Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,664
This is deep and very relatable. Mimi nilienda kupiga boksi nikiwa bado teenager. Kwa hiyo kimsingi nimeanza kuishi peke yangu mbali na wazazi wangu nikiwa na umri mdogo sana.
Kwa watu ambao hawanijui, wanaweza kudhani labda nimekulia kwenye mazingira fulani ya kudekezwa hivi. La hasha! Maisha ya Marekani kama huna skills za maisha ni magumu sana hususan ukiwa bado mdogo.
Nisingekuwa na nidhamu, hekima, busara, na common sense basi leo hii ningekuwa nimeshafulia kabisa na huenda hata ningekuwa jela au marehemu.
Lakini nashukuru kubahatika kurithi sifa bainishi ya common sense kutoka kwa mmoja wa wazazi wangu (nadhani kama siyo mama mzazi basi atakuwa babu mzaa mama).
Peer pressure ni kitu kibaya sana. Nimeona jamaa wengi sana waliokuwa wanabeba boksi waliopotoshwa na hizo pressure na sasa maisha yao hayana mbele wala nyuma.
Hii observation nayo iko on point sana hususan hiyo namba mbili. Kwa watu analytical na observant kama mimi, hii sifa ni baraka na laana.
Binafsi huwa nachanganua hadi cadence ya mtu. Na kwenye observation huwa naenda mbali mno hadi najistukia mwenyewe.
Hivi kwa mfano tu, ni nani humu huwa anajaribu kuangalia kama mwanamke ana nose hair zilizochomoza? Na kama anazo kwangu ni kama deal breaker flani hivi.
Kwa hiyo nakuelewa kabisa unaposema wakati mwingine ukitumia akili (na ukiwa na akili sana) kwenye mapenzi si vizuri kabisa. Kila utayekutana naye utamwona ana kasoro tu na labda hakidhi vigezo vyako na blahze blahze kama hizo.
Kuna jamaa zangu wengi wanaishi Boston, sijui ndio nyie!