Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!

Paskali sioni haja ya kunadi kazi za NEC,mwenye shughuli hizo yupo ni NEC mwenyewe.
Ila ukiona NEC hafanyi kazi yake ipasavyo ndiyo mapungufu ya msingi unayoyatamani yaondolewe mara mmoja, tuwe kama nchi za Scandinavia .Tuwe na utaratibu usiotia shaka kwa wagombea wa vyama vyote.
Kumbe wana demokrasia wanapodai Tume Huru wako sahihi kabisa.ndio transparency unayokusudia tuwe nayo hapa kwetu Tanzania.
 
Nikielewa kwamba ulinzi ulikuwa intact kwa namna wanazojua wao nitakuwa Sina shida, lakini Kama ndo ilikuwa lile gari moja tu hapo nasema hapana. Rais bado anahitaji walau minimum escort. Tatizo letu ninaloliona ni kukosekana kwa upeo mkubwa ktk kuyaona Mambo ya msingi. Mfano, ikitokea mgombea mwingine kaenda kuchukua fomu na msafara hata wa magari matatu, Kuna hatari atazuiwa na polisi ili abaki na gari moja Kama alivyofanya Rais. Naogopa alichofanya Rais leo kugeuka kuwa standard kwa wagombea wengine wote. Hata hivyo, huyo bado Ni Rais na mkuu wa nchi yetu( hakuna asiyejua) apewe hadhi ya kulindwa na hata msafara madamu tu wengine nao waruhusiwe kwa kadri kuwa na watu wataowahitaji ktk misafara yao. Otherwise, Kuna Jambo zuri amelionyesha mheshiwa Rais" unyenyekevu na kukubali kwamba ni mgombea Kama wengine"
 
Unapumbazwa na maigizo ya ccm?
Ya akina kinana kulima mpunga na kamera?
Au ya kufyatua matofali?
Hivi hujaona boda boda zinamwandama?
Unafikiri hao walikuwa bodaboda wa kawaida?
Kwa taarifa yako alikuwa na ulinzi hadi ndani ya daladala walijaa walinzi na magari binafsi
 
Wanabodi,

Bandiko hili ni kufuatia hoja ya mwana jf huyu.
Mkuu Yohane Mbatizaji, kwanza asante kwa bandiko hili.
Mimi ni miongoni mwa tuliyemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM katika ofisi Kuu ya CCM Makao Makuu Dodoma leo asubuhi.

Kwavile sisi binadamu tunatofautiana observation powers, naomba na mimi nichangie nilichokiona kwenye uchukuaji wa fomu huo na kueleza kina maana gani kwa mustakabali mzuri wa siasa za nchi yetu.

