kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 20,142
- 24,432
Ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa..Manara anapata wapi ujasiri wa kuisemaea yanga..Manara ni nani kwenye uongozi wa yanga...Manara ndio mratibu mkubwa wa mambo ya kitoto kwa kisingizio cha utani wa jadi...Manara anasahau kama anadhalilisha watu....juzi kati alimdhalilisha askari magereza...Manara amedhaliisha sana na kutweza utu alipokuwa simba..hili la Manara kuita waandishi na kuisemea yanga kama kiongozi na kuishambulia Tff kama atakaliwa kimya tutajua amepata baraka na ametumwa na viongozi tutajumuisha wale makomandoo pia walitumwa na uongozi ni vyema yanga wakamkana mara moja Manara...Amekwenda mbali na kuudhalilisha uongozi wa yanga Hersi na wengineo kuwa ni waoga na wasio na uwezo kwa kuwa tu wana uhusiano wao mwingine na karia na waoga wa kufungiwa kwa kuwa hawana kazi nyingine zaidi ya soka ila yeye kwa kuwa hana cha kupoteza na ana miradi tofauti hana shida..Je ni kweli Manara katumwa kubwabwaja na viongozi..ni dhahiri shahiri uongozi kama utakaa kimya basi waliwatuma makomadoo na kuwapa baraka za kuzuia simba kufanya mazoezi bado utoto..upuuzi unaendelea yanga!