Ponda apinga Mpango wa Serikali kuweka ulinzi misikitini

Ponda apinga Mpango wa Serikali kuweka ulinzi misikitini

'tatizo kubwa tulilonalo ni mateja tu kuja kuiba ndala kama wanataka waje kutulindia ndala zetu hapo sawa..............lakini sio ndani'

Huo Msikiti unaoibiwa Ndala ni Ile ya KIKATOLIKI/BAKWATA ila misikiti ya Kiislam hawa Gusi wanajua jinsi watu wakikasirika watakavyotembezewa Kichapo/Karate.
 
Ndugu yangu wanachodai waislam n Mahakama ya Kadh itambulike Kisheria means iwepo ndan ya Katba na c vngnevyo.., ss hyo unayozungumzia ww n kiini macho cha Mahakama ya Kadh na co hyo walokua wanaihtaj Waislam...,
Hili wazo halikubaliki labda waliboreshe na kusema Mahakama zote za Kidini zitambuliwe Kisheria ndani ya Katiba,maana hata baadhi ya Madhehebu kama WAKATOLIKI wana Mahakama zao na Rufaa hupitia hatua mbalimbali mpaka hufika kwa Papa.Kwa Ujumla Shekh Ponda na Kundi lake napishana naye kwenye Hoja Dhaifu kama hizi za Mahakama ya Kadhi.
 
Secularism na kadhi vinaendana kweli?? au ndo unataka kusilimisha mpaka katiba?

Hv unajua maana ya kuclmisha ww? Na je hyo Mahakama ya Kadh c itadeal na isue za waislam ambao wanaish Tz na wanahak ya kutambuliwa na Katba yao? Au we mwenzangu unaelewaje?
 
Sawa ulinzi uwepo lakini hilo la kamati kuanza kupitia kwanza mawaidha siliungi mkono ni kuanza kuingiliana kwenye mambo ya kiimani bwana

Hata huu ulinzi ni wa nini? Tangu lini wakasikia msikitini kuna ngumi zinapigwa huko? Kama ni mipango ya kupingana na serikali katika mamboflani serikali wanalaumiwa na waislamu mbona kanisani kuna yanayopingwa na kanisa? Kwanini ulinzi msikitini na sio kanisa.
 
...mh

ama ndio muundo wa Mahakama ya Kadhi unajaribiwa na serikali kabla hawajaupendekeza kwa Waislamu?


Huo inawezekana ukawa muondo wa Mahakama ya Kipagan ila co ya Kadhi!
 
Hili wazo halikubaliki labda waliboreshe na kusema Mahakama zote za Kidini zitambuliwe Kisheria ndani ya Katiba,maana hata baadhi ya Madhehebu kama WAKATOLIKI wana Mahakama zao na Rufaa hupitia hatua mbalimbali mpaka hufika kwa Papa.Kwa Ujumla Shekh Ponda na Kundi lake napishana naye kwenye Hoja Dhaifu kama hizi za Mahakama ya Kadhi.

Sheria iliopo inapinganaje na sheria za kanisa? Tusaidie hapo.
 
Jaribu kuwa Mdadisi Kidogo.Makadhi wameshateuliwa ila Shekh Ponda na Wenzake wanadai hawawatambui kwa sababu wameteuliwa na Shekh Mkuu wa BAKWATA.

Hujuhi kwanini?
Hivi wewe ungekubali maamuzi kufanywa na Taasisi Moja tu ya Kiislam katika Taasisi nyinhgi zilizOpo ?

Mfano wakisema kuna Mkutano wa Wanawake Tanzania, Na Waitwe UWT ya CCM na kufanya Maamuzi kwa niaaba ya Wanawake wote Nchini, Kisa tu wanajina Linalowakilisha Wanawake waTanzania huku si kweli, Ukweli ni kuwa wao ni moja tu ya Taasisi zinazowakilisha wanawake TanzAnia.
 
Kumpa mtu like haimanishi kuwa unakubaliana moja kwa moja na hoja bali kuthamini mchango wake katika uzi uliuanzisha.Tambua hilo.Chamviga ni mwanaccm na mimi ni mwana Chadema lakini penye haki lazima tusimamie haki.Mimi kama mkristo siungi mkono wazo hilo la kijinga la kuratibu mawaidha(za) ya maimamu.Kama hivi ndivyo basi hata sisi wakristo mapadre wetu wahaririwe kwanza kabla hawajasema mbele ya waamini.

Akhsante Mkuu kwa kumuelewesha. Ngoja nikikaa kwenye keyboard utaipata like yangu.
 
