Porini Kwetu- Jamaa ametoka outing Kidogo

Porini Kwetu- Jamaa ametoka outing Kidogo

Mtanga Tc

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
235
Reaction score
84
Ninaamini ni watu wachache wamewahi kufanikiwa kumuona huyu akiwa nje ya maji mchana. Hapa ni katika mbuga zetu akiwa ametoka kidogo kupunga. Anajulikana kama Kiboko (Hippopotamus amphibius) au Wagiriki walimwita Water Horse.
Kwa kawaida Hippo anatumia masaa zaidi ya 16 akiwa amejituliza kwenye maji ili kupooza miili yao ambayo inaonekana kuwa mikubwa!
​
 

Attachments

  • IMG_7978.JPG
    IMG_7978.JPG
    826.6 KB · Views: 395
Kwa ukaribu zaidi......
Kiboko pia anaweza kujituliza pembezoni mwa mto au ziwa na anapokuwa nje, mwili wake hutoa aina ya mafuta ambayo yana rangi nyekundu,(kwa ajili ya kulainisha ngozi yake). Hii ndiyo sababu iliyopelekea watu kuwa na dhana isiyo sahihi kuwa mnyama huyu jasho lake ni damu (sweat blood)
 

Attachments

  • IMG_7979.JPG
    IMG_7979.JPG
    1.1 MB · Views: 116
Nishakutana nae maeneo ya Serengeti kweney hippo pool yaani ni faraja sana kumuona akiwa nje ya maji
 
Hawa wanyama wako wengi sana mto mara,kuna jamaa walikwenda kuwawinda,alivyofyatua risasi mnyama alimfuata kasi jamaa akadandia tawi la mti.Lakini ilikuwa too late maana "mdudu" alimkata tumboni akamgawanya vipande viwili ikawa mwisho wa kuwinda, wakarudi nyumbani na maiti ya mtu badala ya nyama ya Hippo
 
Hapo raha yake ujichanganye ukifikiri kitimoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom