Nchimbi ameanza kwa kuwadanganya uongo mkubwa CCM!

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,348
Katibu mkuu wa CCM katika hotuba yake ya kwanza pamoja na mengi aliyosema amesema huko Marekani vyama vya Republicans na Democrats huwa vinawapitisha Marais bila kuwashindanisha katika kura za ushindani za vyama kugombea muhula wa pili wa kipindi cha urais.

Ameenda mbali zaidi sana akisema huo ni ujinga ambao vyama Wamarekani waliachana nao tangu miaka ya 1980.

Nchimbi amedanganya, ukweli ni kwamba Marais wote wa Marekani walipogombea kipindi cha pili urais walishindanishwa katika vyama vyao

1. Mwaka 1984 Rais wa Marekani wa kipindi hicho katika chama chake alishindanishwa na Harold Stassen pamoja na Ben Fernandez.

2. Goerge H.W Bush mwaka 1992 akigombea mara ya pili urais alishindanishwa na chama chake na wagombea watano mpinzani mkali na maarufu zaidi akiwa Pat Buchanan.

3. Mwaka 1996 Bill Clinton alishindanishwa na LaRouche na wagombea wengi wengi wasio maarufu katika kipindi cha pili kugombea urais.

4. Mwaka 2004 Bush alishindanishwa na wagombea wengi wadogo wasio maarufu kama John Buchanan, Jack Fellure n.k

5. Mwaka 2012 Obama akigombea mara ya pili alishindanishwa katika chama chake na wagombea kama John Wolfe, Jr na Darcy Richardson

6. Mwaka 2020 Trump akigombea mara ya pili alishindana katika chama chake na Bill Weld

Kingine ambacho Nchimbi hakusema ni kwamba kimsingi uchaguzi wa nafasi ya mgombea urais katika vyama vya Marekani inafanyika katika majimbo na sio sehemu moja kama hapa kwetu Dodoma au Dar.

Huko Lazima mgombea ashinde kwa wingi(zaidi ya nusu) ya wa wajumbe katika majimbo na kura lazima zipigwe kabla ya kuidhinishwa na kamati za vyama kitaifa.

Jambo lingine ni kwamba Nchimbi alikuwa akishangiliwa karibu na watu wote wakati anatoa historia ya uongo kuhusu uchaguzi wa Marekani.
 
Waswahili wanasema kibaya chajitembeza

Ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kukubalika ujue hamna kitu hapo
 
Sasa katika mamia ya wagombea urais waliowahi kupita Marekani tangu uhuru mtu mmoja tu kusema amaeibiwa kura huoni huo mfumo unafanya kazi vizuri na uko thabiti sana.
Nani aaminiwe na Wananchi wa Tanzania?

Mawakala wa Makaburu au Viongozi wa CCM?
 
6. Mwaka 2020 Trump akigombea mara ya pili alishindana katika chama chake na Bill Weld
Huyo nchimbi ni mbumbumbu (in this context):
"President Donald Trump informally launched his bid for reelection on February 18, 2017. He launched his reelection campaign earlier in his presidency than any of his predecessors did. He was followed by former governor of Massachusetts Bill Weld, who announced his campaign on April 15, 2019, and former Illinois congressman Joe Walsh, who declared his candidacy on August 25, 2019. Former governor of South Carolina and U.S. representative Mark Sanford launched a primary challenge on September 8, 2019. In addition, businessman Rocky De La Fuente entered the race on May 16, 2019, but was not widely recognized as a major candidate"
 
Back
Top Bottom