Possible Intelligent Life out there

Haina shida. Nikipata nafasi nitatupia hapa hiyo kitu tuichambue.

Shukrani sana mkuu Mkuu Monstgala/Mgalanjuka
Kabla hatujaenda mbali ningependa nijue je tunapaswa kuiamini DRAKE'S EQUATION kwa 100%

.made in mby city.
 
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka nipo interested sana na hii elimu ya anga, kiufupi naipenda sana tangu nipo mdogo
Mkuu je naweza kusoma bachelor ya hii mambo?
Je ntasomea wapi?
Je ina dili kweli hii kitu au ndo nijiandae kuisoma kama hobie tu?
Kwasasa mimi ni mwanafunzi kidato cha sita PCM taker
Nategemea sana ushirikiano wako mkuu

Mkuu NICOLAX nasikikiaga sana hii kitu inaitwa DRAKE'S EQUATION hebu nipeni maujuzi kidogo na mm kabla hatujaenda mbali sana
Mkuu MONSTGALA uko wapi Mkuu?
 
100%? Aisee one thing you should know 100% is something that is not likely to be used in many scientific experiments as a result. Ni unrealistic, 100% ni kwamba katika hali yoyote matokeo yanayotarajiwa yatakuwa sawawasa bila kuwa na punje ya kasoro kitu ambacho ni rare.

Tukirudi kwenye Drake's equation sijui unajua kiasi gani lakini Drake equation ni hoja yenye probabilities. Katika parameters zinazounda equation hii, Drake ameweka makadirio mengi ambayo value zake hazina namba kamili bali range tu kutoka kiasi fulani mpaka kiasi fulani. Kwa hali hii huwezi kupata jibu ambalo litakuwa ni kamili bali litakuwa ni uwezekano tu na majibu mengi sana yanaweza pia kuwa matokeo ya kukokotoa equation hiyo. Hilo moja lakini pia equation yenyewe haikokotoleki kirahisi kwa maana parameters nyingi bado hazina majibu wala si rahisi kukadiria. Utaona bado hatujui kuna nyota ngapi zenye sayari katika Milkyway galaxy, hata average ya sayari zilinazoweza kusupport life katika galaxy yetu bado ni changamoto kujua kwa hakika lakini hata tukipata average na makadirio mengine ya parameters zote katika equation bado jibu la equation litakuwa too vague lakini at least liwe juu ya moja na si chini ya moja. Mfano kama N ambayo ni number of civilizations katika galaxy hii ni zaidi ya moja (+1), hii ina maana hatuko peke yetu. Lakini kama N ikiwa ni ndogo kuliko moja(-1) hii ina maana hakuna uwezekano wa kuwepo extra life katika galaxi hii, hivyo katika Milkyway lote na majinyota bilioni mia mbili kuna uhai katika Dunia tu.

Mfano rahisi kusaidia kumeza: Mtu mmoja mwanakijiji ana kuku wa blue peke yake anajaribu kujua kama kuna kuku wengine wa blue duniani. Parameters anazotumia ni kama ili kujua idadi ya kuku wa blue lazima ajue average ya wafugaji wote duniani, average wafugaji wenye kuku, sehemu ya kuku wenye uwezekano wa kutaga mayai yenye vifaranga wa blue, sehemu ya mazingira yanayopelekea kifaranga awe wa blue na labda muda wa unaotokana na yeye kupata habari hiyo kabla kuku hajachinjwa. Si mfano unaolingana lakini unaweza kupata picha ya equation hiyo ilivyo ngumu. Akiweka values ndogo za makadirio kwenye parameters zake atapata jibu negative kwamba chance za kuku wengine wa blue duniani hamna. Akiweka value kubwa kwenye makadirio yake katika parameter za equation atapata jibu kwamba kwamba kuna zaidi ya kuku mmoja wa blue. Jibu lolote linategemea values za parameters, bahati mbaya hana values hizo na ni mwanakijiji hana reseources za kufanya sensa ya wafugaji dunia nzima ili kupata angalau makadirio ya parameters zake. Kwa sasa kaangalia pale kijijini (Solar system) kaona hamna kuku wa blue wala mfugaji.

