alipokutana na mwandishi wa BBC huko Perth. hivyo, ziara ya Prince Charles ilikuwapo kabla ya tamko hili, naye hajawahi kujitangaza kama ni shoga. Anajulikana kuwa ni rijali tena mwenye kupenda sugar mummy na ndio maana akazamia kwa Bi. Camila akamuacha Princess Diana.

  Pili, ni muhimu pia kuelewa kuwa, ndani ya Uingereza mwenyewe hakuna muafaka juu ya suala hili. Serikali ya Chama cha Conservative inajaribu kuifanya kuwa agenda ya kitaifa na kimataifa. Wameanzia katika kutafuta muafaka kwenye Chama chao na sasa wanataka kutungia Sheria. Miaka miwili tu iliyopita wakati wa Serikali ya Labour Party, jambo hili halikupewa nafasi kabisa ingawa kilio hiki kilikuwamo ndani ya Uingereza. Hivyo, hadi sasa, sio Sera rasmi ya NJE ya Uingereza na kwa vyovyote haihusiani na ziara ya Prince Charles. Balozi wa Uingereza hapa nchini ameshajitokeza Jana kukanusha, jambo ambalo linaashiria kuwa Waziri Mkuu Cameroon aliteleza ulimi kutokana na ugeni wake katika Uongozi wa Nchi.

  Tatu, Prince Charles anakuja nchini kama Mwakilishi wa Malkia (Royal Family) na si Serikali ya Uingereza. Katika Siasa za Uingereza, Waziri Mkuu ndio kiongozi wa Serikali. Prince Charles hana mamlaka ya kutoa msaada wala kuingia Mkataba wowote kwa niaba ya Uingereza. Hivyo, si mtu anayeweza kuathiri Sera au kushawishi Sera fulani. Ujio wake Tanzania ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru na hivyo hauhusiani na tamko la Waziri Mkuu wake. Kwa mantiki hiyo huwezi kuhusisha ziara yake na kupromote ushoga.

  Hayo ndio maoni yangu ikiwa pengine jambo hili halikufanyiwa utafiti na muanzisha mada. Ila kama mwenye mada aliamua kupotosha kwa makusudi, basi maoni haya yapuuzwe.


  a
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  nimekusoma mkuu ila nataka kujua jambo moja tu, nalo ni kuwa katika Uingereza nani ni mkuu wa nchi (head of state)? Pili nani ni mkuu wa kanisa la kiangilikana? hivi unajua kwamba anglikana huko uingereza walibariki ushoga hadi askofu shoga akaolewa? Inaweza kutenganisha vipi suala la ushoga, uanglikana wa uingereza na familia ya kifalme?
   
 19. S

  Sheba JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante, Mkuu wa Kanisa la Anglikana ni Malkia. Kanisa la Anglikana limeruhusu ushoga. Mpaka hapo tuko tuko sawa. Pili, umesema Malkia ni Mkuu wa Nchi. Hapo pia uko sahihi.

  Sasa kukujibu, mosi, unapaswa uelewe kuwa Malkia ni Mkuu wa Kanisa Anglikana kutokana na historia. Kanisa la Anglikana lina uongozi wake na yeye ni symbolic figure tu ndio maana Askofu Mokiwa hapa anatunisha msuli tu na hajaondolewa. Hivyo,si mtu mwenye kuathiri maamuzi ya Kanisa la Anglikana. Hana Mamlaka aliyonayo Papa ambaye anateua hadi padri katika Wilaya yako akiwa Vatican. Lakini isitoshe, Prince Charles haji Tanzania kama Mkuu wa Kanisa la Anglikana kwa kuwa yeye si Mkuu wa Kanisa hilo, bali mama yake. Aidha, Tanzania ni nchi isiyo ya dini, hivyo heshima ya Mama yake juu ya Kanisa haina nguvu hapa. Pengine ushawishi huo anaweza kuwa nao kwenye zile nchi 16 ambazo yeye bado ni Head of State Kama Australia, Canada etc.

  Pili, Malkia ni Head of State. Nenda mbali zaidi kujisomea na utakutana na ukweli kuwa Malkia ni symbolic figure na si Absolute authority katika siasa za Uingereza, ndio maana nchi ya Uingereza ni Constitutional Monarchy na si Absolute Monarchy Kama Swaziland, Saudi Arabia na nyinginezo. Hata katika nchi zenye Presidents kama Heads of State, sio kote marais hao wana absolute powers. Rais wa India na Ethiopia ni symbolic figures, madaraka yote yako kwa Waziri Mkuu.

  Hivyo, familia ya Malkia inaweza kabisa kuamua kuwa Mashoga wote lakini hawana uwezo wa kuathiri maamuzi ya wengine kuwa Mashoga au kutokuwa Mashoga. Uamuzi wa waonkuwa Mashoga wakitaka tunaweza kuuheshimu tu, lakini hawezi na wala Hana instruments za kutushinikiza nasi tuwe Mashoga. Nadhani nimejitahidi kujibu.
   
 20. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,463
  Likes Received: 10,682
  Trophy Points: 280
  mjukuu wangu sheba mbona unahaha kumtetea prince ?unafanya kazi british council?labda nikwambie tu maandamano yatatoa ujumbe kwa familia ya malkia kuwa kijana wao cameron alikosea kutishia nchi maskini kisa hazikubali ushoga.
   
Loading...