Porokwa apasua jipu la CCJ

Porokwa apasua jipu la CCJ

Mkuu kimsingi nimeiweka tu habari kama ilivyoandikwa, lakini pia kuna kauli tata hapo ambazo Porokwa "alinukuriwa alivyooongea".

Ndio maana nikakuuliza wewe Butola ni lini Umeanza Kumuamini Kubenea na Gazeti lake linalodaiwa kumilikiwa na Komu? Swali langu hujalibu kwa makusudi kabisa kwa sababu unafahamu nini linalenga.

Je Unamsadiki Kubenea? Kama ni Kweli Umeanza Kumsadiki leo baada ya Porokwa Kuwataja akina Sitta?
 
Usilete hoja zilizo cheap kabisa. Msajili hawezi katika orodha yake kuwa na wote wanaoanzisha chama. Mapema miaka ya 90 mimi (na mamia Wtz wengine) nilihudhuria mkutano pale diamond jubilee Hall ulioanzisha NCCR-Mageuzi. Lakini jina langu halikuwapo katika orodha ya msajili.


usitumie nguvu kutoa hoja yako. Kama majina yao hayapo kwa msajili, mwakyembe , 6 na nape wakikanusha, kimsingi mimi nitawaamini unless kama unaweza definition nyingine ya '
uanzilishi' mbali na ninayoijua mimi
 
mbombo ngafu....! eheee ikawaje tena......(yaani hadithi iendelee)
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Hii ni kuonyesha yafuatayo:-
  • Kwamba viongozi wetu kutoaminika.
  • Kwamba unafiki ndio unaowatawala.
  • Katika siasa hizi za kupakana matope...hao wanaotajwa wapo na hata kushika nyadhifa ndani ya CCM nao ni wasaliti wa chama chao.
  • Wawapo CCM huonekana ni wenye machungu ya chama chao...nyuma ya pazia sio kabisa.
  • Ni fursa ya dhana ya vua gamba waliyoiasisi...'kuwarudia na kuwatafuna' min'ghairi ya walionyooshewa vidole.
  • Kifuatacho kwa hao waanzilishi wa CCJ na bado wanahodhi nyadhifa kubwa za chama sasa 'wajivue gamba-wajiuzulu' ili kukiletea chama kuwa na watu waaminifu na wasiokisaliti.
  • Kwa wanavyoumbuana hivi...ni faida kwetu raia kuwatazama mara mbili viongozi wetu na mbio zao waombapo ridhaa za kutuongoza.
Hizi ndio siasa za Tanzania, nimesoma toleo la wiki hii la magazeti ya Raia Mwema & Mwanahalisi...ambapo wameongelea kwa kina waasisi wa 'mtandao' uliomuweka mkulu pale magogoni. Imewataja akina mzee Six, Jacka Mwambi na wengineo...na jinsi walivyoparanganyika baadae na kujawa na sintofahamu, SIASA ZA TANZANIA NDIVYO ZILIVYO, kweli kitengo cha propaganda cha system kinafanya kazi zake na sasa inaonekana.
 
Hapa hamna cha unafiki wala undumilakuwili! Huyo jamaa ni kundi la mapacha watatu na ametoka kule kwa Lowasa ndo maana ameamua kuwaponda kina Sitta.Nani asiyejua kuwa Sitta na wenzake wamepigwa vita sana ndani ya CCM mpaka ikafikia hatua ya kutaka kumfukuza? Ulitegemea asiwena wazo la kuchomoka ccm wakati anapigwa vita na maswahiba wa JK?

Mi sioni tatizo lolote kwa kina Sitta kwani hata wewe mwenyewe ungejaribu kuondoka.Huu mchezo mchafu ulioanzishwa na mapacha watatu umelenga kuwaokoa wao tu.Nawasapoti kina Sitta kwani wameonyesha uvumilivu wa hali ya juu kupambana na mafisadi ndani ya chama.Wasikatishwe tamaa na haya maneno ya watu waliokosa hoja! Sasa hivi watz wan hali ngumu ya maisha na migao ya umeme isiyokwisha hivyo tunahitaji ufumbuzi wa matatizo yetu!

