Pres. Magufuli: Don't Put Your Sub-ordinates on Short-Leashes (ala Kilango)

Pres. Magufuli: Don't Put Your Sub-ordinates on Short-Leashes (ala Kilango)

Asante mkuu kwa hoja zako murua. Napenda sana mtu anaekushamiri (engage) kifikra. Inaonesha anakuheshimu.

Sasa katika utawala, kama umerithi timu ya bosi wa zamani basi unaweza kuwatimua watu unavyopenda.

Lakini unapoanza kujenga timu yako mpya hii ina maana unawatathmini vizuri unaowaleta kama wanafaa. Hapa ni muhimu kujenga uaminifu (loyalty). Kama mtu uliemleta hajafanya kosa la kuiporomosha timu yako basi timu nzima inapaswa kujua kuwa bosi atakuwa pamoja nao katika majaribu madogo madogo.

Kusipokuwa na hii team-loyalty, aghalabu timu husambaratika. Hiki ndio ninachojaribu kumuasa raisi.
Sawa sawa mkuu....hapo kwenye ujengaji timu...ni kuwa unaweza ukawa unajenga timu mpyaa lakini wachezaji wakawa ni wale wale...kwa mfano mchezaji au kocha anaweza asiwe mpya mchezoni lakini akawa mpya kwenye timu...na usajili wake kwa kocha makini utakuwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na utendaji wake wa timu aliyotoka...lakini hiyo pia haimpi guanrantee ya kuendelea kubaki kwenye timu mpya isipokuwa utendaji wake mzuri ulimfanya kocha amlete hapo....wapo makocha au wachezaji waliokuwa na viwango vya juu na vya kutukuka huko walikotoka lakini wakashindwa kuonyesha ubora wao kwenye timu mpya...na ili kulinda heshima na ubora wa timu uongozi ukalazimika kuwaondoa kwenye timu....huku kukifanyika jitihada za kuziba nafasi zao....
 
Sikubaliani na mleta post hata kidogo, kwamba kitendo hiki kitaenda kuua creativity and innovation za subordinates wa JPm..
Wewe ulitaka Mtu akionyesha creativity and innovation ktk kudanganya na kukwepa majukumu avumiliwe....!!???
Kwamba viongozi wetu watashindwa kufanya au kutoa maamuzi magumu na muhimu kwa kuogopa kutumbuliwa.....
Naomba nikukumbushe kiongozi mmoja tu aliyefanya maamuzi yenye kuonyesha creativity and innovation na akasapotiwa.
RC MAKONDA, kaagiza wenye silaha wote wahakikiwe, JPM alikuwa wa kwanza kuhakiki silaha yake kutii agizo la RC.Natafsiri kitendo kile kama Ku- promote creativity and innovation. Baadhi walitafsiri kama SHOW OFFS.
Wewe ulitaka avumilie kiongozi Muongo na asiyetimiza wajibu wake, amwite amsihi, ambembeleze, then what!!!???...
Hayo ndiyo aliyofanya Mkwere tukafika haha tulipo fika.
Kitendo hiki kinaujumbe mzito, ujumbe sahihi kama ule aliotuma kipindi alipotoka kukaguliwa Silaha.

Tuchukulie wewe sasa unateuliwa na rais Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Vipi imekuingia hiyo?

Haya, tueleze ni kipi utakipa kipaumbele? Utasubiri Magufuli akupe jukumu la kwaanza la kufanya (wafanyakazi hewa, madawa ya kulevya kwa vijana, kodi migodini, kuua vikongwe kwa tuhuma za uchawi, ...) au utajipangia mwenyewe?

Je, kama utakosea hesabu ya kiasi cha ukwepaji kodi migodini kwa asilimia 50 itakuwa sawa ufukuzwe kazi?

Hii ni mifano ya kijinga lakini nadhani itakupa kina cha utashi wangu niliposikia Mh. Kilango katimuliwa kisa hakujua ana wafanyakazi hewa.
 
diplomasia ndo iliyotufikisha Hapa lengo la JPM ni Ku uproot system iliyozoeleka ya business as usual na kufanya kazi kwa mazoea so watendaji serikalini wabadilike hiyo ni alarm rais hatanii aisee yupo serious
 
Sawa sawa mkuu....hapo kwenye ujengaji timu...ni kuwa unaweza ukawa unajenga timu mpyaa lakini wachezaji wakawa ni wale wale...kwa mfano mchezaji au kocha anaweza asiwe mpya mchezoni lakini akawa mpya kwenye timu...na usajili wake kwa kocha makini utakuwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na utendaji wake wa timu aliyotoka...lakini hiyo pia haimpi guanrantee ya kuendelea habaki kwenye timu mpya isipokuwa utendaji wake mzuri ulimfanya kocha amlete hapo....wapo makocha au wachezaji waliokuwa na viwango vya juu na vya kutukuka huko walikotoka lakini wakashindwa kuonyesha ubora wao kwenye timu mpya...na ili kulinda heshima na ubora wa timu uongozi ukalazimika kuwaondoa kwenye timu....huku kukifanyika jitihada za kuziba nafasi zao....

