Posho za Ubunge nazo zifutwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za Ubunge nazo zifutwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 15, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Salaam,

  Posho za Vikao zinapingwa kwa sababu zinakataa mantiki- Mbunge kutokana na nafasi yake ni wazi atahudhuria vikao mbalimbali vinavyoendana na majukumu yake hivyo kumlipa posho kwa kuhudhuria vikao hivyo haiingii akilini na kama wengine walivyosema ni "wizi" wa wazi. Tukikubali mantiki hiyo lazima tuangalie kile kinachoitwa "posho ya Ubunge"

  Mbunge analipwa posho ya Ubunge kwa vile yeye ni Mbunge- sijui kama kuna Posho ya Urais au ya Udiwani! Na sina uhakika kama Madaktari wanalipwa "posho ya udaktari" na wahasimu wa serikali wanalipwa "posho ya Uhasibu" au yumkini kuna posho ya weledi fulani ambayo mtu analipwa. Siwezi kushangaa ipo posho ya "ualimu" au ya "udereva". Lakini kwa vile sijui hayo mengine nigusie hii ya "ubunge".

  Mbunge anapogombea Ubunge anagombea nafasi ya ajira na anapopata analipwa mshahara wa Mbunge. Siyo kazi ambayo alilazimishwa au kupewa baada ya kushikiliwa bunduki kichwani. Aliiomba kazi hiyo na alijua inakuja na majukumu mbalimbali. ni kwa sababu hiyo Mbunge analipwa mshahara na ameweka maslahi mengine tofauti kama Mbunge (mkopo mkubwa wa gari, nasikia wanajengenewa nyumba - sitashangaa wakauziwa kila mwisho wa term)). Lakini kumpa posho ya Ubunge tena!?

  Posho ya vikao iondoke na pamoja (siyo ikifuatiwa) na posho ya Ubunge kwani zote mbili zinakataa mantiki.
  POSHO ZA MADIWANI
  Mimi kama Diwani nalipwa (sio mshahara) kwa mwezi shilingi laki moja na ishirini (Tzs 120,000).

  Posho ya Kikao cha Halmashauri ni 50,000 x 4
  Posho ya Vikao vya Kamati 50,000 X 4
  Posho ya vikao vya ALAT 65,000

  POSHO ZA WABUNGE

  Posho ya mafuta 2500 kwa Lita 1000 = 2,500,000
  Posho za Kikao = 100,000
  Posho za ukarabati wa gari – 1,000,000
  Posho za Dereva – 400,000 (mbunge anaamua amlipe kiasi gani dereva)
  Posho za Jimbo – 450,000 (nje ya Mfuko wa Jimbo)

  (I stand to be corrected)
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  bora hata madaktari wangepewa posho kwa kuhudhuria au kuwepo hospitalini kuliko hawa wanasiasa ambao asilimia 80% ya ahadi zao hawajawahi kutekeleza au hazitekelezeki
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo ya ubunge ni ipi tena? Nadhani ni vyema aneyezijua posho wanazolipwa wabunge na kwa sababu gani atuorodheshee hapa ili tuzipime. Kwa mfano hivi sasa tunajadili suala la posho ya vikao na tumeona kimantiki haitakiwi kulipwa kwa sababu kukaa bungeni ni kazi ya mbunge. Nawe mkuu umekuja na hii ya ubunge mimi sijajua inalipwa kwa sababu gani au inalipwa kwa kuwa mbunge kama ambavyo ukiwa askari unalipwa posho ya chakula?

  Ni vema tukazijua posho zote tuzijadili na zinazostahili tuwaachie kama vile per diem japokuwa na yenyewe ina mgogoro kwa kuwa wengi wana nyumba zao dodoma. Hivi mbunge wa Dodoma mjini naye analipwa per diem?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye kikao cha Bunge Jummane (14[SUP]th[/SUP] June 2011), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba alinukiliwa na vyombo vya habari akisema kuwa serikali haina uwezo wa kujenga Reli ya Mchuchuma/Liganga-Mtwara kutokana na uwezo mdogo kifedha. Alisema mradi huo utagharimu kiasi cha dola 1.5 bilioni za Marekani ambazo ni sawa na Sh 2.250 trilioni kiasi ambacho alisema ni kikubwa kwa nchi ya Tanzania peke yake!