  1. Kwanza ni kule tuu kuonyeshwa live kupitia TBC tukio la rais Magufuli kuchukua fomu, ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima. Kuna msemo wa Kiswahili usemao, " nyota njema huonekana asubuhi" huku kuonyeshea live toka mwanzo is good for transparency.
  2. Uchaguzi huru na wa haki ni process inayohitaji maximum transparency, kwasababu rigging zote za uchaguzi huwezi kufanyika kutokana na lack of transparency, hivyo hii Transparency ni moja ya mambo muhimu sana yanayoufanya uchaguzi uwe huru na wa haki na matokeo kuwa credible na Kukubalika na wote. Mfano kura zote zinahesabiwa kituoni na matokeo ya kila kituo kubandikwa ubaoni transparently, if there is nothing to hide, kwanini vyama vizuiliwe kufanya independent tallying?!.
  3. Kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, TBC imetimiza wajibu wake wa uhabarishaji umma kikamilifu kwa kututangazia live tukio hili ili umma wa Watanzania tushuhudie kwa kuona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu na sio kuambiwa au kuhadithiwa, kuona ni kuamini.
  4. Natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma.
  5. Wito kwa TBC, kwanza hongereni kwa kazi nzuri, mlichokifanya leo ni mwanzo mzuri wa mchakato huu wa urais. Nawaomba mvitendee vyama vyote haki sawa, msifanye upendeleo kwa chama kimoja na kuvibagua vingine, hivyo tunategemea kuona live za wagombea urais wa vyama vingine nao wakiwa coved na TBC
  6. Pia nimemnote rais Magufuli akitumia usafiri wa gari lenye number binafsi. This is very good thing kwasababu rais Magufuli ametenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali. Rais Magufuli hakutumia gari za serikali, wala hakutembea na msafara na ving'ora, ikiwemo battalion, rais Magufuli ametumia gari moja tuu yenye number za kiraia. Hatutarajii kuendelea kuona vikao vya chama vikifanyikia Ikulu yetu!. Hongera sana rais Magufuli, kwa hili utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa sana kwasababu Mungu ni mtenda haki na anapenda haki, huwabariki watenda haki na kuwaadhibu wasio tenda haki!.
  7. Hatua hii ni hatua yenye essence kubwa sana kwenye mustakabali wa usawa wa kidemokrasia na usawa wa uwanja wa mapambano kujenga uwanja sawa, the level playing field, hivyo ni hatua muhimu kuifuta ile dhana ya kugombea urais Tanzania kufananishwa na kugombea kisu cha makali kuwili huku mgombea mmoja ameshika mpini na kuwashikisha wapinzani wake upande wa makali kuwili
  8. Wito kwa Tume yetu ya Uchaguzi, NEC, nawaombeni mfuate mfumo wa usawa wa wagombea urais wa Nordic countries na Scandinavian countries ambapo wagombea wote wa urais wanakuwa treated the same. Kama kuna mgombea ana ulinzi kwasababu yeye ni rais, then wagombea wote wanapewa ulinzi. Kama kuna mgombea ana msafara wakiwemo media, wagombea wote wanapewa misafara, media na logistical support ili wote pafananie, na sio mgombea mmoja ndio anatumia state logistics kwasababu ni rais na wengine wote wapambane na hali zao.
  9. Kuwatendea haki sawa wagombea wote wa urais wa vyama vyote kutapelekea taifa letu kubarikiwa na kupata neema, baraka na ustawi.
  10. Kukipendelea chama kimoja au mgombea mmoja na kutowandea haki sawa wagombea wote wa vyama vyote kutapelekea Taifa kuchapwa na bakora za karma ya upendeleo na kutotenda haki kwa wote.
Nawatakia Jumatano Njema.

P
Bandiko zuri sana
 
Mkuu P, nimekuelewa msingi wa hoja yako ' usawa' sina hakika ccm watafungua milango ya fahami
 
Hivi Jana Magufuli alikuwa anahutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania au alikuwa anahutubia mkutano mkuu wa ccm? Na je yeye alisimama kama rais,mwenyekiti wa ccm au alisimama na kofia zake zote mbili?
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaongozwa na CCM Chini ya uongozi wa chairman wao..ni Ngumu Sana kutenganisha kofia hizo mbili kwasababu KAZI ya urais haina break time mpaka Term iishe.
 
Ila all in all tulishauri humu tukabezwa shughuli za chama kufanyika Ikulu ila naona walio tubeza ndio wengine watamsifia.
Ikulu ina sehemu mbili,
1. Ni Ofisi ya rais- rais yuko huru kukutana na yeyote na kufanya mkutano wowote na kundi lolote hata mikutano ya CCM au vikao vya Chama, bila kuvunja sheria yoyote, ila kitendo cha kufanyia vikao vya CCM Ikulu, kwa macho ya wapenda haki bin haki, huko ni kutake advantage ya Ikulu yetu kwa manufaa ya CCM, hivyo kama rais ni Mwenyekiti wa CCM na serikali ni serikali ya CCM, na rais yuko Ikulu, hakuna ubaya wowote kwa rais kutake advantage ya Ikulu yetu kwa chama chake kwasababu hajavunja sheria, kanuni wala taratibu yoyote, na kwa kufanya hivyo hata adhibiwa chochote, kwasababu it's doing nothing wrong kisheria, kikanuni na kiutaratibu but morally wrong, hivyo kutokufanyia, vikao vya CCM Ikulu, kunaleta baraka na ustawi zaidi.
2. Ikulu ni makazi ya rais- rais yuko huru kumkaribisha mtu yoyote au kikundi chochote kwa lengo lolote ikiwemo vikao vya Chama, ila kuna eneo la ofisi na eneo la makazi, vikao hivi vikifanyikia eneo la makazi ni haki kabisa, lakini vikifanyikia eneo la ofisi, ni matumizi mabaya ya ofisi kwa advantage ya chama chake, this is not right.

Kwa hili rais Magufuli hakulianza leo
Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!
P
 
Duuh.........
Alikuwa na gari moja wakati njia nzima walijaa askari wa usalam barabarani na magari ya raia yakawekwa foleni.
Mkuu, Kipangaslecial, kwanza asante kuchangia uzi wangu,
Kuwa mkweli, angalia clip hiyo, ilikuwa ni gari moja na hadi foleni imekaa!.
P
 
Nimekuelewa kuwa unawaponda! hawajaonyesha live mchakato wa fomu kwa makamanda!! asante kuliona hilo!!!
Mkuu, the Breed, kwanza asante kuchangia uzi wangu.
Pili ni no!, sijawaponda TBC, bali nimekiuliza tuu kuwa hili ni tukio binafsi la chama, TBC ni TV ya umma, kwavile mimi ni mwanahabari nikajua TBC waliambiwa na CCM na wakalitangaza live, hivyo nimewahimiza na vyama vingine vitoe Ushirikiano kwa TBC ili TBC wajue na nikatoa wito kwa TBC as TV ya umma kutenda haki sawa kwa vyama vyote.
Msikilize Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dr. Ayub Rioba hapa alisema nini kuhusu hilo
Dr. Ayub Rioba atoa Mwelekeo wa TBC kwa Mwaka 2018. Kufikisha viwango vya juu kiwango cha BBC
P
 
Huyu MNAFIKI Mkuu anahangaika sana. Njaa imemzidia kikampuni chake kilichokuwa kinapata zabuni za mamilioni toka Ikulu sasa hakipati hata ya senti 10.

Usipo Teuliwa Mwaka Huu Basi Kajifukize Kwanza;

Ila all in all tulishauri humu tukabezwa shughuli za chama kufanyika Ikulu ila naona walio tubeza ndio wengine watamsifia.
 
Una hoja ya msingi Sana kwamba kuwe na mizani sawa kwa wagombea hata kama mmoja wao ni Rais aliye madarakani.

Ngoja wakati wa kampeni tutaona huo mzani kama utakuwa sawa au kuna upande utapata mbeleko ya dola au tume ya uchaguzi.
Mkuu, proved, kwanza asante kuchangia uzi wangu.
Hili ndio lengo la uzi huu kuzungumzia good practices on the way we do things. Amini usiamini, kitendo tuu cha kuonyesha kuwa kuna silent observers somewhere watching you na wanaangalia, inasaidia!.
P
 
Njaa imemzidia kikampuni chake kilichokuwa kinapata zabuni za mamilioni toka Ikulu sasa hakipati hata ya senti 10.

Mkuu, Bubu Ataka Kusema, BAK, kwanza asante kuchangia uzi wangu na kuendelea kusambaza hiyo video clip yangu, kuonyesha who I'm, that is the real me.

Pili msema kweli ni mpenzi wa Mungu, ni kweli kile kikampuni changu cha PPR kilitegemea tenda za serikali na ni kweli tenda hizo zimefutwa pia ni kweli mimi na hicho kikampuni tuna hali ngumu sana, na ni kweli tunakufa njaa, seriously.

Hivyo nawaombeni sana
"Jamani msinicheke wala msinibeze kufilisika, kufilisika si kilema ni matatizo tuu ya dunia au ni mapito"
Pamoja na umasikini huu, naomba tuheshimiane, heshima ya mtu humu isitokane kumpima kwa utajiri au ana nini, bali itokane na michango yake kwa jf.
Kwa vile baadhi ya mabandiko yangu ni ya level nyingine ambayo yanaeleweka only by some wenye Jicho la Tatu ambao wana uwezo to read me in between the lines, most wakifikiri nasaka uteuzi, hii clip yangu wewe unayoizungusha lila uchao, inanisaidia sana kuwafunza hawa madogo humu who is real me and that is the the real Pasco.
Thanks.
P
 
