Gabriel ZaChariah: Kugomea posho ni msimamo wa chama au mtu momja mmoja
Mbowe: Hapa tunaomba tueleweke kuwa dhana halisi ya issue hii ni ni Posho za watumishi wa umma, wabunge ni sehemu ya watumishi wa umma wapatao miatatu tu miongoni mwa watumishi wengi wa umma. Sasa magazeti yameotosha ukweli, sisi tunapinga sitting allowance ambayo dhana yake inatolewa kwa watu walioewa majukumu nje ya majukumu yao ya kawaida. Sasa watumishi wa umma wana mishahara, wanapokaa kwenye kazi zao za kawaida hawastahili kupewa posho na hii imeambukiza hadi kwenye halmashauri. Chadema tunasema posho hizi zinaharibu sana utendaji katika serikali, sasa nani kalisema kwetu sio issue bali ishu ni dhana nzima ya posho za watumishi wa umma
Gabriel Zacharia: Mheshimiwa Lukuvi,Unalisemeaje hili la Mbowe?
Lukuvi: Concept hii nzima hakuna anaeipinga. Kila mtumishi wa umma amepewa majukumu yake pamoja na malipo yake kwa mujibu wa sheria. Sasa matumizi yake ndio kitu cha kutazama. Hapa nipishane na Zitto, aliyesema posho ziangaliwe ni Mkulo. Serikali imesema wazi katika kipindi hiki itaipitia posho mbalimbali kwa watumishi wa umma ili zilete tija na kuziondoa zinazoondoa tija.ALICHOKOSEA ZITTO ni kulifanya jambo hili kama amelivumbua yeye.
Gabriel Zacharia: Mheshimiwa Mbowe unazungumziaje maelezo ya waziri?
Mbowe: Kulipersonalize kwa kumtaja Zitto ni kumuonea. Nimkumbushe waziri kuwa Viongozi wa serikali walilipinga hili mwanzoni. Suala hili wether kalisema Zitto au Serikalini kwa sasa halina maana kulipersonalise ila tujadili dhana halisi ya suala hili
Gabriel Zacharia: Zipo taarifa za uhakika kuwa Mheshimiwa Mbowe na wenzako wa Chadema mmeshakopa pesa hizi
Mbowe: Si kweli, kwanza mkopo ni haki ya mkopaji na ni makubaliano kati ya mkopajio na mkoeshaji. Posho za bunge ni sitting allowance na hutolewa unapokuwa kwenye kikao. Sasa kama sitakuja Dodoma sitapata hiyo posho sasa watanikopeshaje osho wakati sijahudhuria kikao? Kama ni kukopa unakopa kwenye mshahara wako na sio kwenye osho na kama mtu kakopeshwa kupitia osho basi tatizo lipo kwa mkopeshaji
Gabriel Zacharia:Mheshimiwa waziri unalisemeaje hili
Lukuvi:Concept nzima sio posho bali kupunguza gharama za serikali ndiomaana sasa hivi magari aina ya vx hayanunuliwi tena yananunuliwa GX.
Kuhusu kukopeshwa posho ni kweli walikopa na Mbowe alikopa ppia. Walikopa milioni mia mbili, mia hamsini , mia tisina saba kwa hiyo mh. Zitto na wengine wamekopa.
Gabriel Zacharia:Mbowe wakati mnakataa osho miongoni mwa wabunge wa Chadema wanapokea osho kwenye kamati?
Mbowe: sisi tunazungumzia kupunguza ghara za serikali lakini kujadili mbunga fulani kapokea posho au fulani hapokei ni ishu ndogo sisi tunataka wote kwa pamoja tujadili ishu ya msingi, tusipoteze muda kujadili jambo lisilo na tija
Gabriel Zakaria: kwanini msiige alichokifanya waziri mkuu kwa kukataa VX akapokea GX ingawa Mbowe yeye anaendesha VX?
Lukuvi: Tupe muda tumedhamiria kupunguza gharama ndani ya miaka mitano tutakuwa tumepunguza gharama za serikali
Tanesco washachukua chao