  Aliyeuliza hilo swali alikuwa ni Mh Mariamu Kasembe (mbunge wa Masasi- CCM). Sina shaka mbunge huyu atarudi jimboni kwake na kuwaambia wananchi ameuliza swali na serikali imesema haina fedha, lakini atendelea kuikumbusha serikali. Hata hivyo mbunge huyu anshindwa kuona kuwa yeye kama mbunge anachangia kutokuwepo kwa hii Reli.

  Hoja yangu ya msingi hapa ni kwambwa both Naibu Waziri na huyu mbunge (wote ni ccm) wanasahau kwa mwaka wabunge wanachukuwa takribani trillion moja kama posho ya kukaa kitako kwenye eneo la kazi! (0.9 trillion). Sasa kama serikali itakomesha ‘huu wizi' basi ndani y miaka miwili na nusu tu wanaweza kujenga hiyo Reli ya Mchuchuma/Liganga-Mtwara.

  Hii inadhihirisha wazi kuwa Tanzania haitaji kuwa ombaomba ila wabunge (na hasa wa ccm) wameshindwa au wamemua kwa makusudi kuendesha hii nchi kwa ‘umetonya' kwa sababu mapato ya nchi yanashia kwenye mifuko yao. You can see it very clear where the problem lies.
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye RED i ni milioni 5 kila mwezi wanalipwa kwa kuwa wabunge msharaha wao ni
  milioni 2 jumla inakuwa saba.

  ndio maana Zitto alipogonga sitting allowance walikuja juu maana wanajua mengi yanaweza kuibuka.
  hiyo milioni tano kama sikosehi inatakiwa kutumika kumlipia katibu wa mbunge mshahara wake
  lakini wabunge wetu hawana makatibu, makatibu wao ni wapwa zao lakini kiutaratibu alitakiwa kuwa mtu
  aliyemaliza kidato cha sita.
  kwa maana hiyo kila jimbo linatakiwa kuwa na katibu na mbunge wake ili wananchi wasikose mtu wa kusikiliza
  shida zao mbunge akiwa mjengoni.
  wabunge kwa kutumia hati miliki za majimbo walizojipatia wanaona kuweka katibu ni kama kujitengenezea mwaasi wa baadaye na
  kuchukuwa jimbo maana wengi wa wabunge wetu wameununua kwa bei kubwa sana.