Ikulu ina sehemu mbili,
1. Ni Ofisi ya rais- rais yuko huru kukutana na yeyote na kufanya mkutano wowote na kundi lolote hata mikutano ya CCM au vikao vya Chama, bila kuvunja sheria yoyote, ila kitendo cha kufanyia vikao vya CCM Ikulu, kwa macho ya wapenda haki bin haki, huko ni kutake advantage ya Ikulu yetu kwa manufaa ya CCM, hivyo kama rais ni Mwenyekiti wa CCM na serikali ni serikali ya CCM, na rais yuko Ikulu, hakuna ubaya wowote kwa rais kutake advantage ya Ikulu yetu kwa chama chake kwasababu hajavunja sheria, kanuni wala taratibu yoyote, na kwa kufanya hivyo hata adhibiwa chochote, kwasababu it's doing nothing wrong kisheria, kikanuni na kiutaratibu but morally wrong, hivyo kutokufanyia, vikao vya CCM Ikulu, kunaleta baraka na ustawi zaidi.
2. Ikulu ni makazi ya rais- rais yuko huru kumkaribisha mtu yoyote au kikundi chochote kwa lengo lolote ikiwemo vikao vya Chama, ila kuna eneo la ofisi na eneo la makazi, vikao hivi vikifanyikia eneo la makazi ni haki kabisa, lakini vikifanyikia eneo la ofisi, ni matumizi mabaya ya ofisi kwa advantage ya chama chake, this is not right.

Kwa hili rais Magufuli hakulianza leo
Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!
P
Serikali ya ccm how?katiba ya JMT inasemaje
 
Kusema kweli sijasoma bandiko lako, nimesoma kidogo tu ila ile taito yako tu nikachefwukwa.........kuchukua fomu tu au tendo moja tu ndio lisionekana amefanya kutenganisha shughuli za chama na serikali? mangapi amefanya Ikulu kuhusu chama chake? mangapi? juzi tu bungeni kafanya shughuli za chama akiwa na taito ya Rais? wala hana sababu ya kupongezwa ni usanii tu aliamua kufanya au kaamua kufanya kampeni mapema?

hivi hizi baraka huwa zinamimimika tu kirahisi? au nani huwa anabariki? Paschal muda mwingine una boaaaaaaa
 
Hivi Jana Magufuli alikuwa anahutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania au alikuwa anahutubia mkutano mkuu wa ccm? Na je yeye alisimama kama rais,mwenyekiti wa ccm au alisimama na kofia zake zote mbili?

Yaani nimekijuta nachefwukwa asubuhisubuhi kwa bandiko hili....... Pasco kaniharibia siku........ Miaka yote 5 au hiyo jana tu ni tofauti ya masaa tu mtui kafanya kazi za chama kwenye chombo muhimu kabisa cha Nchi, leo mtu anamsifia.
 
Kisha akatanua.....jamaa wakikimbia kwa pembeni.... akiwa covered kwa nyuma.

Hivi ukitoa namba kwenye gari la ofisi na kuweka zako unakuwa umetumia gari lako binafsi eee.

Makonda alishashutumiwa leo comrade anapewa sifa.
Duuh.........

Alikuwa na gari moja wakati njia nzima walijaa askari wa usalam barabarani na magari ya raia yakawekwa foleni.
 
Wanabodi,

Bandiko hili ni kufuatia hoja ya mwana jf huyu.

Mkuu Yohane Mbatizaji, kwanza asante kwa bandiko hili.
Mimi ni miongoni mwa tuliyemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM katika ofisi Kuu ya CCM Makao Makuu Dodoma leo asubuhi na kuona jinsi alivyoondoka na gari moja la number za kiraia, bila ving'ora wala msafara.

