Pombe za Kienyeji Kuanza Kutengenezwa kwa Teknolojia ya Kisasa ili Kukidhi Viwango vya Ubora kwa Watumiaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

SERIKALI INA MKAKATI WA KUWAWEZESHA WAZALISHAJI WA POMBE ZA KIENYEJI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA

"Hadi kufikia mwezi Oktoba 2022 jumla ya leseni 43 za ubora zimetolewa kwa bidhaa mbalimbali za Pombe za kienyeji zilizokidhi viwango na maombi mengine mapya 22 yapo kwenye hatua mbalimbali za tathmini kuelekea kupata ithibati ya ubora." - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea kutengeneza viwango vya Pombe za kienyeji kwa kadiri ya Mahitaji yatakavyojitokeza" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Suala la Pombe za kienyeji ni kwa lengo la kulinda viwanda vyetu vya ndani, kulinda ubunifu wa watu wetu, kuongeza ajira na kuongeza uchumi kwa ajili ya kulinda mawazo yaliyozalishwa na wananchi wetu" - Mhe. Condester Sichalwe

"Je, ni upi mkakati wa Serikali mmeshaanza kuzipatia leseni zile Pombe ambazo mmezikataza kutumika kwenye jamii mfano Gongo?" - Mhe. Condester Sichalwe

"Je, kwanini Serikali isiongeze kodi kwenye Pombe zote zinazoingizwa kutoka nje zenye Sprit ili kwa ajili ya kuzipa thamani Pombe za ndani na kuwavutia wawekezaji waje wawekeze kwenye Pombe za ndani" - Mhe. Condester Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Serikali ina mkakati madhubuti ambapo mojawapo ni kuona namna ya kuwasaidia kuwafundisha na kuwawekea Teknolojia sahihi ili waweze kuzalisha Pombe za kienyeji zinazokidhi viwango ambavyo vitakuwa havina madhara kwa walaji" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Kupitia TBS na SIDO tumeshaweka fedha katika bajeti ambayo itatumika kama ruzuku kuwafuata wazalishaji wa Pombe za kienyeji na kuwafundisha namna ya kuzalisha Pombe zinazokidhi viwango ili ziweze kuendelea kutumika katika maeneo mbalimbali" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Pombe zilizokuwa na madhara na kupigwa marufuku tutawasaidia ili athari isijitokeze na baada ya hapo zitaruhusiwa na kupewa ithibati ya ubora" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Serikali inafanya juhudi mbalimbali pamoja na kufungua biashara huru kutokana na taratibu na kanuni zilizopo kwa kuruhusu bidhaa kutoka nje ya nchi kama ambavyo sisi tunauza nje ya nchi bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

"Tutaendelea kuweka mkakati madhubuti kulinda viwanda vya ndani pale ambapo tutaona inatakiwa kufanya hivyo, tutafanya hivyo ili kuwasaidia wananchi kuinua kipato ili kuinua uchumi wa nchi yetu" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Aidha, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk Mwigulu Nchemba ameahidi kuifanyia kazi hoja ya kodi kuongezwa kwenye pombe zinazotoka nje ya nchi na kwamba majibu yatatolewa wakati wa kutoa kauli ya Serikali kuhusu bajeti kuu ya mwaka 2023/2024.

Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 05, 2023 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuongeza kodi kwenye pombe zote zinazoingizwa kutoka nje ili kuzipa thamani zile za ndani na kuvutia wawekezaji kwa nia ya kulinsa soko la ndani.
 
Attachments

  • Bunge.mp4
    35.5 MB
  • WhatsApp Image 2023-06-05 at 16.03.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-05 at 16.03.06.jpeg
    164.8 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-06-05 at 17.45.42.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-05 at 17.45.42.jpeg
    30 KB · Views: 7
  • FtB4ty1XgAAobVA.jpg
    FtB4ty1XgAAobVA.jpg
    42.1 KB · Views: 7

Itaondoa ule ukienyeji na kuleta ukisasa hence new product!
 
Back
Top Bottom