Great thinker use your thinking!!!

1. Kwa kipindi Sita, Mwakyembe na Nape walipoa asisi CCJ walikuwan sahihi kabisa na ilihitaji ujasikri mkuu ...Lazima waheshimiwe kwa hilo. Hali ya nchi ilikuwa Tete mapacha watatu walikuwa wanayumbisha nchi na CCM yao!!
2. Wakati CCJ ilipokuwa ina asisiwa ilikuwa ni jambo muhimu na huwezi kuwaita wahaini watu waliokuwa wanafanya hivyo wakati huo.Ilikuwa muhimu na CCM ilikuwa inawajua na wengi walipenda CCJ ikomae na ifanye kazi lakini Mapacha 3 waliimaliza CCJ kwa manufaa yao..
3. Sababu za kuasisi CCJ ndio hizi zilizoleta Gamba Leo. Na mleta gamba wa kweli lazima alione hilo na aone umuhimu wa waanzishi wa CCJ
4. Bila CCJ hapangekuwa na Gamba leo...JK ataniunga mkono na watumie hawa jamaa kama unaniunga mkono.
5. Kikwete atawatumia hao mnaowaona hawafai sasa ..SITA, NAPE na MWAKYEMBE ni MTAJI kwa KIKWETE kwa kuendesha Gamba kampeni kwani Gamba ndio CCJ. nani haoni hilo?
6. Mapacha watatu kwa kuwa ndio waliolengwa CCJ na ndio wanolengwa na Gamba ...watafanya kila upuuzi wanoujua kuwamaliza Mapacha watatu wa CCJ aka Nape, Mwakeyembe Na Sita.
7. Nape, Sita na Mwakyembe waheshimiwe ... kwa kuanzisha CCJ NA GAMBA!!!
8. Kikwete watumie ....Kikwete watumie ...kikwete watumie...!!
9. Kiwete wachana na viporojo vya mafisadi wa CCM wanaowatisha na kuwasumbua mapacha wa CCJ
10. Nani anaujasiri wa kuanzisha CCJ pale CCM ..wote waoga... wale waliokuwa na uajsiri wa kujitena sio wahaini ni wajasiri ...watumike Gamba!! Kikwete analijua hilo na watanzania wanalijua hilo!!
 
mbombo ngafu....! Eheee ikawaje tena......(yaani hadithi iendelee)

hii sio hadithi, unafikra kongwe kama avatar yako, inawaza mambo ya mama na mwana wacheck rtd wanakutumia hadithi ...............
 
Huyu Nape usimsifie. Ni msaliti mkubwa...Aondoke kwenye chama chetu haraka sana...
 
NAPE KISHWAAAAA! Alijifanya kakomaa wakati bado kinda tu!sasa ajilengeshe tena kwa cdm ndo atajua kuwa kuna watu wanamjua tangu yupo chekechea!
 
Wanajamvi tunamfahamu kweli huyu kada? Maana kuna uwezekano kapata msukumo kutoka kwa RACHEL
 
Hata ka Porokwa yuko ile kambi ya 90 days hiyo haibadilishi mantiki kuwa six, nape na mwakyembe ni wanafiki wanaopigania matumbo yao kwa kigezo cha kutetea wanyonge kama walifikia stage ya kuiengineer uanzishwaji wa chama kingine ni wazi walioona CCM hakuwafai lkn still wako pale baada ya kuahidiwa vyeo this is big hypocrisy tushawajua wanafki wakubwa na wenye uchu wa madaraka

Mkuu wanaweza kuwa wanapigania matumbo yao kweli kabisa, lakini nao wamepigwa vita saana kisa ni Richmond!Lakini ikumbukwe pia ili ukitaka kupigania kile unachokiamini hauna sababu ya kukimbia unatakiwa kupambana mpaka kieleweke!
 
