Rajabu Msechu
Member
- Apr 13, 2016
- 35
- 18
Ahlan wa Sahlan wanafamilia ya jukwaa la siasa, pasipo kupoteza muda ningependa kumpa pongezi za dhati mkuu wa mkoa wetu Mh. Paul Makonda kwa jitihada zake anazozifanya kila uchwao ikiwa ni katika kuhakikisha mkoa wa Dar es salaam unakuwa na sifa nzuri na kuigwa.
Nikianza kabisa na suala zima la walimu kutolipa nauli kwenye mabasi, hili wazo alilolitoa kipindi akiwa RC ni wazo zuri na linafaa kabisa kuungwa mkono licha mpaka sasa utekelezaji wake haujaanza kushika hatamu, lakini nina amini kabisa itafika pahala jambo hili litafanikiwa.
Kingine ni suala zima la kuonyesha nia ya kuwaondoa wadadapoa na ombaomba mjini ambao wamekuwa ni kero kubwa hasa kwa wananchi, sipo hapa kuwabeza, lah! Bali nina amini hakuna nchi yeyote Dunia ambayo imehalalisha ombaomba au madada poa.
Kwa kumalizia ni motisha aliyotoa kwa Polisi ya kuwazawadia kiasi cha shilingi Milioni endapo watafanikiwa kuwakabili wahalifu wanaotumia silaha za moto yani nikimaanisha Majambazi, ingawa wazo lake hili limepingwa na watu wengi mmojawapo nikiwa mimi, bali naamini kwa maoni ya wananchi atalifanyia kazi suala hili.