Ngumu zaidi ni kwamba Drake equation inaangazia intelligent life na sio just life maana inatakiwa viumbe wawe na uwezo wa kutuma signals au kufanya activity fulani ambayo vifaa vyetu vitaweza kudetect. Katika mifano hapo juu nimerahisisha tu lakini in reality life inayoangaliwa ni ile inayoweza kutuma ishara fulani ili sisi nasi tuzione tujue kuna wenzetu. Hapo utakutana na mambo magumu sana katika parameter za equation hii maana kuna suala la muda na uwezo wa kuwasiliana wa viumbe hao kama wapo. Lakini sio uwezo tu je wana interest ya kuwasiliana nasisi? Je kama mawasiliano yao ni tofauti sana na radio signals au any of which we have, how can we detect them? Au vipi kama ni mijidudu yenye kuwinda uhai mwingine katika galaxi hii na kuutokomeza alafu sisi hatujui tunatuma signals tu! Kwa hiyo hizo parameters nyingine mbili ambazo kwenye mfano wa kuku wa blue hazifit. Ni ngumu kuzikadiria lakini zipo na zinakadiriwa na tunakwenda mbele. SETI walichofanya na kuona uwezekano upo, kwa njia fulani lakini msingi ukiwa ni Drake's equation wakaona hebu tutume signals huko angani tusubiri majibu.

Drake equation haipo kutoa jibu lakini inajenga msingi na inafaa katika utafutaji wa maisha mengine katika galaxi, at least pa kuanzia. Kuna marekebisho pia maana wataalam wengine hawaoni baadhi ya vigezo muhimu na inakuwa si budi kuweka sawa au kuongeza baadhi ya parameters. Tunazungumzia galaxi moja tu (Milkyway) kwanza katika Drake kwa sababu ukiingiza next spiral galaxy kama Andromeda ugumu unakuwa maradufu. Ni kama yule mkulima hajafanya utafiti wa kuangalia kuku wa blue Duniani na anapanga kuangalia mwezini au vyote kwa pamoja. Sijui kama unanielewa mkuu, uliza tu kama hunipati.
 
Mkuu NICOLAX nasikikiaga sana hii kitu inaitwa DRAKE'S EQUATION hebu nipeni maujuzi kidogo na mm kabla hatujaenda mbali sana
Mkuu MONSTGALA uko wapi Mkuu?

drake-equation.jpg

armi nipo majukumu mengi, Lakini hebu ipitie kidogo hii na uangalie post hiyo nillomjibu Nicolax alafu twende mbele. Pia unaweza angalia vizuri wikipedia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka nipo interested sana na hii elimu ya anga, kiufupi naipenda sana tangu nipo mdogo
Mkuu je naweza kusoma bachelor ya hii mambo?
Je ntasomea wapi?
Je ina dili kweli hii kitu au ndo nijiandae kuisoma kama hobie tu?
Kwasasa mimi ni mwanafunzi kidato cha sita PCM taker
Nategemea sana ushirikiano wako mkuu

.made in mby city.

Nadhani hailipi kwa Tanzania. Kama unadhani unaweza kujiendeleza katika vyuo vya Marekani, Ulaya au nchi nyingine zenye program hizi unaweza kujaribu. ningekushauri soma bachelor program inayoweza kukukwamua kiuchumi na ukiwa na kipato kizuri unaweza kujiendeleza katika fani hii baadae.
 
Ahsante mkuu kwa ushauri, naomba nikusumbue tena
Je naweza nikapata scholarship kutoka kwa baadhi ya ORGANISATION zinazo husiana na hizi mambo popote duniani ??

.made in mby city.
 
Mkuu Monstgala kuna mada hapa jukwaani ulikuwa unazungumzia kuhusu aliens na category zao!!!..
Kwa Bahati mbaya siioni Ile thread!!,
Vp uliidelete au umeihamisha ukumbi!!,
Kama umedelete naweza pata zile notice make!
Pole Kwa kuchukua muda wako!!!
 
