Wadau kama utamaduni wetu wa Kitanzania nimewekewa pressure ya juu sana ya kuoa!. Umri wa miaka 38 kwenda 39 sasa pressure imekuwa juu sana kama unavyojua utamaduni wetu.
Mimi nilivyokuja US kama vijana wengi ambao tulimaliza shule miaka ya kati ya 1990's tulikuwa hatujui vizuri tunakuja huku kwenye nchi nyingine na mazingira yatakuwaje. Hivyo vijana wengi tumeanza kuwa wenyewe bina watu wazima wa kutuangalia au kutupa mawazo kuanzia miaka 21.
Pamoja na kuwa na uhuru wa hali ya juu hasa hapa USA vilevile tumekuja kwenye utamaduni wa kujitegemea sana. Mapema sana kwenye safari yetu ya maisha ya hapa ilibidi tuchague maisha gani tunataka kuna waliochagua kujirusha, kupiga deals na kujichanganya na wengine tuliamua kujaribu kujisomesha na kutafuta kazi au biashara huko mbele. Kwa tuliochangua kwenda shule na kukimbia matamani ya hapa USA tulijaribu kupunguza au kuacha vitu Fulani vinavyo punguza mwelekeo wa maendeleo.
Pamoja na vitu ambavyo mimi binafsi niliamua kupungua ni wanawake/kukaa nawanawake na kuacha pombe. Hii ni baada ya kuona matatizo vijana wenzangu waliyokuwa wanapata. Nilisema nitaacha vishawishi mpaka nipate green card na kumaliza elimu ya degree.
Mungu akanibariki lakini tatizo ni moja tu elimu ya kujisomesha hapa USA sio rahisi na degree ya kwanza hapa ni ndefu sana hivyo nilisubiri green card yangu kwa miaka mitatu ili niweze kulipia shule kwa bei nafuu kwama wenyeji. Kupiga mahesabu na elimu ya kusua sua nilimaliza chuo nikiwa na miaka 31 kitu ambacho ni cha kawaida kwa watu wa kuja kama mimi. Nilifanikiwa kupata green card, kazi nzuri na kila kitu ambacho nilikuwa nataka.
Tatizo ni kwamba baada ya kuweka ule utaratibu wa kujiheshimu na kupunguza vishawishi sasa umekuwa kama utamaduni siwezi kurudi kama zamani. Pamoja na kwamba hii tabia imenisaida kimaisha kwenye kazi na pesa haijanisaidia kwenye maisha ya familia. Watu naokutana nao kwenye kazi si wabongo na hata si waafrica, sehemu nayoishi haina watanzania wengi au waafrica wengi sio mji lakini sihemu ya makazi/mtaa.
Umri wa kwenda madisko na kujirusha umepita na napenda kukaa nyumbani na kufanya mazoezi. Kwa ufupi maisha yangu naweza kuishi mwenyewe bila wasiwasi. Tatizo lingine ni kwamba unavyozidi kuwa mtu mzima vitu viwili vinajitokeza kuhusu mahusiano (1) Unakutana na wanawake wengi wenye matatizo sana kwenye background zao (2) Unakuwa na akili sana ya kiutu uzima na unajua weakness haraka sana za watu. Kuwa smart sana kwenye mapenzi wakati mwingine sio nzuri. Napenda kuwa na familia lakini sitaki kuwa tu na mtu yeyote kwa sababu ya kuwa na familia.
Sasa na pressure kubwa sana wazazi wangu hatuwezi kuongea kitu kingine ni kuoa tu! Cha ajabu nafanyiwa connection za watu ambao siwajui kabisa na marafiki wengine wananipa namba na picha wa wanawake tofauti ambao sijawahi kuwaona eti niwapigie simu.
Pamoja na nia njema za hawa ndugu na marafiki nafikiri tatizo langu kubwa ni mazingira. Naogopa kuongea hawa madada kwenye simu na wenyewe kufikiria wanaenda kuolea na jamaa marekani wakati hata hatujuani.
Pamoja na kwamba sijauliza waunganishi wengi wamekuwa wakinipa viwango vya elimu vya hao madada na picha za vishawishi na kuonyesha uzuri wao.
Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu najihisi kama nilifanya makosa kwa kuwa kama nilitokomeza kabisa mahusiano yeyote ambayo yangeweza kunirudisha nyumba kwenye nia yangu ya elimu na kazi pamoja na mafanikio.
Sijajua bado nitafanya nini lakini nitafanya maamuzi yangu mwenyewe kwani mwishoni mimi ndiye nitakuwa na familia na sio mtu mwingine. Naotoa somo tu hasa kwa wale wadogo zangu.