Posho na Mishahara ya wabunge...

Kumbe wabunge wa Chadema ni wanafiki wakubwa nimeangalia TBC leo asubuhi, Mbowe na wenzake kumbe wamekopa pesa benki wamedhaminiwa na Katibu wa bunge kuna wengine wamekopa milioni 200, wengine milioni 150, watakuwa wanakatwa kwenye posho zao. Mbowe alitaka kukataa Lukuvi akamwambia mmechukuwa Mbowe kimya
Acha unafiki hivi kweli inakuingia akilini ukate tawi ulilikalia? Hiyo ni propaganda ya watu wa system kuwanukisha wote waliokimbelembele katika kudai kufutwa kwa posho, mosi ikiwa ni kutoa personal details zao ambazo hazina tija zaidi ya kuongeza ugumu wa kufika maamuzi.
Nakutahadhalisha nchi hii inahitaji revamp of the whole system, ni kama gari iliyonock. Hakuna boundary kati ya chama na uongozi! Katibu mkuu anakwenda kuwa katibu wa CCM n.k.
 
Tuseme mbunge kaugua kikao chote cha bunge huo mkopo analipaje? Tuwe tunafikiria wakati mwingine bana sio ushabiki tu!
Mkuu, bahati nzuri wabunge wa Chadema wanapita sana humu JF, itakuwa vyema kama watajibu swala ili, kweli wanakopa benki na mdhamini wao ni ofisi ya Katibu wa bunge
 
Wabunge wa Chadema wanafiki wanapinga posho kumbe hizo hizo posho ndio wachukulia mikopo
Hata kama ni kweli basi hiyo siyo dhambi watalipa kupitia vyanzo vingine. Lakini wewe mbona hujauona unafiki wa serikali ya JK total expenditure 8.6tril wakati Total Revenue 7.1tril kwa hiyo 1.5tril deficit! Wakati anajua kabisa akikata posho ata save .9tril na kubaki na deficit ya .6tril, jambo ambalo lingemletea ahueni ya kwenda kuomba kuomba kama matonya huko nje au kujiingiza katika mikopo isiyo ya lazima! Toa banzi kwenye jicho lako ndipo uone bolt iliyo katika jicho la mwenzio, mimi naamini kabisa serikali yetu ni ya kinafiki nafiki isiyojali na kazi yake kuu ni kuandama upinzani usipate nguvu ili waendele kutunyonya!
 
Acha unafiki hivi kweli inakuingia akilini ukate tawi ulilikalia? Hiyo ni propaganda ya watu wa system kuwanukisha wote waliokimbelembele katika kudai kufutwa kwa posho, mosi ikiwa ni kutoa personal details zao ambazo hazina tija zaidi ya kuongeza ugumu wa kufika maamuzi.Nakutahadhalisha nchi hii inahitaji revamp of the whole system, ni kama gari iliyonock. Hakuna boundary kati ya chama na uongozi! Katibu mkuu anakwenda kuwa katibu wa CCM n.k.
Mkuu, ebu tugande hapa kwenye ili ni kweli wabunge wa Chadema wamechukuwa mikopo benki mdhamini wao ni ofisi ya Katibu wa bunge na mikopo hiyo inalipwa kupitia Sitting allowance
 
Hivi ukiwa kama mfanyakazi uwe wa serikali ama binafsi watu wakopa kwenye mshahara ama kwenye Posho?? Naombeni kujuzwa
 
Na nyinyi wachangiaji wengine muwe na akili na ufahamu, we toka lini posho akakopea mtu mkopo?kwani huo ni mshahara wa mtu mpaka waruhusiwe kukopa kwa posho,wao kwa nini wawalazimishe zichukuliwe hizo posho wakati wenyewe hawataki,huoni kuna wapenda posho kuliko kazi.Watu wengine wa ajabu sana siku zote walikuwa wapi kutangaza huo mpango wao wa miaka 5 ijayo?na kama ndo mpango wao na wanawakopesha kupitia posho mbona bado waliruhusu tena wachukue hiyo mikopo.Magamba msituletee danganya toto,toeni hoja za msingi kwa Wtz
 