Mkuu naomba unisahihishe!
Ninavyo amini mimi kuna hii kitu inaitwa Godlock zone hapa si ndipo uhai unapopatikana?
Kama ndivyo me nahisi kila sayari itakuja kuwa na uhai.
Kwa kuwa jua lina zivuta sayari zote kuja kuja kwake
Hivyo sayari zote zitapita kwenye Godlock zone.na zitakuwa na uhai.

Evidence
Mars kufanana kwakaribu kabisa na dunia,kwa kua she is next to Godlock zone.

NB:
Watu wengi wanasema mars ilikuwa kama dunia but me ninavyo hisi Mars inaelekea kuwa kama dunia na sio ilikuwa kama dunia.

Mkuu naomba unisahihishe tafadhari.
 
Mkuu Mjuni Lwambo, Kwa lugha nyepesi, makadirio ya idadi ya nyota katika ulimwengu wote yamebase kwenye vigezo vya standard za observable universe. Hii ina maana average ya nyota katika galaxi moja [galaxi ziko aina tofauti na size tofauti, ndogo (dwarf galaxies) zinaweza kuwa na maelfu ya nyota kwa kila moja na zile kubwa kabisa (giant elliptical galaxies) zinakuwa na kuanzia trillioni moja mpaka trillioni mia moja kwa kila galaxi], eneo la universe ambalo ni miaka 13.8 bilioni ya mwendo wa mwanga,(Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.) kadirio la idadi ya galaxi ambazo ni zaidi ya bilioni 100 na kwa makadirio ya karibuni ni galaxi 170 bilioni katika observable universe.

Kwa lugha ngumu itabidi niweke calculations za wataalam hao jinsi walivyokokotoa hizi approximation. Sijui hii inatosha?

NB:Lakini pia inawezekana universe ni kubwa maradufu ya hiyo tunayoweza kupima au pia inawezekana haina ukomo (infinite).
mkuu unaweza ukaniambia uhusiano wa muonekano wa constellation sagittarius na katikati ya milkwaygalaxy(black hole-)
 
Nitajibu kulingana na mwandishi wa vitabu ambaye pia vitabu vyake vimejenga imani ya dhehebu langu. Anaandika na kusema, katika safari moja, alionyeshwa malimwengu mengine ambayo watu wake wanaishi pasipo dhambi, maana wao hawakukubali madanganyo ya shetani katika kipindi cha kutafuta makazi baada ya kutupwa toka mbinguni, na anaendelea kwa kusema, hata katika safari ya kwenda mbinguni, tutapita katika malimwengu hayo, ili waone namna mwana wa Mungu alivyofanya kazi kubwa kuokoa viumbe wake.

Ni biblia au nn?
 
Wanabodi,

Nimepata maswali mengi sana kuhusu dhana ya viumbe anga za mbali. Baadhi nitayajibu hapa kadri ya uwezo wangu.

Utata:

Wana-anga na wanasayansi wamekuwa wakiangalia mienendo ya nyota, sayari, miezi na vitu vingine vilivyoko mbali nasi(outer space) na hata jirani na Dunia yetu au katika ya mfumo wa Jua (Solar system) ili kuhakiki kama kuna maisha kwa sasa, au kuliwahi kuwa na maisha kabla. Baadhi, kwa mazingira zilizonayo maisha tuyajuayo hayawezi kutokea, hamna hewa, hamna ardhi , joto ni kubwa sana au dogo kabisa etc. Lakini pia baadhi ya sayari na miezi (moons) zina ardhi, atmosphere, na aina fulani ya kiwango cha hewa ingawa si sawa na uwiano sawia na ule wa Dunia.

Mbali na kuangalia sayari pia kuna utafiti wa ku-trace signals from outer space kama SETI na science institutions nyingine zile za wazi na za siri wanavyofanya na sasa ni muda mrefu utafiti wa aina hii unaendelea. SETI wanabase katika Drake's equation kutambua ni nini kinahitajika katika kujua maisha katika anga za mbali. Mbinu nyinginezo nyingi zinatumika kutafuta alama au ishara fulani ambazo zinaweza kuwa ni either mawasiliano ya viumbe hawa wenyewe kwa wenyewe au labda pia wao kama wanatafuta kujua kama kuna wengineo kama jinsi sisi tunavyodhani.