SHEIKH PONDA AIBUA MAPYA
''Hakika mpango huo ni ajenda ya siri kwa waumini wa kiislam, serikali ijibu imekusudia nini kwa uwazi kwa waislam wa Tanzania, wapi duniani ama kwa dunia ya uislam kamati za namna hii zipo? serikali iwe makini vinginevyo itabaki na wasiokuwa waislam na waislam watafutiwe na serikali Tanzania yao''

*Apinga mpango wa serikali misikitini


KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibua mapya baada ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kusitisha hatua ya Serikali ya kuunda Kamati za Ulinzina Usalama misikitini.
Katika barua yake kwa Waziri Mkuu Pinda aliyoisambaza jana kwa vyombo vya habari, Sheikh Ponda anapinga hatua ya Serikali kuunda mpango huo.
Kutokana na hali hiyo, ameshauri Serikali itoe tamko la kuusitisha mpango huo, ili misikiti iendelee na taratibu zake za kidini na kamati za ulinzi na usalama zibaki katika ngazi ya Serikali.
Amesema Waislamu kama walivyowanajamii wengine, watakapohitaji usalama kwa ajili yao, watafuata taratibu zilizowekwa na Katiba zao na Katiba za nchi na si vinginevyo.
"Sisi kama kikao cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, tunapenda kukujulisha hatua tulizochukua kuihami jamii ya kiislamu na madhara ya mpango huu. Tumeiandikia barua hii Serikali itoe tamko la kusitisha mpango wake huu.
"Ieleweke kwamba, Uislamu ni dini huru na uhuru huo unatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una fikra, misingi na taratibu zake.
"Mpango huu wa Serikali, umeonyesha dhana ya utumwa na ukandamizaji, kwani inapofikiahatua ya Serikali kuunda mtandaondani ya misikiti unaolenga kuwasimamia maimamu, masheikh, wahadhiri na wasemajiwengine wa kiislamu, waseme nini na waumini wasikilize nini.

"Na endapo watasema kile ambacho hakipendwi na Serikali yako, basi wadhibitiwe na vyombo vya ulinzi na usalama, hatua hiyo ni kinyume kabisa na uhuru wa dini na misingi ya amani na utulivu," ilisema sehemuya taarifa hiyo.
Sheikh Ponda katika barua yake hiyo, anasema historia inaonyesha kuwa, Tanzania kumekuwa na uvunjaji wa amani na sheria na haki za kiimani ambapo kwa upande wa Waislamu, wanaona huo utakuwani mwendelezo wa historia hiyo ya dola kuvunja haki za kuabudu dhidi yao.
Akitolea mfano, alisema mwaka 1963, Serikali ilipiga marufuku Mahakama ya Kadhi ambacho ni chombo chenye mamlaka ya kutatua mambo ya kiimani na kushughulikia mambo ya ndoa, talaka, mirathi, mali za wakfu, wanawake, malezi ya watoto na usuluhishi.
Alisema kwamba, majukumu hayomsingi wake ni Quran na sunna, lakini pia pamoja na kutambua ukweli huo, Katiba inatamka wazi kuwa, hayo si majukumu ya Serikali, lakini Serikali imeyachukua na kuyakabidhi katika Mahakama.
"Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kupitia Jeshi la Polisi, imeainisha mpango huo ndani ya nyumba za ibada ambapo kwa Waislamu umeanza kutekelezwa kati ya Jeshi la Polisi na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
"Mufti wa BAKWATA, Sheikh Issa Shaaban Simba, alinukuliwa na vyombo vya habari akiishukuru Serikali kwa mpango huo na pia amesema utekelezaji umeanza kwa kusambazwa waraka wa maelekezo katika misikiti yote nchini.
"Ndugu Waziri, sisi Waislamu chiniya kikao chenye hadhi ya mjumuiko wa jumuiya na taasisi za kiislamu, tumeonelea tukuandikie kukueleza kupinga zoezi hilo, kwani linaingilia uhuru wa kuabudu unaohifadhiwa chiniya Katiba ya nchi," inaeleza barua hiyo.
Aidha, Sheikh Ponda alisema zipo taarifa mpya za hatua za uimarishaji wa mpango huo kati ya BAKWATA na Serikali, ambapo muislamu mmoja alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Msemaji wa Mufti wa Baraza hilo, akitakiwa aende katika hoteli aliyokuwa amefikia Sheikh Mkuu katika wilaya moja nchini.
Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, Sheikh Mkuu aliwahi kufukuzwa katika ngazi ya uongozi wa BAKWATA wa wilaya.