Zito amekiri suala la posho si la chadema, wala zitto ni la taifa... Na ndio maana ndani ya mapango uliopitishwa jana na bunge limo
 
Kimsingi ishu hapa sio flani kakopa au flani kaanzisha!Kama mtu aliyekopa na kukubaliana na mkopeshaji kuwa atamkata posho,na anaamua kukataa posho,kwa nini mkopeshaji akatae huku sheria za mikopo zipo?Kama cdm wanajua kuwa wamekopa na serikali inajua kabisa kuwa ni lazima deni lilipwe kupitia posho,na cdm haohao hawataki hizo posho kwanini serikali inakataa?Mi naona huu ndo mwanya wa kuwafunga wabunge wa cdm watakaokataa posho badala ya kuwakomalia kwa makosa ya kuwabambikia!Kingine cdm wanasema wanapinga posho kwa zote za wafanyakazi wa uma.Sidhani kama taasisi zingine za uma zinakopesha kwa dhamana ya posho,ni bunge tu.Kwa hiyo bado cdm wana hoja na serikali inachotaka kufanya hapa ni si'hasa'.
 
Umeelewa,wabunge wasiochaguliwa na wananchi wanatupotezea fedha zetu,hawana umuhimu kama sitting allowances zisivyo na umuhimu.
Hoja tosha

Hoja yako ni ya msingi mkuu. Viti maalum wanamwakilisha nani??
 
Mkuu hizo hesabu zako ni za wabunge tu hujaweka posho za vikao za watumishi wengine serikalini. Ukiziweka hizo nadhani utapata mamia ya mabillioni. Mkuu suala hili ni mtambuka halihusu wabunge peke yao. Ni vema kama wabunge watakataa posho za vikao na kuzifuta na pia zifutwe serikalini. Haiingii akilini kwamba hata vikao vya management watu wanalipana posho, vikao vya kamati mabalimbali wanalipana posho. Posho poosho posho kila mahala.

Mkuu ukikokotoa hesabu za watumishi wote wa serikali unaweza pata presha, Hapo bado pesa inayotoka kwa mgongo wa Extra duty kwa watumishi wa serikali.
Posho nying hazina mashiko ni njia ya kutunisha mifuko yao. Serikali haina dhamira ya kweli ya kuwaondolea watazania umaskini zaidi ya kuwaongezea
 
kama ni hvyo walikuwa wap cku zote?
mpaka CDM Waanzishe..kuhusu kutafuta umaarufu wote waungane na Zito ili wote wawe maarufu
 
Nilikuwa nikitizama Hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi kivuli Mhe. Zitto Kabwe.Wengi tunatambua kuwa yeye ndiye muasisi wa kuikana posho kuwa si halali na amekuwa akiiuza katika vyombo vya habari,sasa imekuwaje tena kuruka na kudai hoja hiyo kuwa si ya kwake ni ya Serikali.Zitto amesisitiza hili kuwa hoja imo ndani ya Mpango wa Serikali wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni kwa majadiliano na si yeye muanzilishi kiasi cha kusababisha Spika Anna Makinda kuingilia kati na kumwambia asome ya kwake anayopaswa kuwasilisha.

Hivi kwa nini Zitto kajitoa kwenye uasisi wa hoja hii,ndio tuseme ameikana baada ya kuona baadhi ya Wabunge wa Chama chake hawamuungi mkono kimyakimya.Pamoja na hayo bado Zitto anamsimamo wake wa kutopokea posho hivyo anataka kutushawishi kuwa alifanya hivyo baada ya hoja hiyo kuwasilishwa na Serikali katika Mpango wa Miaka mitano?
 
Mpango mzima ni kufuta na ruzuku ktk vyama vyote vya siasa, futa ruzuku kwenye vyama siasa na futa posho zote.
 
Back
Top Bottom