Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,497
- 113,592
Wanabodi,
Bandiko hili ni kufuatia hoja ya mwana jf huyu.
Mkuu Yohane Mbatizaji, kwanza asante kwa bandiko hili.
Mimi ni miongoni mwa tuliyemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM katika ofisi Kuu ya CCM Makao Makuu Dodoma leo asubuhi na kuona jinsi alivyoondoka na gari moja la number za kiraia, bila ving'ora wala msafara.
Kwavile sisi binadamu tunatofautiana observation powers, naomba na mimi nichangie nilichokiona kwenye uchukuaji wa fomu huo na kueleza kina maana gani kwa mustakabali mzuri na mwema wa siasa za nchi yetu kuelekea October 2020.
Paskali
Bandiko hili ni kufuatia hoja ya mwana jf huyu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amechukua fomu ya kuwania kinyang'anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Makao Makuu ya CCM, Dodoma.
View attachment 1481048
Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Yohane Mbatizaji, kwanza asante kwa bandiko hili.
Mimi ni miongoni mwa tuliyemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM katika ofisi Kuu ya CCM Makao Makuu Dodoma leo asubuhi na kuona jinsi alivyoondoka na gari moja la number za kiraia, bila ving'ora wala msafara.
Kwavile sisi binadamu tunatofautiana observation powers, naomba na mimi nichangie nilichokiona kwenye uchukuaji wa fomu huo na kueleza kina maana gani kwa mustakabali mzuri na mwema wa siasa za nchi yetu kuelekea October 2020.
- Kwanza ni kule tuu kuonyeshwa live kupitia TBC tukio la rais Magufuli kuchukua fomu, ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima. Kuna msemo wa Kiswahili usemao, " nyota njema huonekana asubuhi" huku kuonyeshea live toka mwanzo is good for transparency.
- Uchaguzi huru na wa haki ni process inayohitaji maximum transparency, kwasababu rigging zote za uchaguzi huwezi kufanyika kutokana na lack of transparency, hivyo hii Transparency ni moja ya mambo muhimu sana yanayoufanya uchaguzi uwe huru na wa haki na matokeo kuwa credible na Kukubalika na wote. Mfano kura zote zinahesabiwa kituoni na matokeo ya kila kituo kubandikwa ubaoni transparently, if there is nothing to hide, kwanini vyama vizuiliwe kufanya independent tallying?!.
- Kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, TBC imetimiza wajibu wake wa uhabarishaji umma kikamilifu kwa kututangazia live tukio hili ili umma wa Watanzania tushuhudie kwa kuona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu na sio kuambiwa au kuhadithiwa, kuona ni kuamini.
- Natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma. Pia vyama vya upinzani jifunzeni kufanya siasa za kistaarabu kwa kushawishi kwa hoja kwa lugha za staha na sio kwa viroja, lugha za maudhi na kutukana
- Wito kwa TBC, kwanza hongereni kwa kazi nzuri, mlichokifanya leo ni mwanzo mzuri wa mchakato huu wa urais. Nawaomba mvitendee haki sawa vyama vyote vya siasa, msifanye upendeleo kwa chama kimoja na kuvibagua vingine, hivyo tunategemea kuona live za wagombea urais wa vyama vingine nao wakiwa coved na TBC
- Pia nimemnote rais Magufuli akitumia usafiri wa gari lenye number binafsi. This is very good thing kwasababu rais Magufuli ametenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali. Rais Magufuli hakutumia gari za serikali, wala hakutembea na msafara na ving'ora, ikiwemo battalion, rais Magufuli ametumia gari moja tuu yenye number za kiraia. Hatutarajii kuendelea kuona vikao vya chama vikifanyikia Ikulu yetu!. Hongera sana rais Magufuli, kwa hili utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa sana kwasababu Mungu ni mtenda haki na anapenda kuona sio tuu haki itendeke bali haki itendeke na kuonekana imetendeka. Huwabariki sana watenda haki na huwalaani watenda maovu na kuwaadhibu wasio tenda haki!.
- Hatua hii ni hatua yenye essence kubwa sana kwenye mustakabali wa usawa wa kidemokrasia na usawa wa uwanja wa mapambano kujenga uwanja sawa, the level playing field, hivyo ni hatua muhimu kuifuta ile dhana ya kugombea urais Tanzania kufananishwa na kugombea kisu cha makali kuwili huku mgombea mmoja ameshika mpini na kuwashikisha wapinzani wake upande wa makali kuwili
- Wito kwa Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, kwenye wagombea urais, nawaombeni mfuate mfumo wa nchi za Nordic na Scandinavian countries ambapo wagombea wote wa urais wanakuwa treated equally and the same. Kama kuna mgombea ana privileges za incumbent president, ikiwemo ving'ora, media, hizo privileges zote zinakuwa scraped down isipokuwa ulinzi, then wagombea wote wanapewa ulinzi. Kama kuna mgombea ana msafara wakiwemo state media, then wagombea wote wanapewa misafara, ulinzi, media na logistical support ili wote wafananie, na sio mgombea mmoja ndio anatumia state logistics kwa state cars kufungwa private number, kwasababu ni rais na wengine wote wapambane na hali zao.
- Kuwatendea haki sawa wagombea wote wa urais wa vyama vyote kutapelekea taifa letu kubarikiwa na kupata neema, baraka na ustawi.
- Kukipendelea chama kimoja au mgombea mmoja na kutowandea haki sawa wagombea wote wa vyama vyote kutapelekea Taifa kuchapwa na bakora za karma ya upendeleo na kutotenda haki kwa wote. Na viongozi wahusika kupata bakora za karma, individuals.
Paskali