Msingi

Na kama tujuavyo ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana kutoka sisi tulipo katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia tano hadi ishirini (5% - 20%) ya nyota zote katika Universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona.

Sasa ukumbuke katika mada ile ya Ukweli wa kustaajabisha kuhusu Nyota, nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na Jua.

Kwa hiyo basi kama kuna nyota zinazoshabihiana na Jua, na pia zina sayari zinazozizunguka tena baadhi ya sayari zina mazingira kama ya Dunia. Kwa probability na scientific evidence, sayari zinazofanana na jua ni lukuki hii inafanya pia uwezekano wa kuwepo Earth-like planet au sayari zifananazo na Dunia kuwa mkubwa. Kama kuna sayari nyingi zenye ardhi na zenye mazingira yanayofanana na dunia basi inakaribisha zaidi dhana ya kuwepo uhai sehemu nyingine katika ulimwengu.

Cha kushangaza:

Hamna ushahidi uliotangazwa "wazi" kuhusu kuonekana kwa viumbe wengine/uhai so far kutoka kwa institutions hizi, serikali za nchi au mamlaka nyinginezo. Lakini theoretical views, scientific projections, personal claims, and philosophical reviews zinaleta information nyingi tofauti kuhusu possible intelligent beings out there.

Wanaofikiri kuhusu dhana ya viumbe vingine nje ya sayari yetu hawatarajii sana kuwepo na binadamu wanaofanana na sisi, viumbe wa kawaida au uhai kama tunavyoujua. Ingawa hilo linawezekana lakini kumbuka kisayansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia mia na sisi. Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.

Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake.
Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza mapema au baadae hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wengine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu au vice-versa. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa ku-evolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa au walitokea mamilioni ya miaka kabla yetu alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.

Pili, kama kuna viumbe wataweza kufika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo wa nyota panya au nyota kundi. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa.

Kwa kuwa maswali yaliyoulizwa yamekuwa na uwigo tofauti basi ni vyema kuyajibia hapa kwa ujumla wake, pale nipatapo nafasi au mtu mwingine ajuaye achangie.

Karibuni.

CC: juve2012 kadoda11 NICOLAX fyddell mtoto wa mjini neo1 Mjuni Lwambo Eiyer CYBERTEQ

..Mkuu kwanza sio Godlock ni Goldilock,na ni kweli unachokisema kuwa hio zone inasupport Life but concept ya sayari kuvutwa towards the sun haina maana Ya kwamba we are moving miles closer to the sun tupo hapa hapo na tutabak hapa hapa since a GoldiLock zone Ina intervals no more life itakua created popote pale
 
Life ni condition ambayo inatokea pale mazingira fulani yanapokuwepo. Mazingira fulani ya kuruhusu uwepo wa uhai inaweza kuwa ndio chanzo cha uhai wenyewe. Na inafahamika maji na Oxygen zipo hata nje ya sayari yetu na sio elements pekee kwamba zipo duniani tu. Na dunia hapo zamani haikuwa na uhai na ilikuwa sayari isiyoweza kuishi uhai kutokana na mazingira yaliyokwepo then it makes sense.

Kama kuna billions of stars with billions of solar systems it can be possible kuwepo kwa another existence of life supported by its own environment na katika its own evolution depending on its environment and its adaptation.

Its just an assumption, hata anayesema hakuna uhai sehemu nyingine its just an assumption too.
 
Wanabodi,

Nimepata maswali mengi sana kuhusu dhana ya viumbe anga za mbali. Baadhi nitayajibu hapa kadri ya uwezo wangu.

Utata:

Wana-anga na wanasayansi wamekuwa wakiangalia mienendo ya nyota, sayari, miezi na vitu vingine vilivyoko mbali nasi(outer space) na hata jirani na Dunia yetu au katika ya mfumo wa Jua (Solar system) ili kuhakiki kama kuna maisha kwa sasa, au kuliwahi kuwa na maisha kabla. Baadhi, kwa mazingira zilizonayo maisha tuyajuayo hayawezi kutokea, hamna hewa, hamna ardhi , joto ni kubwa sana au dogo kabisa etc. Lakini pia baadhi ya sayari na miezi (moons) zina ardhi, atmosphere, na aina fulani ya kiwango cha hewa ingawa si sawa na uwiano sawia na ule wa Dunia.