Katika utekelezwaji wa mpango huo kati ya Serikali na BAKWATA, Sheikh Ponda anasema tayari Wilaya ya Namtumbo, Kijiji cha Rwinga, Mkoa wa Ruvuma, Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Smith James, aliitisha mkutano uliohusisha viongozi wa dini na Serikali.
Ameendelea kusema kuwa, katika mkutano huo yalitolewa maelekezo ya Serikali ya kuundwakwa Kamati za Ulinzi na Usalama ndani ya nyumba za ibada.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Polisiwa Wilaya (OCD), aliyemtaja kwa jina moja la Mwakasanga, aliwaelekeza viongozi wa dini utaratibu wa kuunda kamati hizo pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe.

"Majukumu ya kamati hizo yaliyoainishwa ni kwamba, kamatiitamhoji muislamu yeyote atakayetaka kuzungumza na Waislamu ndani ya eneo la msikiti na wasiporidhika, watamzuia na kuwasiliana na ofisa usalama wa wilaya.
"Kamati itamhoji sheikh au imamukutoka msikiti mwingine kabla ya kuruhusiwa kuongea na waumini,pia kamati itapitia hotuba ya sala ya Ijumaa katika msikiti husika kabla imamu hajaisoma kwa waumini.

"Kamati za ulinzi na usalama ndizo pekee zitakazokuwa na majukumu ya kuomba kibali serikalini kwa ajili ya mikutano yote ya ndani na nje ya Waislamu na mwisho, aliwaagiza wajumbe wa kikao kuwasilisha taarifa kamili kwa kamati hizo ofisini kwake.
"Mwenendo kama huu, kama tulivyoona katika rejea mbalimbalihuko nyuma, ambao umedumu nakuendelezwa na Serikali za awamu zote nne, kwa kiasi kikubwa umejenga mahusiano mabaya kati ya Waislamu na Serikali," alisema Sheikh Ponda.
Nakala ya barua hiyo ipo kwa Waziri wa Mamboyandani.
[/QUOTE]
 
Umeongea Mambo Mengi ya Msingi kasoro kwenye Nyekundu.Ni bora huu Ushauri ukampa Shekh Ponda na Kundi lake wakiwemo baadhi ya Maprofesa.Mambo ya Kidini yafanywe na Dini husika tu bila kuhusisha Serikali.Namuunga Mkono Shekh Ponda kwa Mambo Mengi sana kasoro ni pale anapolazimisha Dini yake ionekane na kila Mtu kwamba ndio Dini Bora.

'Soma BUNGE lako hili

Hoja ya Bunge kupitisha sheria ya
kurudisha ofisi ya Kadhi Mkuu
linajitokeza tena huku
waislamu wakitaka Bunge
litunge sheria ya kutambua
uwepo wake na wakristu
wakipiga kelele
kuwa kufanya
hivyo ni kuvunja Katiba. Hoja
yangu leo ni kuwa, Waislamu
hawahitaji kibali cha serikali
kuanzisha ofisi ya Kadhi Mkuu
kushughulikia mambo yao
yanayoendana na sheria za
Kiislamu.
Waislamu wakae wao
wenyewe
wapitishe uwepo wa
ofisi hiyo na kuendelea na
shughuli zao. Ilimradi tu,
maamuzi ya ofisi yao hiyo
hayaingilii uhuru wa
Mtanzania mwingine
au
utendaji kazi wa sheria zetu za
makosa ya uhalifu na jinai. Pia
waelewe ya kwamba uwepo
wa ofisi ya Kadhi Mkuu ni
subject ya Katiba ya
Muungano
na Mtanzania
yeyote kimbilio lake la mwisho
ni mahakama ya Kiraia. Zaidi
ya yote, watakapoanzisha ofisi
hiyo, wajue kuwa
isiwalazimishe waislamu wote
kutatua matatizo yao kupitia
ofisi hiyo isipokuwa wale
ambao kwa hiari yao
wanataka kufanya hivyo.
Kanisa Katoliki kwa mfano
linayo mahakama yake
na
sheria zinazoliongoza kanisa
hilo (Canon Law) na
mahakama yake hiyo ina ngazi
za rufaa hadi Vaticano. Hata
hivyo Mkatoliki ana haki ya
kutumia sheria hizo kuhusu
masuala mbalimbali ya kanisa
lake
lakini anapofanya kosa la
jinai, sheria za kiraia (civil law)
zinakuwa na mamlaka. Hivyo
basi, waislamu wasisubiri
Bunge kupitisha ofisi ya Kadhi
Mkuu bali waianzishe wao
wenyewe
huku wakiweka
bayana kabisa kuwa ofisi hiyo
haitahusika na makosa ya jinai
au kupingana na Katiba ya
nchi. Then, hakutakuwa na
haja ya kugongana!!!

