Pork! Kitimoto! Pork! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pork! Kitimoto! Pork!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mentor, Jul 27, 2011.

 1. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,281
  Trophy Points: 280
  Wadau,
  mwisho wa mwezi huu nina mpango wa kusafiri sehemu ambapo hakuna hiyo kitu.
  Ninahitaji sehemu hapa dar...affordable... ambapo nitaenda nile kitimoto weeee..mpaka hamu iniishe.
  Tafadhali ushauri...
  Natanguliza shukrani.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Nenda pande za Kilimanjaro Pub-Ubungo Riverside au Kimara SUCA,bila kusahau B Bar Sinza kwa Remmy.
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dah! Tulikua na mpango wa kukukaribisha over the weekend na shemejio.... naona nimeahirisha sasa...
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mentor,

  Ukija Arusha nenda Apache wanatengeza mdudu wa ukweli nakwambia unaweza kuhamia Arusha jamaa wako juu sana.Mwenzako kila jumapili mida ya mchana utanikuta natwanga mdudu na Gordons za kufa mtu.Apache iko mitaa ya Ricks Club unaingia ndani kidogo unapinda mkono wa kushoto unakwenda umbali wa mita 100 unakata kulia mjomba nina hakika hujawahi tafuna mbuzi katoliki wa ukweli.

  Duh nasikitika machalii wa Arusha wanaweza kuvamia anga zangu mdudu akapandishwa bei.Unajua tena law of supply and demand inaweza kuapply.


   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kapige ya kuchoma pale Mburahati

  Au nenda pale kona-baruti kwa Kinibu
   
 6. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  IMG0010A.jpg

  Hii kitu utaipata Iringa Kwa Mama Spencer.

  Karibu na Ofisi za Siasa ni kilimo. Karibu sana Mkuu.

  The best in Iringa. Kule kwenye mabanda ya CCM ni wachafu Sana.

  For more info. ni PM.
   
 7. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,281
  Trophy Points: 280
  Duh..ok ok..
  hizo sides ni mbali sana na mimi nataka kwenda Ijumaa nkitoka kazini..
  Makazi yangu ni Mbagala zaidi..
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,281
  Trophy Points: 280
  aah dada...ukifanya ivo ninaweza kufikiria kubadili mipango..si unajua u will take the higher priority!!!
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  ha ha ha.... haya bana.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mbagala kitu gani bana?
  Kama vipi ibuka kwa AshaDii au nenda mburahati kwa mashingia pale.
  Kama kati nakushauri B Bar sinza.
   
 11. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Duh.

  Kwa mam Spencer Ndio wapi, coz hiyo picha imenipa Njaa Ghafla.
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakuu, mimi natafuta kitimoto pori. Anayejua inakopatikana anijulishe tafadhali. Napenda sana ile kitu
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  niongeleshe vizuri........
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Unataka kuuza nyara ya taifa?Asee yule mdudu hana mafuta, nyama tamu kama balaa.Mkuu njoo ruvu hapa, kusafirisha kuja dar noma, jamaa wakikukamata wanaichukua na inabidi kuhonga.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mkuu iringa hiyo kwa mama siyovelwa.Tuache utani kitu cha kuchoma enzi hizo pale onyonya ukunonze pale Kiboriloni!Walahi hakuna kama hiyo.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wasiliana na Mzee wa Maono, Muhadhiri, Malaria Sugu, Bi Zakia hao lazima watakusadia alipo huyo Mnyama wa taifa
   
 17. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hivi hata yule ni nyara?.....mbona mtamu vile.......basi MzeePunch itabidi uje Yaeda.....hakuna ujanja
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hapa tunahitaji muongozo wa Freetown.....ndio alihudhuria hilo eneo bold hapo juu siku za karibuni......atueleze kama ubora ni ule ule au lah
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Bigirita,

  Onyonya ukununze cha mtoto mambo yote Apache mdudu anachanganywa na mboga mboga,ndizi na kachumbari ya kufa mtu.Walahi nakwambia ukimaliza mlo na double mbili za gordons lazima ucheue na kijasho chembamba lazima kikutoke bila kujali hali ya hewa ni baridi au joto.


   
 20. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,281
  Trophy Points: 280
  Usinifanye nitoe machozi Bigi....Onyonya was the place! too bad sipo moshi tena...
   
Loading...