Press conference ya ACT-Tanzania

Chadema buriani, kwaheri ya kuonana tuliwapenda lakini ubaguzi na ubinafsi umewapenda zaidi.
 
Kuanzishwa kwa ACT ni ishara mojawapo ya kuthibitisha madhaifu ya watanzania!

Vyama legelege uleta viongozi legelege wanaotoka miongoni mwa watanzania legelege!
Kwa mwendo huu taifa nalo litazidi kuwa legelege!
 
Nasikia waanzilishi wa ACT wote ni wale waliokuwa watukutu kwenye vyama vyao vya awali, wameanzisha chama kipya baada ya misukosuko ya kisiasa kutoka huko kila mmoja alikotoka.
 
Chagadema ishakufa mapema subiri matokeo kalenga muone na kule chalinze mshindi kashapatikana.

Unaposema "kufa" una maana gani. Nijuavyo kufa ni kitendo cha kutokuendelea kuwepo. Mtu akifa ina maana hatuwezi kumuona tena. Chama kikifa ina maana kitakuwa hakipo. CDM ina madiwani karibu 500 nchi nzima. Ina viongozi wa vitongoji kibao. Kukosa kushinda kalenga hakukiui Chama. Kujenga chama hadi kushinda chaguzi sio kazi nyepesi. Inawezekana kwa nchi ambazo zimeamka. Tanzania bado watu wake wamepumbazwa na mfumo dume wa CCM na wasiojua haki zao. Itachukua muda. Hadi vijana watakapochukua jukumu la kupiga kura na kuwaacha wazee kutuchagulia viongozi
 
Chapokua hujafuata standards za sheikh Yahya ila una tija.
Huwezi tumia lugha ya kigeni unaacha lugha yako ya Taifa halafu useme Tanzania kwanza!
Jina linareflect mwelekeo wa chama,sasa hawa masalia wanatumia kiingereza ilhali raia wengi hawakijui,sijui wanaficha nn!
Nyota? Kwa nn hakuna msalaba kuonesha ukombozi?
 
Nicolaus,

Utabiri wako unafanana na UKWELI ingawa kwa wenzetu ni mchungu.

Vyama vya kuchukua nchi TZ hii ni CHADEMA au CCM kama USA ilivyo REPUBLICANS na DEMOCRATICS. Sio mbaya wasindikizaji huwa wapo pia.
 
Nani waanzilishi wa hiki Chama wadau?
 



...Mfuasi wa Zitto aanzisha chama:



Dar es Salaam.Chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimeanzishwa na kupewa usajili wa muda huku kikitamba kuwa mbadala wa vyama vyote vilivyopo sasa kwa maelezo kuwa vimekosa demokrasia ya kweli.
Miongoni mwa viongozi wa muda wa chama hicho ni Samson Mwigamba aliyetimuliwa uanachama wa Chadema kutokana na kuhusishwa na waraka uliotaka kumwandaa Zitto Kabwe kuwania uenyekiti wa chama hicho.
Mwigamba aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, alitimuliwa pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo, huku uanachama wa Zitto aliyevuliwa nyadhifa zake zote zikiwamo za Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ukisubiri kesi aliyofungua mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwigamba alisema mchakato wa kuandikisha wanachama mikoani kwa ajili ya kuomba usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria umeshakamilika.
Alisema kimepata wanachama katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Hata hivyo, alisema kimechagua mikoa 10 ambayo Msajili wa Vyama vya Siasa atakwenda kuhakiki kama sheria inavyoeleza kabla ya kupewa usajili wa kudumu.
“Kama tutafanikiwa kupata usajili wa kudumu mapema, tunatarajia kushiriki kwa nguvu zote katika chaguzi zote ndogo zitakazojitokeza, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani,” alisema Mwigamba.
Alisema bendera ya chama hicho itakuwa na rangi ya zambarau inayoashiria haki, heshima na uadilifu na rangi nyeupe inayonyesha uwazi na usafi.
“Katikati ya bendera inayozungukwa na rangi zambarau kuna nyota mfano wa chama kinachojitokeza katikati ya vyama vingi inayokuja kutatua matatizo ya wanyonge yaliyowakabili kwa kipindi kirefu,” alisema Mwigamba na kuongeza:
“Pembeni mwa bendera hiyo kuna misitari ya rangi ya dhahabu inayoonyesha rasilimali zetu, rangi nyeusi zinazoashiria sisi ni Waafirika.”
Alisema hivi sasa hakuna kiingilio katika kujiunga na chama hicho na kwamba mara baada ya kupatikana kwa katiba, ndipo suala hilo litakaposhughulikiwa sambamba na kiingilio.
Mwenyekiti wa chama hicho, Kadawi Limbu alisema ACT - Tanzania kinaamini katika demokrasia jamii na kina shabaha kuu ya kupigania na kusimamia mabadiliko na uwazi ambayo ni lazima jamii inufaike nayo.
Alisema ACT-Tanzania kinaongozwa na msingi mitano ambayo ni: uzalendo, usawa, uadilifu, demokrasia ya kweli, uwazi na uwajibikaji vitu ambavyo vyama vyote vya siasa nchini vimeshindwa kuvisimamia kwa vitendo.
“Hakuna chama hata kimoja chenye demokrasia ya kweli na hii inatokana na vyama kuanzishwa na watu kwa malengo yao. ACT-Tanzania inakuja kuwafuta machozi wanyonge wote kwani vyama 21 vilivyopo vimeshindwa,” alisema Limbu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) na kuongeza:
“Watu wameipora demokrasia, wanyonge wanahangaika kutafuta usawa katika huduma za jamii kama elimu, afya na nyinginezo. Sisi hatutakubali, tutahimiza usawa kwa kila kitu.”
Msajili wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi alithibitisha chama hicho kupata usajili wa muda na kusema kipo katika hatua za kusaka usajili wa kudumu.
 
Mleta uzi kumbe na sisi WAHA tumeanzisha ACT? Kwanza niweke wazi si kila anayeishi Kigoma ni Mha, ingawa kwa asili waha ndiyo wengi huko Kigoma. Naamini hata ZZK hakuchaguliwa kule Kigoma Kaskazini kwakuwa ni Muha. Leo aende na hiyo alama yake ya nyota akawaeleze wapiga kura wake ina maana gani. Nasikitika kwa huu mgawanyiko ambao ZZK anaendelea kugawa taifa letu kwa tamaa tu ya madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…