source: Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
wao wanakaa tu hata hawashiriki mnayofanya? Ponda saivi kaelekea wapi vile?
Kuna maofisa wa serikali wengi tuu katika nyumba za Ibada, haikuwa Issue, lakini hili la serikali kuanzisha kamati officially za ulinzi ndilo tatizo. Wanataka kutuletea mambo ya Green Guard misikitini na makanisani kupenyeza UCCM wao
 
Mi sioni kama kunatatizo kwa kuanzisha kamati za ulinzi kwenye nyumba za ibada.
kwa sababu kuu zifuatazo:-
1. sio wote wanaokwenda kanisani ni wakisto
2. sio wote wanakwenda misikitini ni waislamu
Sasa ukitafakari sababu hizo ndio utajua kuwa huitaji elimu ya ziada kufahamu kwanini zianzishwe kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada.

Hoja yako mfu na iNaelekea wewe Huna Dini.

Hakuna dini Duniani inayokataa wageni au waumini wageni kuingia au kushiriki Ibada za+, Labda kama ni Ibada ya siri ya shetani au huko Freemason.
 
Tafadhali Toa mfano ni wapi au ni kipi alikifanya au kukitenda kuashiria Dini yake ni Bora kuliko za wengine?

Ni kutendo cha kutaka Mahakama ya Kadhi(Kiislamu) iingizwe kwenye katiba na kuzipuuza Dini zingine wakati nazo zina Mahakama zao.
 
Je hayo yanayo somwa Nchi nzima yamekaguliwa na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Kijiji/ Mtaa? OCD anajua kinasomwa nini sikuhiyo?

Embu tuoneeni huruma nyinyi Ndugu zetu U-SLAM nchi hii umetekwa MACCM chini ya BAKWATA iliyoundwa na MKRISTO NYERERE.

Kwanini hamna huruma? Hivi Kweli YESU anakubaliana na haya tunayofanyiwa waislam wa Tanzania?

Yaani pamoja na dhulma wanazofanyiwa waislamu na watanzania kwaujumla na serikali yetu bado mimi naiunga mkono ccm kwakuwa wakristo ambao wamejaa chadema hawanaga huruma kabisa na mateso na fuatiliafuatilia wanazokumbana nazo toka huko nyuma mpaka yanayoendelea hapa Tanzania. Lau wafuasi hawa wangeelewa hili wakapunguza chuki na uislamu na waislamu wakaisimamia haki chadema kingeungwa mkono na kila mtanzania na ukombozi usingechelewa. Ila asili inawahukumu wakristo.
 
Sheria iliopo inapinganaje na sheria za kanisa? Tusaidie hapo.

Lengo sio kupingana bali ni kutafuta sheria ambayo unaweza kuijengea hoja na mtu mwenye uelewa akaridhika.Nikirejea kwenye swali lako,kuna baadhi ya Sheria za Nchi ambazo Kanisa halizipendi lakini zinatumika mf.Hukumu ya Kifo na Ndoa za wake Wengi.
 
Lengo sio kupingana bali ni kutafuta sheria ambayo unaweza kuijengea hoja na mtu mwenye uelewa akaridhika.Nikirejea kwenye swali lako,kuna baadhi ya Sheria za Nchi ambazo Kanisa halizipendi lakini zinatumika mf.Hukumu ya Kifo na Ndoa za wake Wengi.

Hukumu ya kifo inapingana na kanisa au injili ya yesu au zabur au taurati?
 
Yaani pamoja na dhulma wanazofanyiwa waislamu na watanzania kwaujumla na serikali yetu bado mimi naiunga mkono ccm kwakuwa wakristo ambao wamejaa chadema hawanaga huruma kabisa na mateso na fuatiliafuatilia wanazokumbana nazo toka huko nyuma mpaka yanayoendelea hapa Tanzania. Lau wafuasi hawa wangeelewa hili wakapunguza chuki na uislamu na waislamu wakaisimamia haki chadema kingeungwa mkono na kila mtanzania na ukombozi usingechelewa. Ila asili inawahukumu wakristo.

Jiunge na CUF.Au Julius Mtatiro anakukwaza?
 
Back
Top Bottom