  hii nchi ina wizi mwingi kwa sababu wabunge wetu wengi ni wachafu na wamekwenda mjengoni kutajirika, bora kuondaa haya maposho
  ili watu watakao gombea ubunge iwe kuwakilisha kweli na sio kutajirika.
  sera za chama chetu cha mapinduzi bado zinatumaliza TIME IS NOW kama hawafuti hizo posho za kujikimu dawa ni sisi
  wananchi kuwadai posho za kujikimu na hali ngumu ya maisha kama walivyofanya vyuo vikuu sasa watakula 10000
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mzee JF ingekuwa na critics kama wewe kumi hivi hadhi ya zamani ingerudi, umesema maneno makali sana ila yote ni ukweli mtupu. Tatizo linalotusibu wa Tanzania ni ubinafsi na hii inayoonekana kwa wabunge wetu ni reflection ya jamii nzima maana hawa si malaika kusema walishushwa ila ni wenzetu miongoni mwetu..
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapa kweli yataibuka mengi. 5 mill posho kwa mwezi. Hiyo rate imefikiwafikiwaje?
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hako ni kasehemu tu kwa watu takribani 400. Sasa ukiingia huko serikalini hiyo miposho ya vikao nadhani ni mara ishirini ya hiyo. Hii kitu itawaumiza wengi na ikipita itawasaidia wengi kama hiyo saving itatumiwa ipasavyo.
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  wewe unashanga hii subiria siku raisi mwenye uzalendo akiingia ikulu utashangaa KIKWETE alikuwa anavuta
  ngapi kwa mwezi,
  kama siko hela ya aibu usiri wa nini? kuna nchi first lady analipwa pia sasa sijui wakwetu inakuwaje.
  nje ya mikataba mibovu Tanzania tumefilisiwa na posho na misharaha mineno ya vigogo pamoja na wizi,
  mbaya zaidi hiyo hela wanapeleka kimagendo nje ya nchi badala ya kufungua miradi.
  ndio maana BOT kamwe hawataweza kuimalisha thamani ya pesa yetu ni kutoka na hawa hawa viongozi
  kuichimbia na kuipoteza kwenye mzunguko
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Naona mnataka kuua viongozi wetu lol! Hivi mnafahamu mtu mwenye tumbo kubwa akihisi njaa anakuaje? BTW hz pesa zichinjwe ipasavyo na kama wao walivyoshika bango la kujifanya ati viongozi wa set mindset za wananch kuhusu mipango ya maendeleo ya serikali vivyo hivyo na wao waset akili zao kwa dhati kabisa katika kupunguza matumizi makubwa ya Serikali na pesa za umma na kwa dhati kabisa wafahamu kuwa kwa mujibu wa katiba kazi yao ni kuisimamia serikali na si kuitetea serikali. Tukiendelea kwa mtindo huu tutaendelea kuwa na nchi ya posho tusikatae social stratification lkn kuwe na proportionality na accountability ya dhati.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hiyo "posho ya ubunge" kwa kweli ni mjumuisho wa posho mbalimbali zinazohusiana na kazi za ubunge; kama mshahara wa dereva (sielewi kwanini wabunge ndio watumishi pekee wa umma wanaoajiri madereva wao bila kusimamiwa na yeyote - hata Rais haajiri dereva wake!), posho za mafuta (nasikia ni lita 1000 kwa mwezi - haijalishi kama anatumia kiasi hicho au la) na viposho vingin.
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Welcome to The United Republic of Poshonia !!!
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kinachonichekesha ni pale baadhi ya wabunge na viongozi wa CCM na serikali kutaka kutuaminisha kwamba hatustahili kufahamu wabunge wanapata nini na is some sort of illegal kujadili mapato ya mbunge, waziri na hata raisi. This is where I salute democracy. This kind of a discussion would have never as it is by say 1995.

  Yaani wewe umeajiriwa na ajira umeomba mwenyewe unalipwa mshahara halafu tena sijui mafuta, usafiri, posho ya dereva, posho ya pombe, posho ya ulinzi, posho ya cheo etc. etc. Sasa mshahara ni wa nini? Basi nao ungechambuliwa kiposhoposho. Posho ya msosi, posho ya viatu, posho ya nguo etc.
   
 14. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Binfsi sioo Posho Napeda kuona proirity za serikali zinaenda mpaka kwenye Salary scheme.

  Sikubaliani na mfumo amabo mbunge ndo kuwa best paid public employee mkoani au wilayani.

  Alfu serikali inasema sera yake ni ya kilimo kwanza????? Mimi sioni hoja na sababu kwa nini mbunge awazidi hawa watu hata kwa

  • Afisa Elimu wa mkoa au wilaya
  • Mganga mkuu wa mkoa na wilaya
  • RPC au DSO
  • Mhandissi wa mkoa au wilaya
  • Bwana/bibi Nyuki au Afisa mifugo wa mkoa au wilaya
  Majukumu na wajibu wa hawa watu hapo yana umhimu mkubwa na ndio hasa watu wanatakiwa frontline uboesha maisha ya watu. Kutumia lugha ya dipmoasia tuseme lengo si kuwapunguzia wabunge lakini wabunge wahakikishe watu wenye majuumu sawa na wajibu sawa au zaidi yao wanapata zaidi yao au sawa na wao.

  Nitafurahi kusikia mbunge anauliza kwa nini waanawazdi mshara hao watu.?

  Na kama wanaiga wazungu waangalie uko katika mkoa au aijimbo who is best paid public employeee. Always sio politician. Lakini huku africa ni vice versa
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Posho zote pamoja na ruzuku kwa vyama vya siasa ni wizi na ujambazi usiovumilika. Tunaomba posho na ruzuku vifutwe mara moja.

  1.Mbunge ama mfanyakazi atayelalamika kufutwa kwa posho ajiwajibishe mwenyewe kwa kukubali kuwaachia wengine watao kubali fanya kazi chini ya mshahara husika.

  2. Chama cha siasa kitakacholalamika kufutwa kwa ruzuku ama kushindwa kujiendesha kwa michango ya wanachama wake, ina maana chama hicho hakikubaliki, ni halali yake kijifie, kwanini kuendesha chama kwa jasho la watu wengine ambao hawana vyama? Hii ni sawa na mahakama ya kadhi ama baraza la maaskofu kuendeshwa na kodi ya wananchi.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi sioni faida ya hawa wabunge.....tujenge mabweni ya kisasa dodoma,yenye vitanda na wapishi na wasafishaji pamoja na walinzi ili ku-create jobs,
  Watu waombe kwenda kufanya kazi msimu wa bajeti kupika na kusafisha hilo bweni,na kuwe na mabasi ya kuwapeleka bungeni,hakuna haja ya posho kama hawataki,watu wenye moyo watagombea ubunge kwani ni nafasi ya heshima sana haswa ukiwa unawafanyia kazi maskini walio vijijini.
  Kama tunataka maendeleo,inabidi tuionyeshe Africa,who is the real revolutionary!...tutaheshimika na tutaendelea.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  it could be a good idea, but hii ya kudandia-dandia kabla hoja moja haijaisha ndio moja ya prime reasons watanzania tunashindwa kwenda mbele... we want to lift both legs and still walk like human beings

  PESA INATUCHANGANYA SANA SIKU HIZI
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Hilo ndio tatizo letu,tunajua kabisa kuwa tulikuwa na wabunge wanaolipwa sawa na afisa utumishi na walikuwa wakifanya kazi zao kama kawaida,they were writing bills and turning them to acts and ultimately laws,designing policies na kupitisha bajeti tena wakati mgumu sana....na walikuwa na ma land rover ambayo huyaacha majimboni mwao,na tulikuwa tunapanda nao UDA kama kawaida wakiwa hapa Dar kwenye kikao cha bajeti,
  Wengi wao wakati nasoma forodhani walikuwa wananunua mihogo ferry kama kawaida......sasa nini kimebadilika? Usharobaro hauwezi kutufikisha popote pale,tutabaki kusifia mbunge wangu ana benz,hummer,BMW...mara ooh ipad,whateva!
  We don't need that!,...we don't need to think twice.
  Nilikuwa kwenye train moja na Elijah cummings,representative wa maryland,hana dereva.Representatives wa hapa US ni watu wenye chenji zao ila most of them wakiwa DC huwa wanakaa kwenye boarding houses....remember representative Stupak? kwenye obamacare?Walimbana kwa kuwa yeye na wenzake ambao wanaitwa K-street gang walikuwa wanaishi kwenye hosteli ya kanisa ambayo hailipiwi property tax(exempted),na Rachel maddow akajaribu kuunganisha uhusiano wa kanisa(K street hostel) na representative Stupak ambaye aliongoza democrats waliokuwa wanapinga Obamacare's support on abortion.
  Ni mfano tu kukuonyesha kuwa wenzetu huku wanakaa hostel na sio hotel(ambazo pia wana uwezo wa kukaa humo).
   
 19. T

  Taso JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Sasa kama hujui hao wengine wanalipwa au hawalipwi hizo posho, hapo unawa compare na wabunge au unafanya nini? What's the point? Why raise the issue of other professions' perks?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa hoja haijawekwa sawa; kuna watu wanaamini kuwa tatizo ni "sitting allowances" hivyo wakisikia sitting allowances zimefutwa basi kwao tatizo la posho linakuwa limekwisha pia. Tushughulikie tatizo zima - posho. Once and for all kwanini tufanye kwa vipande vipande?

  MkamaP amegusia suala la ruzuku - hivi kwanini vyama vya siasa vinapata ruzuku ili viweze kuja kututawala? Yaani badala ya kutoa ruzuku kusaidia makampuni na taasisi zetu ziweze kujijenga vizuri katika uzalishaji sisi tunatoa ruzuku ili waje kututawala? It makes absolutely no sense at all.
   
Loading...