Porokwa apasua jipu la CCJ

Kwani Nape kuanzisha CCJ ni ufisadi? Nape wala asijihangaishi sioni kosa hapo tuna angalia je amewahi kuliibia Taifa! Mbona Dr Slaa alitoka CCM akenda Chadema kwani ni kosa mtu kupata wazo la kuanzisha Chama? Nape endelea na msimamo wako wa kuwaondoa EL,RA na Chenge

Nape kuanzisha CCJ na kukataa ni unafiki wa kindumilakuwili .... kwanini asiseme ndiyo aliyeanzisha...? watu wengine bana ni ubishi tuu kama mataruma ya reli
 
usiwe mvivu wa kuelewa

kinachozungumziwa hapa ni dhana ya unafiki na undumilakuwili kwa viongozi wetu ....period

Anfaal hawa hawawezi kuwa wanafiki kwa CCM wakawa ni wazuri kwa Watanzania. Zaidi ya hapo ni wanasiasa masilahi hawa na tunajua nchi inatafunwa na wanasiasa masilahi akiwepo JK. Kama hulioni hilo ebu bainisha masilahi yako kwenye kuwatetea usisingizie utaifa
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Hii siyo habari tena, haina tija tena kulijadili labda kama CCM ndio wanataka kuleta hoja mpya ilikusahaulisha watu vitu muhimu tunavyovidai hasa swala la Mafisadi na ahadi ya kuvua magamba
 
usitumie nguvu kutoa hoja yako. Kama majina yao hayapo kwa msajili, mwakyembe , 6 na nape wakikanusha, kimsingi mimi nitawaamini unless kama unaweza definition nyingine ya '
uanzilishi' mbali na ninayoijua mimi

Mbona Rosti Tam hayuko kwenye kampuni ye yote lakini anachukua hundi za malipo kwa mkono wake? Hapo unakazia hukumu ya watanzania juu ya ufisadi ndani ya chama la magamba na serikali yake ulivyokubuhu
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?
Inasaidia kuwajua wanasiasa wanafiki wanaokana vivuli vyao
 
Anfaal hawa hawawezi kuwa wanafiki kwa CCM wakawa ni wazuri kwa Watanzania. Zaidi ya hapo ni wanasiasa masilahi hawa na tunajua nchi inatafunwa na wanasiasa masilahi akiwepo JK. Kama hulioni hilo ebu bainisha masilahi yako kwenye kuwatetea usisingizie utaifa

Tuna angalia Uadilifu kwa maslahi ya Taifa! Habari ya vyama ni utashi wa mtu! Ila kama kuna ufisadi wamefanya Sitta,Mwakyembe na Nape hapo tupambane nao lakini kwa hili la kuanzisha chama kingine liko ki-CCM zaidi nashangaa hata watu wa Chadema kulichukulia kama agenda! Leo Mpendazoe katoka CCM yuko CDM kapitia CCJ sasa unaweza sema tusimwamini Mpendazoe kisa kahama au kabadilisha chama? Ina muondolea uaminifu mwana siasa kuhama au kubadili chama? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "CCM sio baba wala Mama yangu kama kuna Chama kitaonekana kina mlengo mzuri naweza kuwapa kadi yenu CCM" hivyo tunapoteza muda kujadili hoja mfu!
 
Hii siyo habari tena, haina tija tena kulijadili labda kama CCM ndio wanataka kuleta hoja mpya ilikusahaulisha watu vitu muhimu tunavyovidai hasa swala la Mafisadi na ahadi ya kuvua magamba

Tunawapa umaarufu kuwajadili Sitta,Mwakyembe na Nape kisa CCJ! Halafu CCJ yenyewe haipo! Tumeingizwa mkenge kujadili hoja za CCM!
 
Mbona Rosti Tam hayuko kwenye kampuni ye yote lakini anachukua hundi za malipo kwa mkono wake? Hapo unakazia hukumu ya watanzania juu ya ufisadi ndani ya chama la magamba na serikali yake ulivyokubuhu

Nimeipenda hii. Ni jibu kwa wote wanaokazania kusema kuwa mbona majina yao hayapo kwa msajili. Kama walishiriki na wenzao wakasema walishiriki inakuaje tena wanakana? Kama siyo kosa, au siyo ufisadi kujiunga na chama chchote, kwa nini wanan'gaka?
UNAFIKI TU!!!!!!!
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?
waanzilishi wa ccm, cuf, chadema nccr nk tunawajua na wao huona fahari kwa kuwa waasisi, sasambon awaanzilishi wa ccj wanakana? hapo ndo tatizo
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Waanzilishi wa CCM, CUF, CHADEMA, NCCR n.k, tunawajua na wao huona fahari kwa kuwa waasisi, sasa mbona awaanzilishi wa CCJ wanakana uhusika? Hapo ndo tatizo.
 
Tuna angalia Uadilifu kwa maslahi ya Taifa! Habari ya vyama ni utashi wa mtu! Ila kama kuna ufisadi wamefanya Sitta,Mwakyembe na Nape hapo tupambane nao lakini kwa hili la kuanzisha chama kingine liko ki-CCM zaidi nashangaa hata watu wa Chadema kulichukulia kama agenda! Leo Mpendazoe katoka CCM yuko CDM kapitia CCJ sasa unaweza sema tusimwamini Mpendazoe kisa kahama au kabadilisha chama? Ina muondolea uaminifu mwana siasa kuhama au kubadili chama? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "CCM sio baba wala Mama yangu kama kuna Chama kitaonekana kina mlengo mzuri naweza kuwapa kadi yenu CCM" hivyo tunapoteza muda kujadili hoja mfu!

Wewe mgumu wa kuelewa kinachobishaniwa hapa! Na usiconclude kwamba wote wanaoishabikia mada hii ni wana CDM! Wako wana-CCM ambao wanachukizwa na hayo ya akina Nape.

Tunasema wawe majasiri, wasiwe waoga, kwani ni haki yao kikatiba kujiunga na chama chchote, bila kijificha jificha, wasikane! Mbona Mpendazoe alitoka CCM na kuiingia CCJ na kutangaza hivyo, halafu akaingia CDM na kutangaza hivyo.

Hawa kina nape ni popo tu, walikuwa wanapenda kufaidi the best of both worlds.
 
Re: Tuzungumze ufisadi na matumizi ya rasilimali za umma au sarakasi za watuhumiwa??
Aaah baada ya kupata kama simu ya nane toka kwa waandishi wa habari juu ya sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi(hasa hoja ya CCJ) nikajiuliza, tuzungumzie ufisadi ambao kimsingi ni namna rasilimali za nchi yetu zinavyotumika katika kushughulikia matatizo ya wananchi au nasi tucheze sarakasi hizi?

Nape ameanzisha thread na kuendeleza unafiki wake ...haya siyo maadili ya uongozi
 
Wewe UNAYEJIITA Mlengo wa kati, shari ufahamu kuwa kuna tofauti kubwa ya tuhuma za ufisadi na uhaini wa kuasi chama.

Kwa chama cha siasa, kosa la uhaini wa kuasi chama ni kosa kubwa sana kuliko ufisadi. Ufisadi umefanyika ndani ya serikali na ndiyo maana kina Nape wanazungumzia kuwaondoa katika chama wanaowatuhumu. Hawazungumzii kuwafikisha mahakamani.

Sasa kama wanataka kuwaondoa katika chama wanaowatuhumu, basi lazima wawaondoe kwanza wasaliti wa kwenye chama…
 
Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe.
 
Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe – Daniel ole Porokwa.
 
Katika hoja zote zilizotolewa hapa hakuna ya kipumbavu kama ile inayosema eti kwa kuwa majina yao hayako kwa msajili, basi hawawezi kuwa waanzilishi.

Sijaona nonsense kama hii. Mikutano inayoitishwa kuanzisha chama huhusisha mamia ya watu lakini si wote hatimaye wanaingia katika daftari la msajili. Wanaoingia huko ni viongozi (bila shaka wa muda) na wadhamini (nao bila shaka wa muda).
 
Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe – Daniel ole Porokwa.
 
ni vizuri mkiendelea kuomba mungu aibariki tanzania labda kuna siku mtaomba kwa imani ya kweli na mungu akawasikia.
Tumekuwa na tabia ya muda mrefu ya kupenda kusikia yale tunayoyataka, na si vinginevyo.
Kuna kipindi anaweza akaingia mtu hapa na hoja fulani, utaona namna watu wanavyom-crash na kusema toa ushahidi. Katika hili sioni mtu akidai ushahidi, watu wanajikita moja kwa moja katika kujadili na kutoa laana na kashfa na lawama, hawataki ushahidi kwani wanajua ukitolewa ushaihidi huo utaonyesha taswira na ukweli halisi tofauti na kile wanachotaka na kupenda kukisikia.
Watu wa mahari hapa wanafikiri vizuri sana, lakini ushabiki na mapenzi huondoa mara moja nguvu na uwezo wao huo.
Kweli mungu ibariki tanzania.
 
Back
Top Bottom