Nimeshangaa sana kusikia eti kuondoa posho kwa wabunge ni hoja ya serikali ya ccm kupitia mpango wa maendeleo wa miaka 5.Watanzania ni wepesi kusahau kwani Dr Slaa alishaahidi ktk kampeni.Kuweka suala la posho kwenye mpango huo ni kutekeleza ahadi za Dr Slaa kwa mlango wanyuma.
source:soma mwananchi la 11.9.2010 na habari leo 2.9.2010
[TABLE="width: 99%"]
[TR]
[TD]Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
Imeandikwa na Levina Kato; Tarehe: 2nd September 2010 @ 07:50 Imesomwa na watu: 1328; Jumla ya maoni: 11
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 310, align: right"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 98%, align: right"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[TABLE="width: 98%, align: right"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema, akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atashusha bei ya vifaa vya ujenzi ili kuwezesha wakazi wa Dodoma kujenga nyumba za kisasa na kuondokana na nyumba za tembe walizonazo hivi sasa.
Dk Slaa alitoa ahadi hiyo juzi, alipohutubia wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Winza Kibakwe wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.
Katika hotuba yake hiyo alisema atapunguza gharama ya saruji, mabati na bidhaa nyingine zinazohusika katika ujenzi ili kuwezesha watu wengi kuishi katika nyumba bora.
Akitania, Dk Slaa aliwaambia wananchi hao kuwa, rubani wake alipata shida kukiona kijiji hicho kwa sababu nyumba zote zimeezekwa kwa tope - tembe.
Imenichukua muda mrefu angani wakati rubani wangu alipokuwa akijaribu kutafuta kijiji chenu, hatukuona nyumba zenu, alisema Dk Slaa ambaye alifika kijijini hapo kwa helikopta.
Mwanasiasa huyo alisema, hawadhalilishi wakazi wa Kibakwe ila anawaeleza ukweli, kwamba wanapaswa kuishi katika nyumba bora.
Alisema, akichaguliwa kuwa Rais, Serikali yake itapunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika vifaa vya ujenzi hasa vinavyotengenezwa nchini, kama vile saruji, ili kuwezesha masikini kujenga nyumba bora.
Akitolea mfano, Slaa aliiambia hadhara hiyo kuwa serikali yake itapunguza marupurupu kwa wabunge na kuelekeza fedha hizo katika mfuko wa miradi ya maendeleo.
Ni dhihaka kwa wawakilishi wenu (wabunge) kupata fedha nyingi kutokana na vikao vya Bunge, wakati ninyi mnalala katika nyumba za tembe, alisema wakati akielezea nini atawafanyia Watanzania.
Katika hadhara hiyo pia Dk Slaa alimtambulisha mgombea ubunge Benson Kigaila ambaye aliahidi kujenga shule katika jimbo hilo, ili watoto wengi wa masikini wapate elimu, hasa wasichana.
Lakini akiwa Kiteto, Manyara jana, Dk Slaa alitoa ahadi nyingine kuhusu vifaa hivyo vya ujenzi, akisema akiingia madarakani atavifutia kodi zote zinazovigusa.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]