Vijana wa miaka 17-35+ Ndio wanaongoza kunywa pombe

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Habari za uzima wakuu!

Kwa Sasa kundi kubwa sana la vijana wanaokunywa pombe ni hili rika la kuanzia miaka17-27.

Kundi hili ukubali ukatae ndilo Lina idadi kubwa ya watu wanaokunywa pombe kuzidi umri wowote ule.

Ukichukua vijana 10 wa miaka17-27 kati 6-7 wanatumia pombe.

Kwenye sherehe nyingi sana hata kwenye kumbi za starehe kundi kubwa ni hili la miaka17-27 si mabinti Wala vijana wa kiume wote ngoma droo

Jana nimehudhuria party flani kulikuwa na pombe ya kujimiminia kwenye mitungi Tani Yako (sijui special name) nilichokishuhudia ndo hiki almost walikuwa wanakunywa pombe ni miaka hii 17-35 zaidi ya hili kindi ni mmoja mmoja sana wa miaka 40+.

Najiuliza shida Nini ?
Kipindi Cha nyuma kwenye miaka ya 2005 kijana kumkuta anakunywa pombe ilikuwa ni nadra sana labda MACHIMBONI na ZIWANI Kwa wavuvi ndo Unakuta hivo na hii Wala ilikuwa haishangazi maana kule tuna chukulia Kwa watu walioshindikana.

Mimi siisemi vibaya pombe maana namimi ni mdau mzuri tu. Nachokiwaza na kufikiria Nini haswa kimechangia vijana wamekuwa walevi kiasi hiki?

Takwimu zangu eneo ninalo fanya kazi

Vijana kati ya miaka18-30 walio fukuzwa kazi Kwa kosa la kuja wamelewa kazini Kwa mwaka huu 2023 Ni vijana 11 wengi wao hawajaoa.

Vijana wa miaka30+ walio fukuzwa kazi Kwa ulevi ni 3.

Nini shida hasa? Ukizingatia ajira ni ngumu sana kuzipata lkn kijana anaipata na anaichezea!?

Wewe unadhani shida Iko wapi?
Nini kifanyike kuokoa Hawa vijana wenzetu ambao Taifa linawahitaji sana Kwa uzalishaji na maendeleo ya family zao?

Karibuni

Ahsanteen Sana

NB: Miti ya mtunda ni muhimu sana jitahidi upande miti.
 
Hao unawasongizia pesa watowe wapi labda wanakunywa gongo tu, njoo hapa bar zimejaa wa baba kuanzua 45 hadi 65 watu wazima wana magari yao
Mkuu soma Hadi mwisho. Jana kulikuwa na pombe za Bure watu wamekunywa mbaya sna. Pia elewa hata gongo ni pombe. Japo pia usichukulie Kila sehemu uchumi upo sawa hapana.

Mwezi wa5 tembelea Kanda ya ziwa maeneo ya kahama vijijin uone bar zinavyoazishwa utashangaa wakivuna mpunga hutokaa uamini. Gunia la mpunga Kwa Sasa 140+ akiuza 2 Hilo balaa lake hao wazee wake wakae pembeni Kwa muda. Huo ndio ukweli
 
Nikweli mkuu. Sababu kubwa ni kuwa wengi wao hapo ni graduates na wapo mitaani hawana ramani so stress na depression ndio zimewasonga. Njia pekee wanayoiona ni bora kulewa kupunguza msongo wa mawazo. Japo in reality ndio hali inazidi kuwas mbaya.

serikali ilikata viroba ila sasa vimewekwa kwenye vikopo watu wanajipimia tu vya jero jero.
 
kunamadogo Jana nimewalipa helazao kilamtu elfu 65 chakushangaza hawajaenda mbali wameenda jirani kunabaa napita naona wamechafua meza navaibu kibao nimecheka sanaa
Huo ndio uhalisia kabisa pesa kidogo tu vibe lake hutokaa uamini wewe hata ukiwa na m1 yeye ana 100k kaa mbepeni kwanza.
 
Back
Top Bottom