Tukiendeleza metaphor hii ya timu.

Wewe ni kocha mpya. Umemrudisha kiungo wa zamani na kumpa elekezo kuwa akifika golini ampasie striker wa kuaminika. Alipofika golini akajaribu kufunga goli lakini hakufanikiwa. Kwa kosa hili moja kweli utamfukuza timu?
 
Kwani mfumo unaundwa na mazimwi au individual....??
Kama mfumo unaundwa na Individual ajianze yeye aliyemuuzia nyumba hawara yake. Mbona mnakuwa wanafiki hivi? Yeye mwenyewe jipu mnajipa upofu kama vile hamuoni. Barbara kibao kajenga hazimalizi mwaka mashimo kibao! Ajianze yeye kujitumbua. Au alipokuwa waziri alikuwa jipu na sasa ni Rais sio jipu! Si ni individual yule yule? Unamtazama kama Waziri, Rais au Magifuli? Sasa nadhani unaelewa ninaposema kuhusu mfumo na Individual!
 
diplomasia ndo iliyotufikisha Hapa lengo la JPM ni Ku uproot system iliyozoeleka ya business as usual na kufanya kazi kwa mazoea so watendaji serikalini wabadilike hiyo ni alarm rais hatanii aisee yupo serious

Katika lugha ya mtaani ninachomaanisha ni kuwa majipu yanapaswa kutumbuliwa - lakini sasa tutumie ganzi jamani.
 
Inategemea na timu ipo katika msimamo gani wa ligi...kwa timu yetu hii na hapa ilipo kwenye msimamo wa ligi hatutakiwi kuyavumilia makosa....
Tukiendeleza metaphor hii ya timu.

Wewe ni kocha mpya. Umemrudisha kiungo wa zamani na kumpa elekezo kuwa akifika golini ampasie striker wa kuaminika. Alipofika golini akajaribu kufunga goli lakini hakufanikiwa. Kwa kosa hili moja kweli utamfukuza timu?
 
Inawezekana watu wamechoka au inawezekana ni kwa sababu tu ya ushabiki (tumeshuhudia watu wakishangilia kila kitu) au yote kwa pamoja na matokeo yake watu tunashindwa kuelewa hoja ya msingi: watu kufanya kazi kwa hofu!

Hakuna jambo baya kama watu kufanya kazi kwa hofu! Ufanisi huwezi kupatikana wakati watu wana hofu! Ndani ya hofu unajenga tabaka la wafanyakazi wenye nidhamu ya woga!

Athari nyingine ya kuwajengea watu hofu ni kwamba itakuwa ngumu ku-outsource nje ya serikali! Sekta binafsi kuna very resourceful Tanzanians! Wengine wapo abroad na wote ni experts!

Watu kama hawa hata wakipata presidential appointment wanaweza kuchomoa!
 
You will stifle creativity & innovations in governance.

So, probably Hon. Kilango deserved it. However, such summary dismissals will scare your subordinates (ministers and below) to a point of being Zombies instead being your linchpins in perfecting your governance.

Kama kuanzia mawaziri hadi vigogo wilayani watakuwa na mtera wakiogopa kisu chako cha majipu basi utawala utakuwia mgumu sana. Wasaidizi wako wataogopa kutoa maamuzi magumu (na pengine yenye hitlafu hapa na pale - i.e., not to your liking) wakichelea kuumbuliwa na bosi.

Mkuu wa ngazi ya juu akiteleza muite (au waziri wako amuite) chemba na kumpa karipio la kirafiki (faragha) halafu mtie moyo (encourage) aendelee kuthubutu makubwa zaidi.

Hii fukuza-fukuza hii utakuja jikuta uko peke yako kifikra katika awamu hii ya tano. Watanzania wengi wangependa urudi tena 2020 na nina uhakika utarudi lakini tumia diplomasia sasa katika utawala wako.

Kila mtu sasa anajua kasi yako na nidhamu yako. Najua Rais you are not diplomatic in nature but you need diplomacy (in your rule) now more than ever. Unaweza kubaki na kasi hiyohiyo ulionayo bila kudhalilisha wasaidizi wako.

Ushauri kwako kama rafiki.
Well said!!! Lakini humu ndani utatukanwa mno.
Nimewahi kuuliza ni lini Mh amekuwa saint kiasi ambacho ukiaribu kutoa mawazo tofauti unaishia kushambuliwa?
Watanzania tumsaidie Rais na kumsaidia ni pamoja na kusema uliyoandika.
 
Wewe hasa ndie aliekuwa mlengwa wa bandiko langu.

Jamani jifunzeni lugha ya malkia. Hatuwezi kuwa washindani wa Kenya, Uganda, S. Africa, EU, USA, n.k., wakati ukiguswa na ung'eng'e tu basi domo linajaa zege.

