Pres. Magufuli: Don't Put Your Sub-ordinates on Short-Leashes (ala Kilango)

Pres. Magufuli: Don't Put Your Sub-ordinates on Short-Leashes (ala Kilango)

Ukiendelea hivyo, wasaidizi wako wote wataamua kutulia, wakikuacha wewe kama main player, wakihofia kutofautiana nawe, watakuwa wanafanya kitu kinaitwa, "go slow" yaani mgomo baridi.

Serikali ya Magufuli ni ya kwenda mbio speed ya kilomita 1000 kwa saa ukiwa ni GO SLOW au una mgomo baridi jiandae kufunga virago utafute shughuli ingine ya kufanya lakini sio kubaki kuwa mfanyakazi wa serikali.Wako watanzania kibao tena vijana wasomi wa uhakika wenye uwezo wa kuchukua nafasi yako.

Kwa ufupi usijifanye hata uko frustrated na kazi ya serikali ikakufanya ufanye kazi chini ya kiwango kwa ajili ya frustration ni kujipa tiketi ya kuondolewa kazini.Kama unaona ajira ya serikali haikufai kwa vile ulivyozoea jiondoe mwenyewe upesi tena haraka.Magufuli keshasema waliozoea kufanya kazi kwa mazoea kimbunga kitawakuta.
 
Ingekuwa enzi zile za Mwl tungekuita Kibaraka wa Makabaila!
Muda wa kubembelezana umekwisha! Tunahitaji huo Mgomo baridi kama Watu walikuwa wanapiga kazi lakini
Hospital hakuna dawa
Kila mtumishi ni Mungu mtu!
Huduma za Maji, umeme n.k ni mbovu. Acha tuone wakigoma hali itakuaje kama walikuwa hawapo kwny mgomo lakin huduma zinatolewa kama wamegoma vile!
 
Hapa Kazi mabadiliko ya kweli ulijua nini? wakigoma fukuza tu watu wapo kitaa hawana ajira,mambo ya kubembelezana yameshaisha hapa kazi tu.
 
Jifunze kufanya encouragement pia.

Mchapakazi yeyote duniani hahitaji kutiwa moyo na mtu yeyote duniani.Kama ni mkulima atajiamkia mapema atachapa kazi ya kilimo ya kufa mtu bila kuhitaji encouragement ya mtu awe jirani,raisi au yeyote.Akiwa mfanyakazi atachapa kazi bila kusubiri encouragement ya mtu.

Ni mijitu mivivu,isiyo mibunifu inayokaa kaa tu ndio inahitaji kubembelezwa.Ikifanya kazi ndogo tu inataka isifiwe sana.Kama uko kwenye hilo kundi na uko serikalini nakuhurumia utaondoka.Ukienda kazini chapa kazi utiwe moyo usitiwe moyo chapa kazi afterall ndio maana unalipwa mshahara .Mshahara huo ndio encouragement yako.
 
Yani mbebwe msibebeke eti unatutisha na mgomo baridi?
 
Mlizoea kubebwa safari hii, kutoka nje ya mstari tu, treni inakuacha tuko speed sana. Ukitaka kujua speed ya awamu ya tano muulize mama yetu ma-malecela na RAS wake. Namshauuri Rais wetu akusanye CV za watanzania wote nchi nzima awe nazo,na tena ikiwezekana awape kazi Delloitte wawafanyie usaili wote wenye vyeti nakuwafanyia ranking.Tuanzishe Taasisi inayojulikana kama HUMAN RESOURCES BANK OF TANZANIA(HRBOT) hii itaondoa kiburi cha wafanyakazi kujiona wao zaidi.Mfanyakazi akichemsha Rais achota mtu kutoka benki kuu.Hii pia itasaidia kujua watanzania wangapi wasomi hawana ajira.Pia itasaidia kuanza kuuza vipaji nje kama Kagame anavyofanya kwa strategy ya TTT( Tujiendeleze Twende nje Tukatafute kazi)
 
Majizi yaliyoifirisi nchi hii yanataka kuonewa huruma. Nyie mbona hamkuwahi kutuonea huruma?

Hakuna wa kuleta mgomo baridi, hutaki kufanya kazi acha mara moja, watanzania wapo wa kutosha watafanya kazi.
 
Nimeipenda sana concept hii "....you are not diplomatic in nature but you diplomacy (in your rule)"
 
Wewe huna lolote
Kwanza naona kama Rais anawalea Upumbavu
Nenda kaseme live hayo maneno kama huendi kulima mchicha

Unataka turudi nyuma!!! Haiwezekani
 
Mlizoea kudekezwa na awamu zilizopita, huyu ndo raisi wa watanzania hakuna kuchekacheka, viongozi wakibembelezwa nchi hii haitaenda watanzania wengi hatujitumi tumezoea kufanya kazi kwa kusimamiwa. "Magu waoneshe maujuzi"
Hawa watu hawa fai kuishi Tanzania
 
Wakileta MGOMO baridi tupa kulee [emoji23] [emoji23] [emoji23] si wakati wasiasa huu
 
Mh. Rais Magufuli, wengi wanakusifia kwa kauli na matendo yako. Pengine wanakuogopa kukushauri moja kwa moja wakihofia kutofautiana na wewe.
Lakini kumbuka akutakiae mazuri atakukosoa daima.

Kuna kauli tata umekuwa ukizitoa ambazo kwa kiongozi hapaswi kuzitoa kwa watu anaowaongoza, sina haja ya kuzirudia, bali unazifahamu mwenyewe.

Tafakari kwa makini na ufahamu kuwa mtumishi ni binadamu, na ubongo wa binadamu huwa na tabia na hulka ya kuganda na kufunga kwa kiingereza wanasema "Freezing and Shutting Down" pale unapokuwa umeelemewa na vitisho vyenye kukatisha tamaa.

Nafahamu, unayo nia njema ya kukomesha Ufisadi, Rushwa na uzembe, na ninakuunga mkono.

Lakini kaa chini utafakari kuwa Uongozi wa nchi ni zaidi ya kutoa Maneno makali mbele ya Luninga na Vyombo vya habari.

Ukiendelea hivyo, wasaidizi wako wote wataamua kutulia, wakikuacha wewe kama main player, wakihofia kutofautiana nawe, watakuwa wanafanya kitu kinaitwa, "go slow" yaani mgomo baridi.

Jifunze kufanya encouragement pia.

Nakushauri kama Mwananchi Mzalendo.

Wewe unampa ushauri kama nani umetumwa? Acha propaganda na huna sababu yoyote ya kumpa ushauri maana tayari umeingiza dhana ya woga
 
Huyu mpuuzi katumwa huyu au kaumizwa! My president mbele kwa mbele wananchi tupo nawe achana na haya magarasa!
 
Back
Top Bottom