Kazi ya bunge sio kugawa pesa za posho kwenye majimbo yao. Wabunge are LEGISLATURES, meaning wanatunga sheria na kusimamia utendeji wa serikali, full stop. Siku hizi kumeibuka kasumba ya wabunge kuomba omba, kila kukicha wako kwenye balozi za nchi za nje hapa Tanzania pamoja na mashirika ya kimataifa wakiomba vitu vidogo vidogo. Yes, ni vizuri kwa wabunge kutafuta misaada lakini ni kweli serikali haiwezi kutatua haya matatizo bila omba omba ya wabunge?
Tuchukulie kwa mfano, kama wabunge bila kujali chama wangesimama imara na wakaiwajibisha serikali leo tusingekuwa na EPA, Richmond, IPTL, TICS etc. Wabunge wanaomba msaada wa USD 10 million (kwa mfano) wakati EPA ni USD 90 na ushee!!!! ndio maana wafadhali wanatudharau maan wanaona kabisa tunaacha hela zinaenda mifukoni mwa wachache lakini tunawasumbua na vibakuli kila kukicha.
Sasa kisingizio cha Chilligati kuwa wabunge wa CCM wanatumia posho kuwasaidia wananchi, hiyo siyo primary role yao wao wabunge. Kusaidia wananchi sio kutuleta pombe, kanga, mipira na t-shirt. ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi na serikali inatimiza wajibu wake. Maadam hilo wameshindwa sasa tunataka posho zikome. kabisa. Chilligati na wenzake watafute vianzo vingine vya kuwahonga wanachi pombe na t-shirt. Nasema posho mwisho.