Kama hayo unayoeleza KISAIRO ni kweli, mbona hao kina Nape wanaikana CCJ. Soma nukuu hii ya MwanaHALISI.
[FONT="]
Kwa upande wake, Dk. Mwakyembe alisema, "Ninakushauri kwenda kwa msajili wa vyama, kule kuna orodha ya viongozi waasisi, wadhamini na wanachama waanzilishi. Kueni waangalifu, msiwalishe watu porojo za kina Mpendazoe." [/FONT]


[FONT="]Alisema, "…uandishi wa Kitanzania umekuwa wakipuuzi tu. Wewe si unajua kuna msajili wa vyama? Nendeni huko mtaona." [/FONT]
 
Hii ni vita ya Waarabu wa Pemba (Wanajuana).

Hapa hakuna msafi sio Sitta na kundi lake wala kina Lowassa pia. Hawa wote walikuwa kundi moja la mtandao lililomuweka JK madarakani ila baada ya kutofautiana kimaslahi hasa issue za madaraka.

Watanzania tusiwe wepesi kusahau, hakuna miongoni mwa hawa watu mwenye machungu na watanzania hata kidogo. Kila mmoja wao anajifikiria binafsi sababu kama si WANAMTANDAO leo Tanzania isingefika hapa tulipo kila kitu vururuvuru.
 
Great thinker use your thinking!!!

1. Kwa kipindi Sita, Mwakyembe na Nape walipoa asisi CCJ walikuwan sahihi kabisa na ilihitaji ujasikri mkuu ...Lazima waheshimiwe kwa hilo. Hali ya nchi ilikuwa Tete mapacha watatu walikuwa wanayumbisha nchi na CCM yao!!
2. Wakati CCJ ilipokuwa ina asisiwa ilikuwa ni jambo muhimu na huwezi kuwaita wahaini watu waliokuwa wanafanya hivyo wakati huo.Ilikuwa muhimu na CCM ilikuwa inawajua na wengi walipenda CCJ ikomae na ifanye kazi lakini Mapacha 3 waliimaliza CCJ kwa manufaa yao..
3. Sababu za kuasisi CCJ ndio hizi zilizoleta Gamba Leo. Na mleta gamba wa kweli lazima alione hilo na aone umuhimu wa waanzishi wa CCJ
4. Bila CCJ hapangekuwa na Gamba leo...JK ataniunga mkono na watumie hawa jamaa kama unaniunga mkono.
5. Kikwete atawatumia hao mnaowaona hawafai sasa ..SITA, NAPE na MWAKYEMBE ni MTAJI kwa KIKWETE kwa kuendesha Gamba kampeni kwani Gamba ndio CCJ. nani haoni hilo?
6. Mapacha watatu kwa kuwa ndio waliolengwa CCJ na ndio wanolengwa na Gamba ...watafanya kila upuuzi wanoujua kuwamaliza Mapacha watatu wa CCJ aka Nape, Mwakeyembe Na Sita.
7. Nape, Sita na Mwakyembe waheshimiwe ... kwa kuanzisha CCJ NA GAMBA!!!
8. Kikwete watumie ....Kikwete watumie ...kikwete watumie...!!
9. Kiwete wachana na viporojo vya mafisadi wa CCM wanaowatisha na kuwasumbua mapacha wa CCJ
10. Nani anaujasiri wa kuanzisha CCJ pale CCM ..wote waoga... wale waliokuwa na uajsiri wa kujitena sio wahaini ni wajasiri ...watumike Gamba!! Kikwete analijua hilo na watanzania wanalijua hilo!!


Ni kweli Azimio Jipya, tatizo wao wanaukimbia ushujaa huu, itakuwaje sisi tuuenzi na kuwapa credit hizo. Kama wangekubaliana na kuanzisha chama hiki, nami ningeungana nawe kwenye haya. Tatizo la unafiki ni manifaa binafsi na si kama lengo kuu la kukianzisha chama kwa manufaa ya UMMA. tafadhali tuwe makini rtunapotoa credits kama hizi.
 
