Tumebakiwa na miaka michache tu tukutane na wenzetu nje ya dunia

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
1696074730536.png
Uzi huu unakusudiwa uwe ni endelevu na uwe unapokea taarifa mpya mpya kila huo muda unavyokaribia.Kwa sababu imeelezwa kuwa matayarisho yanaendelea kukutana na wenzetu nje ya dunia.
Wanasayansi wengi wanaamini kuwa zipo dalili nyingi zaidi sasa kuwa binadamu hatuko peke yetu kwenye ulimwengu wa cosmos.
Kwa upande mwengine maafisa wa CIA akiwemo mstaafu John Ramirez wanasema uwezekano huo ni mkubwa kutokana na idadi ya UFO ambao wameongezeka kuitembelea dunia.
John Ramirez ametoa hofu yake kwamba serikali ya nchi yake inaficha habari hizo na si jambo jema kwani watu wanatakiwa watayarishwe kuwapokea wageni hao badala ya kuja kuzuka taharuki wakiwaona ghafla karibu yao kwa mara ya mwanzo
Wanasayansi wanaofanya kazi kituo cha NASA hasa chumba cha mawasiliano ya kusikiliza sauti kutoka mbali wamesema kila siku wanajitayarisha kupokea sauti kutoka huko na japo bado hawajapata sauti zenye kufahamika vyema lakini wanahisi kuna dalili ya jambo hilo kutokea hivi karibuni na haitozidi miaka 20mpaka 30 ijayo.Tatizo la wazi wanaloliona ni lugha ya kujibu sauti hizo.
Zipo nyota zaidi ya bilioni 300 ndani ya galaksi ya Milky way ambako dunia imo ndani yake. Kila nyota inakisiwa ina angalau sayari moja mfano wa dunia.
Zaidi ya hapo tayari zimeshaonekana sayari 5000 nje ya mfumo wa Jua (Solar System). Zaidi ya galksi hii ya Milky way ziko galaxy nyengine zaidi ya bilioni 200 zilizoonekana kwa teknolojia ya sasa.
Darubini ya James Webb tayari imeweza kuona baadhi ya sayari zikiwa na gesi ambazo hutolewa na viumbe hai tu kwa hapa duniani.


1696074830009.png
 

Attachments

  • 1696074830243.png
    1696074830243.png
    68.4 KB · Views: 21
Utakua jambo jema.

Tunapaswa kuona viumbe wengine walio nje ya hii Dunia.

Hata Elon anasema 2030 ataanza mchakato tuhamie sayari ya Mars, mungu abakie na dunia yake sisi tutasepa.
 
Kama ilivyokua kipindi kile wazungu walivyokua wanahisi wako wenyewe kwenye hii sayari,ndio kinachoenda kutokea.
 
Back
Top Bottom