Mbali na kuangalia sayari pia kuna utafiti wa ku-trace signals from outer space kama SETI na science institutions nyingine zile za wazi na za siri wanavyofanya na sasa ni muda mrefu utafiti wa aina hii unaendelea. SETI wanabase katika Drake's equation kutambua ni nini kinahitajika katika kujua maisha katika anga za mbali. Mbinu nyinginezo nyingi zinatumika kutafuta alama au ishara fulani ambazo zinaweza kuwa ni either mawasiliano ya viumbe hawa wenyewe kwa wenyewe au labda pia wao kama wanatafuta kujua kama kuna wengineo kama jinsi sisi tunavyodhani.

Msingi

Na kama tujuavyo ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana kutoka sisi tulipo katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia tano hadi ishirini (5% - 20%) ya nyota zote katika Universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona.

Sasa ukumbuke katika mada ile ya Ukweli wa kustaajabisha kuhusu Nyota, nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na Jua.

Kwa hiyo basi kama kuna nyota zinazoshabihiana na Jua, na pia zina sayari zinazozizunguka tena baadhi ya sayari zina mazingira kama ya Dunia. Kwa probability na scientific evidence, sayari zinazofanana na jua ni lukuki hii inafanya pia uwezekano wa kuwepo Earth-like planet au sayari zifananazo na Dunia kuwa mkubwa. Kama kuna sayari nyingi zenye ardhi na zenye mazingira yanayofanana na dunia basi inakaribisha zaidi dhana ya kuwepo uhai sehemu nyingine katika ulimwengu.

Cha kushangaza:

Hamna ushahidi uliotangazwa "wazi" kuhusu kuonekana kwa viumbe wengine/uhai so far kutoka kwa institutions hizi, serikali za nchi au mamlaka nyinginezo. Lakini theoretical views, scientific projections, personal claims, and philosophical reviews zinaleta information nyingi tofauti kuhusu possible intelligent beings out there.

Wanaofikiri kuhusu dhana ya viumbe vingine nje ya sayari yetu hawatarajii sana kuwepo na binadamu wanaofanana na sisi, viumbe wa kawaida au uhai kama tunavyoujua. Ingawa hilo linawezekana lakini kumbuka kisayansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia mia na sisi. Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.

Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake.
Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza mapema au baadae hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wengine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu au vice-versa. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa ku-evolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa au walitokea mamilioni ya miaka kabla yetu alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.

Pili, kama kuna viumbe wataweza kufika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo wa nyota panya au nyota kundi. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa.

Kwa kuwa maswali yaliyoulizwa yamekuwa na uwigo tofauti basi ni vyema kuyajibia hapa kwa ujumla wake, pale nipatapo nafasi au mtu mwingine ajuaye achangie.

Karibuni.

CC: juve2012 kadoda11 NICOLAX fyddell mtoto wa mjini neo1 Mjuni Lwambo Eiyer CYBERTEQ

mmh mambo makubwa haya.
 
kujiangaisha kote huko kwa wanadamu,na kuishughurisha akili kiasi kikubwa namna hiyo ni kwa7bu ya HOFU YA KIFO TUU...!!!...siachi kusema wanadamu tumepewa akili kwa ajili ya kudadisi na kujipambanulia mambo ktk mazingira tuishiyo......
mungu ni mkubwa.....

Sent from my HUAWEI G750-U10 using JamiiForums mobile app

Sory! HV wana anga wanapoenda ktk uchunguzi huko juu! Ndani ya kile chombo wanabeba na Misosi kama ugali,wali au pizza?????
 
Nadhani kutakuwa na vyakula vyao maalum mkuu
Wabebe ugali huo mda wa kwenda toilet kila saa wataupata wapi
 
Wanabodi,

Nimepata maswali mengi sana kuhusu dhana ya viumbe anga za mbali. Baadhi nitayajibu hapa kadri ya uwezo wangu.

