Ponda apinga Mpango wa Serikali kuweka ulinzi misikitini

Ponda apinga Mpango wa Serikali kuweka ulinzi misikitini

Mi sioni kama kunatatizo kwa kuanzisha kamati za ulinzi kwenye nyumba za ibada.
kwa sababu kuu zifuatazo:-
1. sio wote wanaokwenda kanisani ni wakisto
2. sio wote wanakwenda misikitini ni waislamu
Sasa ukitafakari sababu hizo ndio utajua kuwa huitaji elimu ya ziada kufahamu kwanini zianzishwe kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada.
Soma tena thread, usiishie kusoma heading tuu.
Moja ya kamati hiyo inayoanzishwa ni kupitia hotuba ya shekh kabla hajahutubia waumini wake kwenye ibada wanazofanya.
Hii ni too much.
 
ningemshauri mheshimiwa rais wetu hebu amwite Ponda akae nae amuulize anataka nini yy kama mtanzania na yy kama kiongozi wa kiislamu.

swala la ulinzi msikitini eti kuhoji kila anayeingia mskitini na mawaidha kusomwa kabla na kikos cha ulinzi ndipo wasomewe waumini ni kuharibu utaratibu wa ibada na pia ni kuharibu uhuru wa waumini.

kama serikali inahaofu na huyu Ponda bado inauwezo wa kukaa nae na kujua nini hasa kinachomfanya a-act kama afanyavyo.

Mkuu gfsonwin. Mimi napingana na baadhi ya mambo anayosimamia au anayoamini. Ila ana mambo ya muhimu sana ambayo serikali imekuwa muda mrefu ikidharau na badala yake kushughulikia matokeo ya matatizo hayo. Haiwezekani kabisa kunipangia khutba ya kuwasilisha kwa waumini. Kwakweli hili ni too much! Naamini kama likipitishwa halitokuwa na matokeo mazuri. Hasa mashekh au imamu wakianza kukamatwa na kuhojiwa au kushtakiwa kwa sababu ya khutba aliyotoa.
 
Last edited by a moderator:
Haya sasa BAKWATA wameanza kumtumikia bwana wao MAGAMBA kuelekea 2015. Eti kamati ya ulinzi inamuhoji na kupitia hotuba yote ya mawaidha ya mgeni husika, hii nimeiskia Tanganyika tu.
 
Mkuu gfsonwin. Mimi napingana na baadhi ya mambo anayosimamia au anayoamini. Ila ana mambo ya muhimu sana ambayo serikali imekuwa muda mrefu ikidharau na badala yake kushughulikia matokeo ya matatizo hayo. Haiwezekani kabisa kunipangia khutba ya kuwasilisha kwa waumini. Kwakweli hili ni too much! Naamini kama likipitishwa halitokuwa na matokeo mazuri. Hasa mashekh au imamu wakianza kukamatwa na kuhojiwa au kushtakiwa kwa sababu ya khutba aliyotoa.
kimsingi serikali inakosea sana kutumia mabavu kwa huyu mtu badala ya kutumia diplomsia.
cha ajabu ni kwamba sasa wanataka kuadhibu waislamu wote kwa kosa la mtu mmoja jambo ambalo ni kuwakosea waislamu wote. tena serikali iwe makini manake yawezekana kabisa baadhi ya waislam wenzie ni wahanga wa haya anayoyafanya huyu Ponda.

ningeshauri uhuru a kuabudu na kushiriki ibada usiingiliwe kiasi cha kuwafanya waislamu washindwe kushiriki kwenye ibada zao.
 
SHEIKH PONDA AIBUA MAPYA

*Apinga mpango wa serikali misikitini


KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibua mapya baada ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kusitisha hatua ya Serikali ya kuunda Kamati za Ulinzina Usalama misikitini.
Katika barua yake kwa Waziri Mkuu Pinda aliyoisambaza jana kwa vyombo vya habari, Sheikh Ponda anapinga hatua ya Serikali kuunda mpango huo.
Kutokana na hali hiyo, ameshauri Serikali itoe tamko la kuusitisha mpango huo, ili misikiti iendelee na taratibu zake za kidini na kamati za ulinzi na usalama zibaki katika ngazi ya Serikali.
Amesema Waislamu kama walivyowanajamii wengine, watakapohitaji usalama kwa ajili yao, watafuata taratibu zilizowekwa na Katiba zao na Katiba za nchi na si vinginevyo.
“Sisi kama kikao cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, tunapenda kukujulisha hatua tulizochukua kuihami jamii ya kiislamu na madhara ya mpango huu. Tumeiandikia barua hii Serikali itoe tamko la kusitisha mpango wake huu.
“Ieleweke kwamba, Uislamu ni dini huru na uhuru huo unatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una fikra, misingi na taratibu zake.
“Mpango huu wa Serikali, umeonyesha dhana ya utumwa na ukandamizaji, kwani inapofikiahatua ya Serikali kuunda mtandaondani ya misikiti unaolenga kuwasimamia maimamu, masheikh, wahadhiri na wasemajiwengine wa kiislamu, waseme nini na waumini wasikilize nini.

