Pongezi kwa Chuo Kikuu SUA

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Kwanza nitoe pole kwa wote walioguswa na vifo vya vijana wetu.

Zaidi nitoe pongezi kwa Uongozi, wakufunzi, wanachuo na jumuiya yote ya Chuo kikuu cha kilimo Sokoine Morogoro.

Kusafirisha maiti wawili kutoka Morogoro hadi Arusha kugharamia sanda, jeneza kutuma wawakilishi, bado mkatoa na fedha za rambirambi juu, hakika huu ni wema mkuu.

Vijana wetu tumewapumzisha wote leo hapa Karatu.

Mungu awabariki mno
 
Jinsi mandhari ya chuo hiki ilivyo nzuri na ya kupendeza ndivyo jinsi mioyo ya watumishi na wanachuo wa chuo hiki ilivyo mizuri,, mbarikiwe sana.

IMG_20230716_102107.jpg
 
Ndio chuo pekee nchini wahitimu wanatija na kuitendea haki taaluma zao.

Poleni na msiba mkuu. Nini Chanzo cha kifo cha hao waliotangulia?
Vijana wao wawili walipata ajali wakiwa na pikipiki (waligongwa na gari) wakafa wote.

Wote ni wenyeji wa hapa Karatu (mmoja mwanafunzi wangu o level).

Kwa kweli nmesikitika kuaga picha tu maana miili haijaruhusu kuangaliwa ila participation ya chuo kwenye hii misiba imenifanya nifungue uzi wa kuwapongeza.
 
Hawa vijana walikuwa wapumbavu sana, mambo ya kuiga iga na bangi za vijana wa Arusha zimewaharibu na mwishowe ni msiba na vilio kwa wazazi wao

Unataka kutoka na pikipiki SUA- Morogoro mpaka karatu - Arusha tena mbovu kwa mwendo ambao hauheshimu barabara?

Kuna Vifo vingine vya kujitakia, Hawa vijana wamekiita kifo na wamekipata. Mimi ni mtu wa mwanzo kufika eneo la tukio kwa mwendo lazma tu lolote lingewatokea

Japo sitakiwi kuhukumu ila Hawa wamejitakia
 
Hawa vijana walikuwa wapumbavu sana, mambo ya kuiga iga na bangi za vijana wa Arusha zimewaharibu na mwishowe ni msiba na vilio kwa wazazi wa...
Kwa tabia za ovyo sikubaliani nawe mkuu, ebu fikiria huyo mmoja ana miaka 24 na kwenye kozi yake ashapiga miaka 4 ndo alikuwa anaelekea wa 5 na kozi enyewe ni BVM, taaluma ngumu kuliko udaktari wa binadamu, waulize wanaojua watakwambia km kuna mda wa kufanya starehe kwenye, na kwao ni maskini kweli

Huyo wa pili nimemfundsha O level na huwa anakuja kutusalimu akirudi likizo, dogo ni fighter tangu yuko shule, analima anafuga na anapiga boda, hadi alikuwa anafanya biasharavya kukopesha watu pesa kwa riba, inshort alikuwa mchumi kweli, inasemekana ameacha magunia mengi ya mazao ndani fedha nyingi benki.

Basi tu siku ikifika utaanguka hata kitandani na utaondoka.
 
Kuna Vifo vingine vya kujitakia, Hawa vijana wamekiita kifo na wamekipata. Mimi ni mtu wa mwanzo kufika eneo la tukio kwa mwendo lazma tu lolote lingewatokea
Wengine wamekufa kwa ajali za ndege, wengine ajali za meli, wengine ajali za treni, wengine ajali za trekta wengine ajali za baiskeli, wengine wamekufa kwa kutembea kwa miguu.

Je upumbavu wa hawa marehemu wa SUA uko wapi? Kuna watu wana ride pikipiki toka Johansberg mpaka Cairo iweje hawa wa SUA Karatu waitwe wajinga?
 
Wengine wamekufa kwa ajali za ndege, wengine ajali za meli, wengine ajali za treni, wengine ajali za trekta wengine ajali za baiskeli, wengine wamekufa kwa kutembea kwa miguu.

Je upumbavu wa hawa marehemu wa SUA uko wapi? Kuna watu wana ride pikipiki toka Johansberg mpaka Cairo iweje hawa wa SUA Karatu waitwe wajinga?
Umesoma umeelewa, pikipiki mbovu halafu mwendo wa kichaa, ungewaona wanavyokimbia hapo barabarani ungewaonea huruma kabla ya ajali
 
Back
Top Bottom