Posho wanazojilipa Wakurugenzi na Mameneja huwa ni wizi mtupu! Bila kuzifuta posho hatutoboi

Tatizo huu mjadala wamejaa layman, eti posho ziondolewe hahaha hustle na wewe ufike levels hizo ambapo taaluma yako itaanza kukulipa kwa masaa. Mimi mwenyewe sijafika level hizo ila usiku na mchana nafanya juhudi nifikie huo uwezo ambapo taaluma yangu itaanza kujilipa yenyewe.
 
Hoja sio taaluma kuna watumishi wana masters Ila hawana hizo posho mfano mwalimu. Ila kuna watu wana certificate lakini wanakunja posho kibao sababu wako wizara ya fedha au BOT au TRA au hazinaa

Makampuni ya kigeni huwa wanashangaa sana na kuchoshwa na hili la posho.
Wanashindwa kuelewa hata mimi nashindwa kuelewa, eti kikao cha kujadili kazi zao waandaliwe na bahasha.

Vilevile bungeni, posho za kikao huku wana mishahara, kisha Africa tunataka tuwe kama ulaya, huku fedha zote zinalipa wachumia tumbo, haziendi kwenye miradi ya maendeleo.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Yaani posho ni nyingi kuliko mradi wenyewe
 
Wewe inaonekana huna elimu hata kidogo
Kama na wewe unajihesabu ni msomi basi elimu yako haina thamani bora wazazi wako wangenunua ngurue wafuge kuliko kupoteza hela kukusomesha huo ujinga bin sufuri!
 
Yaani mtu analipwa posho kwa ajili ya kuandaa ripoti ya kwenda bungeni? Kwanini alipwe wakati ndio kazi yake? Mama SSH hizo Posho zingepelekwa kwenda kuajiri watu wengine maana poshi zinazidi mishahara ya watumishi wa umma.
 
Mizizi wa haya yote chanzo chake ni bungeni kule tulikotuma wawakilishi wetu, mshahara 3.8m posho 8m kwa mwezi, akihudhuria kikao cha bunge kwa siku anakula 360k ambao ni mshahara wa mtumishi mwingne kwa mwezi, anapewa mafuta ya gari lita 1000 kwa mwezi na mkopo wa gari 90m, bima ya afya daraja la kwanza ambayo utatibiwa popote duniani na pensheni ya 250m ndani ya miaka 5.
Afu wakiwa bungeni wanajadili nguvu za kiume mamaye haya mambo yanatia hasira.
Ndio maana kila mtu anakimbilia bungeni aisee, ndani ya miaka mitano huu mzigo si unazidi 1 bi. kweli?
 
Hoja sio taaluma kuna watumishi wana masters Ila hawana hizo posho mfano mwalimu. Ila kuna watu wana certificate lakini wanakunja posho kibao sababu wako wizara ya fedha au BOT au TRA au hazinaa

Ualimu ni wito sasa unataka ulipwe sawa na Admininstrators? Kipindi wenzake wanachagua taaluma yeye hakuona hizo kozi za kusoma hadi akimimbilie ualimu ? Think big
 
Back
Top Bottom