Kwavile sisi binadamu tunatofautiana observation powers, naomba na mimi nichangie nilichokiona kwenye uchukuaji wa fomu huo na kueleza kina maana gani kwa mustakabali mzuri na mwema wa siasa za nchi yetu kuelekea October 2020.
  1. Kwanza ni kule tuu kuonyeshwa live kupitia TBC tukio la rais Magufuli kuchukua fomu, ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima. Kuna msemo wa Kiswahili usemao, " nyota njema huonekana asubuhi" huku kuonyeshea live toka mwanzo is good for transparency.
  2. Uchaguzi huru na wa haki ni process inayohitaji maximum transparency, kwasababu rigging zote za uchaguzi huwezi kufanyika kutokana na lack of transparency, hivyo hii Transparency ni moja ya mambo muhimu sana yanayoufanya uchaguzi uwe huru na wa haki na matokeo kuwa credible na Kukubalika na wote. Mfano kura zote zinahesabiwa kituoni na matokeo ya kila kituo kubandikwa ubaoni transparently, if there is nothing to hide, kwanini vyama vizuiliwe kufanya independent tallying?!.
  3. Kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, TBC imetimiza wajibu wake wa uhabarishaji umma kikamilifu kwa kututangazia live tukio hili ili umma wa Watanzania tushuhudie kwa kuona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu na sio kuambiwa au kuhadithiwa, kuona ni kuamini.
  4. Natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma.
  5. Wito kwa TBC, kwanza hongereni kwa kazi nzuri, mlichokifanya leo ni mwanzo mzuri wa mchakato huu wa urais. Nawaomba mvitendee vyama vyote haki sawa, msifanye upendeleo kwa chama kimoja na kuvibagua vingine, hivyo tunategemea kuona live za wagombea urais wa vyama vingine nao wakiwa coved na TBC
  6. Pia nimemnote rais Magufuli akitumia usafiri wa gari lenye number binafsi. This is very good thing kwasababu rais Magufuli ametenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali. Rais Magufuli hakutumia gari za serikali, wala hakutembea na msafara na ving'ora, ikiwemo battalion, rais Magufuli ametumia gari moja tuu yenye number za kiraia. Hatutarajii kuendelea kuona vikao vya chama vikifanyikia Ikulu yetu!. Hongera sana rais Magufuli, kwa hili utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa sana kwasababu Mungu ni mtenda haki na anapenda haki, huwabariki watenda haki na kuwaadhibu wasio tenda haki!.
  7. Hatua hii ni hatua yenye essence kubwa sana kwenye mustakabali wa usawa wa kidemokrasia na usawa wa uwanja wa mapambano kujenga uwanja sawa, the level playing field, hivyo ni hatua muhimu kuifuta ile dhana ya kugombea urais Tanzania kufananishwa na kugombea kisu cha makali kuwili huku mgombea mmoja ameshika mpini na kuwashikisha wapinzani wake upande wa makali kuwili
  8. Wito kwa Tume yetu ya Uchaguzi, NEC, nawaombeni mfuate mfumo wa usawa wa wagombea urais wa Nordic countries na Scandinavian countries ambapo wagombea wote wa urais wanakuwa treated the same. Kama kuna mgombea ana ulinzi kwasababu yeye ni rais, then wagombea wote wanapewa ulinzi. Kama kuna mgombea ana msafara wakiwemo media, wagombea wote wanapewa misafara, media na logistical support ili wote pafananie, na sio mgombea mmoja ndio anatumia state logistics kwasababu ni rais na wengine wote wapambane na hali zao.
  9. Kuwatendea haki sawa wagombea wote wa urais wa vyama vyote kutapelekea taifa letu kubarikiwa na kupata neema, baraka na ustawi.
  10. Kukipendelea chama kimoja au mgombea mmoja na kutowandea haki sawa wagombea wote wa vyama vyote kutapelekea Taifa kuchapwa na bakora za karma ya upendeleo na kutotenda haki kwa wote.
Nawatakia Jumatano Njema.

Paskali
Watu wengi wanaamini Rais Magufuri ni dictator, siyo mwanademokrasia, anapendelea Ccm. Nawahakikishia Rais Magufuri ata prove it wrong. Nawahakikishia yawezekana Rais Magufuri ataweza kuwa mwanademokrasia kupita Marais wote kwenye huu uchaguzi.

Binafsi naamini vyama pinzani wakichanga karata zao vizuri bunge lijalo litakuwa na wapinzani wengi tu Hadi ikatushangaza.

Refer kwenye hotuba yake kuwa uchaguzi wa safari hii utakuwa wa huru na haki. Naamini ataiprove Duni wrong.
 
Back
Top Bottom