Binafsi Dr.Pombe huwa namkubali ktk utendaji wake. lakini kwa hili la daraja la Mbutu sincerely sitomkubali. jana katika kumnadi Dr.kafumuka Dr. Pombe alisema katika budget ya 2011/2012 wizara yake imepanga budget ya kulijenga daraja hilo na ameenda Igunga ili awe km mwarobaini wa matatizo yanayotokana na daraja hilo.
Ukitafakari kw umakini utaona huu ni usanii mkubwa, ukizingatia kuwa matatizo yatokanayo na daraja hilo hajaanza leo ni ya miaka nenda rudi. Leo kwa sababu kuna uchaguzi mdogo ndo wameliona hilo na wanakuja na propaganda eti sasa dawa yake inapatikana. kwa taarifa nilizonazo daraja hili liko chini ya Council ambamo mbunge ni mjumbe ktk vikao vihusuvyo maendeleo ya wilaya.
Kwa miaka takiribani 18 RA alikuwa mbunge na ni mjumbe wa council, je, walishindwa kutenga mafungu ya kulijenga daraja hilo? Ama kwa ukwasi aliotuibia huyu jamaa alishindwa kweli kutenga vijisent km 1b kuwakwamua wananchi wake kutokana na matatizo yanayowasibu? Huu jamani ni ujanja wa kuwarubuni watu.
Ndg wanajamvi naomba kuwasilisha.