Utata:

Wana-anga na wanasayansi wamekuwa wakiangalia mienendo ya nyota, sayari, miezi na vitu vingine vilivyoko mbali nasi(outer space) na hata jirani na Dunia yetu au katika ya mfumo wa Jua (Solar system) ili kuhakiki kama kuna maisha kwa sasa, au kuliwahi kuwa na maisha kabla. Baadhi, kwa mazingira zilizonayo maisha tuyajuayo hayawezi kutokea, hamna hewa, hamna ardhi , joto ni kubwa sana au dogo kabisa etc. Lakini pia baadhi ya sayari na miezi (moons) zina ardhi, atmosphere, na aina fulani ya kiwango cha hewa ingawa si sawa na uwiano sawia na ule wa Dunia.

Mbali na kuangalia sayari pia kuna utafiti wa ku-trace signals from outer space kama SETI na science institutions nyingine zile za wazi na za siri wanavyofanya na sasa ni muda mrefu utafiti wa aina hii unaendelea. SETI wanabase katika Drake's equation kutambua ni nini kinahitajika katika kujua maisha katika anga za mbali. Mbinu nyinginezo nyingi zinatumika kutafuta alama au ishara fulani ambazo zinaweza kuwa ni either mawasiliano ya viumbe hawa wenyewe kwa wenyewe au labda pia wao kama wanatafuta kujua kama kuna wengineo kama jinsi sisi tunavyodhani.

Msingi

Na kama tujuavyo ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana kutoka sisi tulipo katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia tano hadi ishirini (5% - 20%) ya nyota zote katika Universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona.

Sasa ukumbuke katika mada ile ya Ukweli wa kustaajabisha kuhusu Nyota, nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na Jua.

Kwa hiyo basi kama kuna nyota zinazoshabihiana na Jua, na pia zina sayari zinazozizunguka tena baadhi ya sayari zina mazingira kama ya Dunia. Kwa probability na scientific evidence, sayari zinazofanana na jua ni lukuki hii inafanya pia uwezekano wa kuwepo Earth-like planet au sayari zifananazo na Dunia kuwa mkubwa. Kama kuna sayari nyingi zenye ardhi na zenye mazingira yanayofanana na dunia basi inakaribisha zaidi dhana ya kuwepo uhai sehemu nyingine katika ulimwengu.

Cha kushangaza:

Hamna ushahidi uliotangazwa "wazi" kuhusu kuonekana kwa viumbe wengine/uhai so far kutoka kwa institutions hizi, serikali za nchi au mamlaka nyinginezo. Lakini theoretical views, scientific projections, personal claims, and philosophical reviews zinaleta information nyingi tofauti kuhusu possible intelligent beings out there.

Wanaofikiri kuhusu dhana ya viumbe vingine nje ya sayari yetu hawatarajii sana kuwepo na binadamu wanaofanana na sisi, viumbe wa kawaida au uhai kama tunavyoujua. Ingawa hilo linawezekana lakini kumbuka kisayansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia mia na sisi. Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.

Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake.
Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza mapema au baadae hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wengine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu au vice-versa. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa ku-evolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa au walitokea mamilioni ya miaka kabla yetu alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.

Pili, kama kuna viumbe wataweza kufika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo wa nyota panya au nyota kundi. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa.

Kwa kuwa maswali yaliyoulizwa yamekuwa na uwigo tofauti basi ni vyema kuyajibia hapa kwa ujumla wake, pale nipatapo nafasi au mtu mwingine ajuaye achangie.

Karibuni.

CC: juve2012 kadoda11 NICOLAX fyddell mtoto wa mjini neo1 Mjuni Lwambo Eiyer CYBERTEQ
Mkuu Monsstgala Uko wapi siku hizi, tunamiss sana madini yako.

Mm ni mmoja wa wale tuliokuwa tunakufuatilia tangu enzi hizo.

Rudi mkuu uje kuendelea kutupa madini ya aina hii
 
Mkuu nimerudi, nashukuru sana. Napitia baadhi ya topics mpya za jukwaa hili nipate kuchangia lolote. Cheers..
 
Back
Top Bottom