Posta kutamu bwana, asikuongopee mtu.

Posta kutamu bwana, asikuongopee mtu.

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Dah, nilijikuta ghafla nimefika Posta ya zamani, acha ile mpya yenye makelele na mijengo mingi ya kisasa.
Pale kwanza kuna upepo bwana, wa bureeh! Afu kuna garden pale mbele ya NBC Corporate ambalo hata hulipi kuwako hapo, ingawa kuna viuchafu vya hapa na pale vya chupa za maji na maganda ya shikirimu, potelea mbali!
Cha bure huchagui bwana!
Yote tisa, kumi ni yale makundi ya raia wa Kiswahili wakicheza drafti na bao, kwanza hawana ubaguzi, hawaulizi kabila wala dini, mradi unasema lugha kama yao we unaliunga na stori zao. Wengi ni madereva taksi na mishen tauni, wanaujua mji vema sana, mtaa mpaka mtaa. Ukijiloga ukiwauliza eneo fulani, watakupa maelezo ya kina mpaka watakukera! Nilipata muda wa kujumuika nao, ni wacheshi, hawana ubaguzi hata kama ndo wanakuona mara ya kwanza, I mean hawakuulizi 'join date' au 'rep. power'?
Ah, Mungu Mwenyezi awazidishie viumbe wale...
Hivi nishawajuza kama pale kuna upepo wa bure eh? Miksa unasafisha macho yako kwa 'view' ya bandari na maji ya bahari, bila kusahau majengo imara ambayo umri wayo si haba ati?
Cha mwisho, hakuna kuchefuana pale, wale vijana wenye maisha ya 'bongo movies' wanaopatikana Mlimani City pale hawapo, kila mtu ni 'genuine' kama alivyo... Wala hautaona vi-skin vya kubana makalio na vitop vya kuacha matiti inje. Utamaduni wa Mswahili ungali na uhai fulani pale.
Hiyo ndo POSTA bwana,
afu ati watu wanalazimisha wengine wahamie Dodoma,
chezea Posta weye?
 
Ndiyo unafika Dar mara ya kwanza au umeamua tu kuchangamsha baraza.
 
Umepaeleza vizuri hadi nimetamani na mimi nikatembee huko. lol
 
Utamu upate vibabu vya kukuhadithia Dar zamani tangu jinsi lile kanisa la Azania lilivyojengwa pale 1903.
Pale palikuwa pazuri zaidi zamani kabla ya overpopulation ya Dar, ukienda mjini karibu kila mtu unamjua, huyu mnasoma naye, yule jirani yake mjomba etc.

Lakini ubovu wa enzi hizo ukikaa kaa tu mjini bila kazi polisi wa Sokoine hawachelewi kukukamata kama "mzembe na mzururaji" na kukupakia kwenye lori, unapelekwa Kinyerezi (eti Kinyerezi kulionekana mbaaaali siku hizo) Gezaulole na Kibugumo.

Siku hizi hata kupanda pantoni kwenda kuangalia Mikadi kukoje Magufuli anataka kukupandishia ushuru.
 
sijui unapafurahia nini maana mbele kuna kituo cha daladala mikelele kibao ya wapiga debe kwa kifupi hamna sehemu tulivu maeneo hayo
 
Dah, nilijikuta ghafla nimefika Posta ya zamani, acha ile mpya yenye makelele na mijengo mingi ya kisasa.
Pale kwanza kuna upepo bwana, wa bureeh! Afu kuna garden pale mbele ya NBC Corporate ambalo hata hulipi kuwako hapo, ingawa kuna viuchafu vya hapa na pale vya chupa za maji na maganda ya shikirimu, potelea mbali!
Cha bure huchagui bwana!
Yote tisa, kumi ni yale makundi ya raia wa Kiswahili wakicheza drafti na bao, kwanza hawana ubaguzi, hawaulizi kabila wala dini, mradi unasema lugha kama yao we unaliunga na stori zao. Wengi ni madereva taksi na mishen tauni, wanaujua mji vema sana, mtaa mpaka mtaa. Ukijiloga ukiwauliza eneo fulani, watakupa maelezo ya kina mpaka watakukera! Nilipata muda wa kujumuika nao, ni wacheshi, hawana ubaguzi hata kama ndo wanakuona mara ya kwanza, I mean hawakuulizi 'join date' au 'rep. power'?
Ah, Mungu Mwenyezi awazidishie viumbe wale...
Hivi nishawajuza kama pale kuna upepo wa bure eh? Miksa unasafisha macho yako kwa 'view' ya bandari na maji ya bahari, bila kusahau majengo imara ambayo umri wayo si haba ati?
Cha mwisho, hakuna kuchefuana pale, wale vijana wenye maisha ya 'bongo movies' wanaopatikana Mlimani City pale hawapo, kila mtu ni 'genuine' kama alivyo... Wala hautaona vi-skin vya kubana makalio na vitop vya kuacha matiti inje. Utamaduni wa Mswahili ungali na uhai fulani pale.
Hiyo ndo POSTA bwana,
afu ati watu wanalazimisha wengine wahamie Dodoma,
chezea Posta weye?

umeona eeeeh!!
 
sijui unapafurahia nini maana mbele kuna kituo cha daladala mikelele kibao ya wapiga debe kwa kifupi hamna sehemu tulivu maeneo hayo

msongamano
shombo za feri
vurugu za kugombea
daladala hasa mida
ya jion asee spendi kuwa huko labda
niwe na jambo muhim!
 
Umepaeleza vizuri hadi nimetamani na mimi nikatembee huko. lol

Tena uje na Yule Shosti wako Zinduna nawasubiri kwa hamu... Mkifika mje kwenye Maliwato ya Baharini ndo nachukua 200 za kijisaidia... Jibu mtakuja lini ili nijikoki siku hiyo...
 
Back
Top Bottom