Watanzania tunaoipenda nchi yetu hatutakiwi kumwamini mtu yeyote aliyeko CCM. Ikiwa Sitta na Mwakyembe wanachukizwa na udhalimu wa CCM unaoua maendeleo ya nchi yetu walipaswa kutokaCCM. Kama walitaka kuanzisha CCJ kwa ajili ya kujitoa CCM ni vyema lakini sasa bado wako CCM wakifurahia huo uovu wa CCM hawatufai.

Tatizo CCM wanapigana wenyewe na ukionekana kuwapinga hawa wanafiki wanaojifanya wanavua gamba unaonekana unawaunga mkono RACHEL. Sisi tunasema wote hawatufai. Hatuwataki RECHEL, hatuwataki pia Six, Mwakyembe, Maghufuli na wengine wote wanojifanya wema kwetu lakini wanataka CCM iendelee kuwepo madarakani hata kama wanaangamiza nchi lakini maslahi yao wanayapata kwa gharama ya umaskini wetu.

Wanasiasa wa aina hii ni wabaya kweli make wanadhoofisha nguvu ya walio na uchungu na nchi kuleta mabadiliko. Kinachotokea ni kuwa nguvu ya mabadiliko inagawanywa na hawa wanafiki mwisho wake walewale waovu wanaendela kutawala wao wakiwaunga mkono. Mfano mzuri ni bwana Kalonzo Msyoka ambaye ni makamu rais wa Kenya aliyegawanya nguvu ya ODM, kajiunga na Kibaki akaendelea kutawala kwa gharama ya kukwamisha mabadiliko ili mradi tu apate maslahi yake.

Hivo iwe kuwa Porokwa kaja kwa mkono wa RECHEL kwetu wazalendo tunafurahia manake wale wanafiki wanaopunguza nguvu ya mabadiliko kwa kujifanya wema kwetu wanadhihirishwa wazi na pia wanaharibu huko wanakopata maslahi yao ya kinafiki.

HIVI MCHAWI NA MWIZI WAKIKUTANA WAKAPIGANA MPAKA WAKACHOKA MPAKA WAKASHINDWA KWENDA KUROGA NA KUIBA NANI ATAFAIDI? SIYO YULE ANAYEENDA KUIBIWA NA ANAYEENDA KUROGWA? Asubuhi ikifika wakakutwa wamechoka kama watu hawakumjua mwizi watamjua; kama watu hawakumjua mchawi make hawa huwa wanafiki sana atakuwa amejulikana.
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Mzee kila kitu kina historia yake . Mwanzo na mwanzilishi daima huwa wana beba uzito sana .Sasa wewe ukitaka kukwepa ukweli huu nadhani utakuwa unakosea sana .Jambo lolote la wengi litawavuta watu baada ya kuona nani yuko kwenye usukani .Ni vyema kasema pia maana Nape amekuwa akisema hovyo na sasa amejulikana CCM wakae nay tu laini wajue si mtu wa maana anaganga njaa tu
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

ndugu yawezekana haushi duniani au basi leo ndo umekuja jf. Kila mtanzania anaelewa kwa nini mada hii imekuwa amplified na imesemwa si kwa sababu kuanzisha chama ni ajabu,la! Na je kwa nini hasemwi mwenykt wa ccj ila 6,mwakyembe na nape. Usipoteze mada ndugu.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Mkutano tayari umemalizika, Nape kwisha

Kwani Nape kuanzisha CCJ ni ufisadi? Nape wala asijihangaishi sioni kosa hapo tuna angalia je amewahi kuliibia Taifa! Mbona Dr Slaa alitoka CCM akenda Chadema kwani ni kosa mtu kupata wazo la kuanzisha Chama? Nape endelea na msimamo wako wa kuwaondoa EL,RA na Chenge
 
Back
Top Bottom