Ponda hali mbaya

Ponda hali mbaya

Status
Not open for further replies.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
attachment.php


Na Mwandishi Wetu

SIKU chache baada ya kupelekwa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar kisha Mahakama ya Mkoa Mrogoro kwa helikopta, hali ya kiongozi na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Shehe Ponda Issa Ponda imedaiwa kuwa mbaya.


Shehe Ponda Issa Ponda.

Agosti 19, 2013 saa 2:12, Shehe Ponda alifikishwa Mahakama ya Kisutu, Dar akitokea Gereza la Segerea ambapo alifutiwa mashitaka ya kuchochea vurugu nchini kati ya Juni 2 na Agosti 10, mwaka huu kwenye maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Morogoro.


Kama hiyo haitoshi, siku hiyohiyo alikimbizwa Morogoro kujibu mashitaka ya uchochezi aliyoyafanya katika mkutano wa hadhara hivi karibuni mjini humo, hali ambayo ilimfanya atoneshe kidonda chake cha risasi aliyodai kupigwa.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu, kutokana na jeraha hilo la risasi alilonalo kiongozi huyo, hekaheka alizozipata siku hiyo zilisababisha atoneshe kidonda na kumfanya ashindwe kusimama wala kulala hadi familia kufikia hatua ya kuomba arudishwe Hospitali ya Muhimbili katika kitengo cha mifupa (Moi) kwa matibabu zaidi.


“Kiukweli hali ni mbaya, wamempeleka harakaharaka tena ghafla, matokeo yake wamemtonesha kidonda. Tunaomba wamrudishe tena Moi (Muhimbili),” alisema mmoja wa ndugu wa familia aliyeomba hifadhi ya jina.

Akiwa Morogoro, alipandishwa kizimbani na kujibu shitaka la kwanza la uchochezi pamoja na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Zanzibar. Agosti 10, mwaka huu kwenye mhadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Ndege, mjini Morogoro, Ponda alidaiwa kuchochea kwa kusema:


“Ndugu Waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa serikali.”
Shitaka hilo liliunganishwa na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Shehe Ponda maeneo ya Dar na Zanzibar.

PONDA HALI MBAYA - Global Publishers
 

Attachments

  • PONDA.jpg
    PONDA.jpg
    31.9 KB · Views: 7,176
angetoneshwa hapo chini ya mgongo, kw ile njia ya vima.. pambaaaf.
 
Ni bora afe tu ili mambo ya udini tusiyasikie tena!!

udini hauta ondoka kwa kufa Ponda ila utaondoka ukiondoka mfumo kristo ambapo nchi itaendeshwa kwa misingi ya haki usawa na bila kujali dini za watu.. tukifika hapo udini utaondoka....
sana akifa ponda ndio matatizo yatazidi....tutachukulia ameuliwa na mfumo ambao hautaki kuona unaondoka
 
Kwa maoni haya, sipati picha ikitokea laana ya CDU kushika madaraka! Nadhani waislamu watakimbia nchi!
 
udini hauta ondoka kwa kufa Ponda ila utaondoka ukiondoka mfumo kristo ambapo nchi itaendeshwa kwa misingi ya haki usawa na bila kujali dini za watu.. tukifika hapo udini utaondoka....
sana akifa ponda ndio matatizo yatazidi....tutachukulia ameuliwa na mfumo ambao hautaki kuona unaondoka


mfumo kristo ni hofu yenu nyie mliokimbia kusoma na msiotaka kufanya kazi. anayewapandikizia hyo sumu ndo huyo ponda ambaye kaishia la 7. waislamu wenye bidii na kujitambua wamefanikiwa bila kusubiri kubebwa na kuzawadiwa vyeo.
Jitambue..
 
udini hauta oondoka kwa kufa Ponda ila utaondoka ukiondoka mfumo kristo ambapo nchi itaendeshwa kwa misingi ya haki usawa na bila kujali dini za watu.. tukifika hapo udini utaondoka....
sana akifa ponda ndio matatizo yatazidi....tutachukulia ameuliwa na mfumo ambao hautaki kuona unaondoka

Mkuu km kweli za kuambiwa unachanganya na zako basi utajua kuwa mfumo kristo hauziiliki kwani upo kila mahali.....upo misri. Syria, iraq, afghanistan, tunisia, somalia ndo maana wanachinjana kwa sbb ya kudai haki ili mfumo kristo uondoke......
Changanya na zako mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom