Mkuu, wewe na watanzania wengine mnanishangaza sana, kweli kabisa unaamini kuwa KQ walinunua 49% shares kwa ajili ya kuua shirika!!? Seriously?
PW haikuwa competitor mkubwa wa KQ only kwa safari ya Nairobi ambayo players wakubwa wakati huo walikuwa ni ATCL na KQ, then kwa woga gani KQ wamwage mabilioni kununua shirika ili waliue wakati sio mshindani wao. Unatilia mashaka uwezo wa BoD wa KQ kwamba kwa ujinga wao waliruhusu such a dubious merge!? Mimi siamini hivyo, naamini kuwa kwa KQ, PW ndo ulikuwa strategic airline kuinunua kwa ajili ya kuingia soko la Tanzania na walifanikiwa vilivyo in terms of operations. Kwangu Mimi kama mteja mzuri enzi hizo naona makosa yao makubwa ilikuwa zile trip za Lubumbashi na Lusaka na ile ya Johannesburg ambayo ilikuwa usiku sana na hivyo ilikuwa na abiria wachache. Huwezi kulaumu ambition aliyokuwa mayo Alfonse Kioko kuanziaha hizo safari kwa vile CEO yoyote mzuri lazima aangalie expansion of operations. Tofauti na ma CEO watanzania wengi hawafanyi risky decisions kwa kuogopa kulaumiwa, na hii ni Kansa katika kila sekta ya nchi hii hadi huko kwenu kwenye siasa. Mtamlaumu Kioko but wengine tunampongeza kwa kujaribu ingawa haikulipa.
Sauda Rajabu aliingia kwa kulaumu kila kitu cha Kioko. Strategically soko la ndani la Tanzania kwa safari za Mwanza, KIA na Mbeya zinahitaji mid size aircraft kama Boeing 737 au Airbus A320, lakini Sauda alipoingia akaanza kwa kurudisha Boeing walizokodi akabakiza ATR peke yake ambazo abiria tunaziita Bajaj. ATR kwa Dar Mwanza ni saa mbili na dk 10, wakati ile Boeing yao ilikuwa saa moja na dk 10, tayari umetumbukiza saa nzima kwenye safari, nani anataka hivyo? Pili kuondoa Boeing kijinga jinga kukasababisha upungufu mkubwa, kukawa na delays haijapata kutokea, ndipo loyal customers kama Ulukolokwitanga walipojitoa kupanda ndege za PW na abiria wengine kibao. Pia PW tradition ya entertainment ndani ya ndege ikaondolewa kupunguza gharama, watu tulikuwa tunagonga hadi bia, tukaanza kupewa maji kwenye viglass vya plastic. Kingine Saida ameshindwa ni kuangalia soko linataka nini, ameshikilia ATR ambazo abiria hatuzipendi zinatuchelewesha, niache kupanda JET ya ATC unatumia fk 70 au Airbus ya Fastjet dakika 90 nikapanda ATR ya dk 130 tena kwa bei kubwa mno ukilinganisha na wengine, no way. Dhambi kubwa kabisa ya Sauda ni kutengeneza hesabu za uongo kuipatia kampuni hasara feki ili shareholders wasilipwe na kuihadaa serikali iwapatie ruzuku kubwa ya $30M, a Bernard Madoff kind of thing...
I like PW, naombea wabaki kutuhudumia, lakini nikiwa kama abiria naona kama wamejimaliza wenyewe, tusimsingizie mkenya.