“Na endapo watasema kile ambacho hakipendwi na Serikali yako, basi wadhibitiwe na vyombo vya ulinzi na usalama, hatua hiyo ni kinyume kabisa na uhuru wa dini na misingi ya amani na utulivu,” ilisema sehemuya taarifa hiyo.
Sheikh Ponda katika barua yake hiyo, anasema historia inaonyesha kuwa, Tanzania kumekuwa na uvunjaji wa amani na sheria na haki za kiimani ambapo kwa upande wa Waislamu, wanaona huo utakuwani mwendelezo wa historia hiyo ya dola kuvunja haki za kuabudu dhidi yao.
Akitolea mfano, alisema mwaka 1963, Serikali ilipiga marufuku Mahakama ya Kadhi ambacho ni chombo chenye mamlaka ya kutatua mambo ya kiimani na kushughulikia mambo ya ndoa, talaka, mirathi, mali za wakfu, wanawake, malezi ya watoto na usuluhishi.
Alisema kwamba, majukumu hayomsingi wake ni Quran na sunna, lakini pia pamoja na kutambua ukweli huo, Katiba inatamka wazi kuwa, hayo si majukumu ya Serikali, lakini Serikali imeyachukua na kuyakabidhi katika Mahakama.
“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kupitia Jeshi la Polisi, imeainisha mpango huo ndani ya nyumba za ibada ambapo kwa Waislamu umeanza kutekelezwa kati ya Jeshi la Polisi na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
“Mufti wa BAKWATA, Sheikh Issa Shaaban Simba, alinukuliwa na vyombo vya habari akiishukuru Serikali kwa mpango huo na pia amesema utekelezaji umeanza kwa kusambazwa waraka wa maelekezo katika misikiti yote nchini.
“Ndugu Waziri, sisi Waislamu chiniya kikao chenye hadhi ya mjumuiko wa jumuiya na taasisi za kiislamu, tumeonelea tukuandikie kukueleza kupinga zoezi hilo, kwani linaingilia uhuru wa kuabudu unaohifadhiwa chiniya Katiba ya nchi,” inaeleza barua hiyo.
Aidha, Sheikh Ponda alisema zipo taarifa mpya za hatua za uimarishaji wa mpango huo kati ya BAKWATA na Serikali, ambapo muislamu mmoja alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Msemaji wa Mufti wa Baraza hilo, akitakiwa aende katika hoteli aliyokuwa amefikia Sheikh Mkuu katika wilaya moja nchini.
Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, Sheikh Mkuu aliwahi kufukuzwa katika ngazi ya uongozi wa BAKWATA wa wilaya.

Katika utekelezwaji wa mpango huo kati ya Serikali na BAKWATA, Sheikh Ponda anasema tayari Wilaya ya Namtumbo, Kijiji cha Rwinga, Mkoa wa Ruvuma, Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Smith James, aliitisha mkutano uliohusisha viongozi wa dini na Serikali.
Ameendelea kusema kuwa, katika mkutano huo yalitolewa maelekezo ya Serikali ya kuundwakwa Kamati za Ulinzi na Usalama ndani ya nyumba za ibada.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Polisiwa Wilaya (OCD), aliyemtaja kwa jina moja la Mwakasanga, aliwaelekeza viongozi wa dini utaratibu wa kuunda kamati hizo pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe.

“Majukumu ya kamati hizo yaliyoainishwa ni kwamba, kamatiitamhoji muislamu yeyote atakayetaka kuzungumza na Waislamu ndani ya eneo la msikiti na wasiporidhika, watamzuia na kuwasiliana na ofisa usalama wa wilaya.
“Kamati itamhoji sheikh au imamukutoka msikiti mwingine kabla ya kuruhusiwa kuongea na waumini,pia kamati itapitia hotuba ya sala ya Ijumaa katika msikiti husika kabla imamu hajaisoma kwa waumini.

“Kamati za ulinzi na usalama ndizo pekee zitakazokuwa na majukumu ya kuomba kibali serikalini kwa ajili ya mikutano yote ya ndani na nje ya Waislamu na mwisho, aliwaagiza wajumbe wa kikao kuwasilisha taarifa kamili kwa kamati hizo ofisini kwake.
“Mwenendo kama huu, kama tulivyoona katika rejea mbalimbalihuko nyuma, ambao umedumu nakuendelezwa na Serikali za awamu zote nne, kwa kiasi kikubwa umejenga mahusiano mabaya kati ya Waislamu na Serikali,” alisema Sheikh Ponda.
Nakala ya barua hiyo ipo kwa Waziri wa Mamboyandani.


