Posta yataka vyama vya wafanyakazi kuhimiza wafanyakazi kutimiza wajibu wao

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Kaimu Postamata Mkuu Macrice Daniel Mbodo amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania kushirikiana na uongozi wa Shirika katika kuhakikisha wafanyakazi wanatimiza wajibu wao katika utekelezaji wa malengo ya Shirika.

Wito huo umetolewa tarehe 17 Julai, 2021 alipokuwa na kikao na Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Bara na Zanzibar, katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Mbodo ametumia nafasi hiyo kuelezea mpango mkakati wa Shirika kwa mwaka 2021/2022, ikiwa ni pamoja na kuongeza masoko kwa kutafuta na kutumia fursa mpya za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Aidha, katika kikao hicho Mbodo amewaeleza viongozi wa wafanyakazi mwelekeo wa Shirika katika kipindi hiki cha maendeleo ya kiteknolojia na namna ambavyo Shirika limejipanga kiutekelezaji hasa katika maeneo matano ambayo ni usismamizi wa rasiliamali watu, utawala bora, utoaji wa huduma kwa wateja, kusimamia kazi za msingi za Shirika, utendaji na ufanisi wa usimamizi wa fedha.

“Tumekutana hapa leo ili tujadiliane na tuangalie nini mwelekeo wa Shirika kwa mwaka 2021/22 hasa katika maeneo haya matano ili tutembee pamoja na tuwe na mwelekeo unaofanana, kwa sababu naamini viongozi wa wafanyakazi ni viongozi kama tulivyo sisi”. Alisema Mbodo

Pia ameongeza kuwa Shirika limejipanga kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kuboresha utendaji kazi na kuhakikisha Shirika linatoa huduma kulingana na mahitaji ya umma.

Mbodo amesema, ndani ya miaka mitano ijayo anataka kuona Shirika la Posta linafanya vizuri zaidi duniani na kuongeza kuwa Posta imekuwa moja ya taasisi kubwa nchini yenye kuleta tija kwa taifa.

"Shirika la Posta ni Shirika lenye Mtandao Mpana sana, limeunganishwa na Ofisi zaidi ya 600,000 kote Duniani, ambazo zote zipo chini ya Umoja wa Posta Duniani, kwa upana huo Shirika linaweza kufikia wananchi wengi kwa wakati mmoja”. Alisema mbodo

Kwa upande wa Meneja Mkuu Rasiliamali za Shirika Aron Samwel ameeleza kuwa, kwa sasa Shirika liko kwenye maboresho makubwa ya kiutendaji hasa kwa upande wa mifumo yake ili kuhakikisha Shirika linatoa huduma stahiki kwa wananchi kama inavyotarajiwa.

“Hatujakaa kimya maboresho ya mifumo yetu yanaendelea kufanyika na tunafanya kazi usiku na mchana kulishughulikia hilo”. Alisema Aron.

Naye Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara Constantine Kasese ameongeza kuwa Shirika linaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ambapo kwa sasa tayari mchakato wa kuagiza magari 13 ambayo yatatumika kuwezesha shughuli za usafirishaji umeshaanza.

“Tumepata kibali cha kununua magari na tayari mchakato umeshaanza, niwatoe hofu Shirika linaendelea kuboreshwa kila siku”. Alisema Kasese.

Kikao hicho kilihuhudhuriwa Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara, Meneja Rasilimali watu, Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na baadhi ya wawakilishi wa wafanyakazi.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania;
17 Julai, 2021.

IMG_20210718_142627_104.jpg

IMG-20210718-WA0076.jpg

IMG-20210718-WA0078.jpg
 
Hivi inafanya kazi gani siku hizi?!.

Tangu yawepo mashirika binafsi posta na simu. Naiona hii ya umma ikifa kifo cha mende
 
POSTA YATAKA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUHIMIZA WAFANYAKAZI KUTIMIZA WAJIBU WAO

View attachment 1858298

View attachment 1858299

View attachment 1858300
Naunga mkono hoja

P
 
Kuliko kuzuia wengine wasifanye / mfanye wenyewe kwanini msiwaachie wafanye pia ila nyie muwe bora zaidi?

Unadhani kuna atakayependa kumpa konda kifurushi kama nyie mgekuwa manaaminika na more efficient? Lakini Hapana... mnataka kuziba mianya yote mbaki nyie tu msioweza kazi (let the customer decide) sio vikwazo mara vibali mara sijui nini?
 
Shirika la Posta Tanzania wapo vizuri Sana siku hizi...!! Kuna mabadiriko makubwa Sana katika mfumo mzima wa uendeshaji wa Shirika la Posta Tanzania. Tembelea ofisi zilizopo Karibu nawe Ili ujionee mabadiriko hayo ya utoaji huduma
 
Naunga mkono hoja

P

Kabisa maana shirika la Posta Tanzania linatoa huduma zake kisasa zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Hongera Sana kwake Kaimu PostaMasta Mkuu ndg. Macrice Daniel Mbodo kwa hatua anazozichukua za kuboresha shirika la Posta Tanzania kwenda katika ushindaji wa kiutendaji Kati soko la kutoa huduma zake kwa wananchi
 
Shirika la Posta Tanzania wapo vizuri Sana siku hizi...!! Kuna mabadiriko makubwa Sana katika mfumo mzima wa uendeshaji wa Shirika la Posta Tanzania. Tembelea ofisi zilizopo Karibu nawe Ili ujionee mabadiriko hayo ya utoaji huduma
Hata ingekuwa bora kuliko ubora isitumie nguvu ya kuwazuia wengine ili ifanye peke yake (Monopoly)
 
Back
Top Bottom