Sasa najua lugha ya malkia inakupiga, hebu nieleze katika kiSwahili fasaha ni kipi hasa kilichokukwaza katika bandiko langu. - Tafadhal.
LOh ha haha hiyo ya kuunga unga unaona ndiyo lugha ya malkia, labda wa uwanja wa fisi !! U sound like le mutuz na lizaboni type !!!
Waziri husika lazima aheshimiwe, mwongozo ulitolewa, akaambiwa cha kufanya lkn yy analeta za kuleta na kukimbilia ktk press.
Unajua ni mikoa mingapi ilikosea nawalipoambiwa wakarekebisha ??
 
You will stifle creativity & innovations in governance.

So, probably Hon. Kilango deserved it. However, such summary dismissals will scare your subordinates (ministers and below) to a point of being Zombies instead being your linchpins in perfecting your governance.

Kama kuanzia mawaziri hadi vigogo wilayani watakuwa na mtera wakiogopa kisu chako cha majipu basi utawala utakuwia mgumu sana. Wasaidizi wako wataogopa kutoa maamuzi magumu (na pengine yenye hitlafu hapa na pale - i.e., not to your liking) wakichelea kuumbuliwa na bosi.

Mkuu wa ngazi ya juu akiteleza muite (au waziri wako amuite) chemba na kumpa karipio la kirafiki (faragha) halafu mtie moyo (encourage) aendelee kuthubutu makubwa zaidi.

Hii fukuza-fukuza hii utakuja jikuta uko peke yako kifikra katika awamu hii ya tano. Watanzania wengi wangependa urudi tena 2020 na nina uhakika utarudi lakini tumia diplomasia sasa katika utawala wako.

Kila mtu sasa anajua kasi yako na nidhamu yako. Najua Rais you are not diplomatic in nature but you need diplomacy (in your rule) now more than ever. Unaweza kubaki na kasi hiyohiyo ulionayo bila kudhalilisha wasaidizi wako.

Ushauri kwako kama rafiki.
Uko sahihi, ila kwa huyu aliyefukuzwa alistahili hiyo adhabu.

Hana adabu kabisa huyu mamake Le Mutuz
 
JPM anatufundisha kuwa ni kosa kubwa kumdanganya Rais wa nchi. RC Anna Kilango alifanya kosa kubwa kuwaamini Wakurugenzi wa Halmashauri kwasababu hawa wamezoea mambo ya usanii. Hakuna muda wanakuwa serious katika kazi zao.

Wakurugenzi wa Halmashauri siku zote ni sifa tu.

JPM = SOKOINE = TANZANIA YENYE NEEMA!!!!!
 
LOh ha haha hiyo ya kuunga unga unaona ndiyo lugha ya malkia, labda wa uwanja wa fisi !! U sound like le mutuz na lizaboni type !!!
Waziri husika lazima aheshimiwe, mwongozo ulitolewa, akaambiwa cha kufanya lkn yy analeta za kuleta na kukimbilia ktk press.
Unajua ni mikoa mingapi ilikosea nawalipoambiwa wakarekebisha ??

Inaelekea hata kiSwahili kinakupiga. Huyu "Waziri husika" hasa ni nani unaemzungumzia? Nimeshindwa kukuelewa mkuu ingawaje mimi ni mzaliwa na mkulia uswahilini.
 
Mh. Rais Magufuli, wengi wanakusifia kwa kauli na matendo yako. Pengine wanakuogopa kukushauri moja kwa moja wakihofia kutofautiana na wewe.
Lakini kumbuka akutakiae mazuri atakukosoa daima.

Kuna kauli tata umekuwa ukizitoa ambazo kwa kiongozi hapaswi kuzitoa kwa watu anaowaongoza, sina haja ya kuzirudia, bali unazifahamu mwenyewe.

Tafakari kwa makini na ufahamu kuwa mtumishi ni binadamu, na ubongo wa binadamu huwa na tabia na hulka ya kuganda na kufunga kwa kiingereza wanasema "Freezing and Shutting Down" pale unapokuwa umeelemewa na vitisho vyenye kukatisha tamaa.

Nafahamu, unayo nia njema ya kukomesha Ufisadi, Rushwa na uzembe, na ninakuunga mkono.

Lakini kaa chini utafakari kuwa Uongozi wa nchi ni zaidi ya kutoa Maneno makali mbele ya Luninga na Vyombo vya habari.

Ukiendelea hivyo, wasaidizi wako wote wataamua kutulia, wakikuacha wewe kama main player, wakihofia kutofautiana nawe, watakuwa wanafanya kitu kinaitwa, "go slow" yaani mgomo baridi.

Jifunze kufanya encouragement pia.

Nakushauri kama Mwananchi Mzalendo.
 
Nimezinyaka kwamba mgomo umeanzia kwa mawaziri
 
Back
Top Bottom