toka huyu anayeitwa 'BAKWATA' awekwe kusimamia mambo ya waislam, imekuwa ni kero tupu, hakika ni dhambi kubwa ya ushirikina kuongozwa na sheria za kitwahut..muongozo wa mwislam ni kuran na suna tu...vingine vyote ni ukafiri. huu ndio msimamao wa dini ya kiislam, ila ukisemwa unaonekana ni uchochezi na ugaidi, hakika hawatoacheni kukupigeni vita mpaka wahakikishe wamewatoa kwenye dini yenu ya uislam...
 
nyinyi mnalindwa sawa jee na hotuba ya padri imepita kituo cha polisi kwanza ?

mkuu padri hua hana hotuba, wanafanya mahubiri na husoma kitu kimoja dunia nzima kwa siku!.
make references juu ya mapadri
 
kimsingi serikali inakosea sana kutumia mabavu kwa huyu mtu badala ya kutumia diplomsia.
cha ajabu ni kwamba sasa wanataka kuadhibu waislamu wote kwa kosa la mtu mmoja jambo ambalo ni kuwakosea waislamu wote. tena serikali iwe makini manake yawezekana kabisa baadhi ya waislam wenzie ni wahanga wa haya anayoyafanya huyu Ponda.

ningeshauri uhuru a kuabudu na kushiriki ibada usiingiliwe kiasi cha kuwafanya waislamu washindwe kushiriki kwenye ibada zao.

Sidhani kama haya yanatokea kwa sababu ya harakati za Ponda pekee kwakuwa kama Ponda angekuwa tatizo kwa amani au mvunjaji wa amani sheria isingemuachia aendelee kupitapita mtaani. Hapa napata ukakasi nini hasa makusudio ya serikali au alietoa hili wazo.
 
Je Policcm wao ni Mungu unayejua nani mkristo na nani sio mkristo au Muislamu na sio muislamu? Suala la ulinzi ni la waumini wenyewe, sio serikali iweke watu wake

wewe jikomboe kutoka katika huo umaskini wa fikra, shughuli ya siku moja tu ya harusi huwa kuna kamati ya ulinzi, itakuwa shuguli za kila siku za ibada, badilika acha kuwa na mawazo mgando. this is 4 ur own good.
 
wewe jikomboe kutoka katika huo umaskini wa fikra, shughuli ya siku moja tu ya harusi huwa kuna kamati ya ulinzi, itakuwa shuguli za kila siku za ibada, badilika acha kuwa na mawazo mgando. this is 4 ur own good.

Good gani mkuu Kuwaandalia watu cha kuzungumza?
 
wewe jikomboe kutoka katika huo umaskini wa fikra, shughuli ya siku moja tu ya harusi huwa kuna kamati ya ulinzi, itakuwa shuguli za kila siku za ibada, badilika acha kuwa na mawazo mgando. this is 4 ur own good.
Je hiyo kamati ya ulinzi katika harusi, inawekwa na serikali? Suala la ulinzi ni la waumini wenyewe, sio kushurutishwa na serikali. Get out of the CCM box and see the world, it doesn't need a form VI education to know right and wrong
 
Tatizo la Shekh Ponda haelewi anachopigania.Wakati anapinga kamati ya Ulinzi na Usalama Misikitini inayoratibiwa na Serikali,Anataka Mahakama ya Kadhi inayohudumiwa na Serikali.Ponda,Mpe Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yake Mungu.
 
sasa kwani kuimarisha ulinzi ni kosa tena, jaman watanzania mbona kila kitu mnalalamika, mbona sisi hapa arusha Kanisa kotoliki siku ya j pil tunalindwa japokuwa kanisa letu liko karibu sana na makao makuu ya polisi, polis hutanda kila kona kukukikisha ibada inamalizika kwa usalama na magari ya waumini yako salama,

'na padre kabla hajahubiri hao polisi wanayapitia hayo mahubiri au wanamuhoji na wasiporidhika wanamstopisha au.............wee kababu bwana usiongee kama kabibi bwana'
 
Last edited by a moderator:
Wangeweka JW au Police kulinda viatu na magari nje, lakini sio kamati ya Ulinzi. Huo ni kuingilia uhuru wa waumini

'si wanasema kuwa serikali huwa haina DINI sasa hizi kamati za serikali za ulinzi mpaka misikitini zinafata nini..................na huyu jamaa MIZENGWE ILIYOPINDA si mkristo huyu kwa nini asiwape ulinzi wakristo wenzake anajifanya kujipenyeza kwa WAISLAM huku kuna mhusu nini au nye.ge tu,pambaaaf'
 
'mwehu wewe na babako bwe.ge wee...'

Mkuu Mwanahip. Naelewa unavyojisikia kwenye mambo kama haya ila jaribu kupunguza jazba na naamini pia upo ndani ya funga kwahiyo maandishi yanaweza kukuhukumu ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom