Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Kumekuwa na tabia za kutumiwa meseji za kitapeli kwenye simu za mkononi upande wa meseji za kawaida. TCRA wameweza kuzi block meseji hizo. Kwa sasa ukituma meseji ya kawaida yenye ujumbe ndani yake una neno FREEMASON sms hiyo haiendi! Watu wengi wamelizwa kwa kudhani meseji hizo ni za freemason kweli kumbe matapeli. Hongera sana TCRA. Fanyeni hivyo na meseji zingine zote za kitapeli mfano; meseji za bahati nasibu, meseji za iyo hela tuma kwenye namba hii jina litatoka fulani, meseji za kutongozana, meseji za mikopo ya kitapeli nakadhalika.
Nawapongeza sana TCRA.
Nawapongeza sana TCRA.