Nimejikuta nimesoma hii ripoti kama asilimia 80.
Inasikitisha sana..Inaonesha ni kwa jinsi gani watu walivyokuwa binafsi.. Mameneja wamepindisha sheria ili tu wajilipe karibu milioni mia mbili (200,000,000) kila mmoja.
Yaani HR anatakiwa aende jela moja kwa moja kwa kutafsiri mikataba vibaya....eti anasema Chief Accountant 'was not happy with the payments'...pia anasema alipaswa awajibike moja kwa moja kwa Director of Finance ambaye pia alimuonya CA kwa nini hakulalamika kwake instead akaandika barua kwa DG..
Watanzania wenzangu, hizi hela ni nyingi sana. Hebu fikiria mtu anafanya kazi ya mkataba kwa miaka mitatu or so, anaondoka na mamia ya mamilioni, halafu anaajiriwa tena kwa kuongeza mkataba, akitegemewa kulipwa tena hayo mamilioni kwa mara nyingine..
Sina mengi ya kusema, lakini huwezi kuamini Tanzania ni maskini, kwa jinsi watu wanavyojua kula pesa..tutapiga sana kelele, lakini watu wanakula nchi kiulaini kabisa.
Ajira zenyewe za kupeana.. mtoto wa Saidi Mwema, Musiba, n.k! Sijui, lakini ningependekeza mtu achukue maamuzi mazito kwa faida ya nchi.