Pombe na daraja la Mbutu

GINHU

Member
Feb 7, 2011
68
14
Binafsi Dr.Pombe huwa namkubali ktk utendaji wake. lakini kwa hili la daraja la Mbutu sincerely sitomkubali. jana katika kumnadi Dr.kafumuka Dr. Pombe alisema katika budget ya 2011/2012 wizara yake imepanga budget ya kulijenga daraja hilo na ameenda Igunga ili awe km mwarobaini wa matatizo yanayotokana na daraja hilo.

Ukitafakari kw umakini utaona huu ni usanii mkubwa, ukizingatia kuwa matatizo yatokanayo na daraja hilo hajaanza leo ni ya miaka nenda rudi. Leo kwa sababu kuna uchaguzi mdogo ndo wameliona hilo na wanakuja na propaganda eti sasa dawa yake inapatikana. kwa taarifa nilizonazo daraja hili liko chini ya Council ambamo mbunge ni mjumbe ktk vikao vihusuvyo maendeleo ya wilaya.

Kwa miaka takiribani 18 RA alikuwa mbunge na ni mjumbe wa council, je, walishindwa kutenga mafungu ya kulijenga daraja hilo? Ama kwa ukwasi aliotuibia huyu jamaa alishindwa kweli kutenga vijisent km 1b kuwakwamua wananchi wake kutokana na matatizo yanayowasibu? Huu jamani ni ujanja wa kuwarubuni watu.

Ndg wanajamvi naomba kuwasilisha.
 
Wajinga ndio waliwao. Kwanini amesubiri hadi kipindi cha kampeni?
Sheria za uchaguzi zinaruhusu serikali kushiriki ktk uchaguzi?
HIYO NI RUSHWA!!!
 
Wajinga ndio waliwao. Kwanini amesubiri hadi kipindi cha kampeni?
Sheria za uchaguzi zinaruhusu serikali kushiriki ktk uchaguzi?
HIYO NI RUSHWA!!!

Yes hii ni rushwa live lakini kwa kuwa imefanywa na mtu wa ccm its ok hakuna tatizo. After all hiyo budget iliyotengwa kujenga daraja si ya ccm so whether mgombea wa ccm kachaguliwa ama la daraja linapaswa kujengwa kwani linajengwa kwa kodi za wananchi kutoka vyama vyote na wasio na vyama pia.
 
ccm wanahaha - maji shingoni. hizi ni dalili za chama kugawanyika na kufa - leo hii magufuli amekuwa lulu - Sita na group lake hawana nafasi igunga. Dhana ya ufisadi na kujivua magamba haina nafasi kampeni za igunga - duh kweli akili mu kichwa.
 
Ukisoma sheria ya gharama za uchaguzi zinakataza afisa wa serikali kutumia miradi iliyopangwa kama mtaji/sera zake ilibidi tume au msajili wamuondoe mgombea wa magamba kwa kuvunja sheria hii.
 
Chadema wanakusanya ushahidi ushindi huu utapingwa mahakamani na Lissu au Marando ataunguruma
 
Wajinga kweli ndo waliwao! Yaan jamaa wameishiwa sera hadi wanatumia njia ya kusingizia mipango ya bajet kuwaokoa. RA alikuwepo kwa miaka 18 hawakuliona tatizo hadi aende dakika za mwisho kutoa rushwa ya daraja. F@#k Eng. Dr. Magufuli japo ninakuheshimu kwa utendaji wako uliotukuka ila sio hata pale unapokumbatia visivyokumbatiwa
 
kama Magufuli aliwahi kuhonga nyumba ya serikali kwa malaya atashindwaje kuongea ufala huo mbele za umma.....
 
Binafsi Dr.Pombe huwa namkubali ktk utendaji wake. lakini kwa hili la daraja la Mbutu sincerely sitomkubali. jana katika kumnadi Dr.kafumuka Dr. Pombe alisema katika budget ya 2011/2012 wizara yake imepanga budget ya kulijenga daraja hilo na ameenda Igunga ili awe km mwarobaini wa matatizo yanayotokana na daraja hilo. Ukitafakari kw umakini utaona huu ni usanii mkubwa, ukizingatia kuwa matatizo yatokanayo na daraja hilo hajaanza leo ni ya miaka nenda rudi. Leo kwa sababu kuna uchaguzi mdogo ndo wameliona hilo na wanakuja na propaganda eti sasa dawa yake inapatikana. kwa taarifa nilizonazo daraja hili liko chini ya Council ambamo mbunge ni mjumbe ktk vikao vihusuvyo maendeleo ya wilaya. kwa miaka takiribani 18 RA alikuwa mbunge na ni mjumbe wa council, je, walishindwa kutenga mafungu ya kulijenga daraja hilo? Ama kwa ukwasi aliotuibia huyu jamaa alishindwa kweli kutenga vijisent km 1b kuwakwamua wananchi wake kutokana na matatizo yanayowasibu? Huu jamani ni ujanja wa kuwarubuni watu.

Ndg wanajamvi naomba kuwasilisha.

Wajinga ndio waliwao. Hilo daraja limekuwa ni mtego wa kura kwa CCM. Hata Rostam Aziz alitumia hilo hilo daraja kutega kura mwaka jana.
 
Wajinga ndio waliwao. Hilo daraja limekuwa ni mtego wa kura kwa CCM. Hata Rostam Aziz alitumia hilo hilo daraja kutega kura mwaka jana.
Katika watu ambao kidogo nilikuwa nawakubali ni Magufuli ila kwa jana
 
Ninaombea sana Mbunge wangu afe. Maana najua huku kwetu kutakuwa Ulaya ndogo kwa jinsi Serikali itakavyokujali katika kipindi chote cha kampeni mpaka uchaguzi. Kwa sasa Serikali ya CCM inatuona kwamba tuna allergy na madaraja ndio maana wametuacha tukiliwa na mamba tukivuka mito kipindi cha Masika, kipindi hicho watakuwa wamefumbuliwa macho na kuona kuwa wasipotuletea madaraja ya zege Mungu atawalaani, kwa sasa serikali ya CCM wanajifanya eti wanatuona tuna allergy ya barabara za lami kipindi hicho wataona kwamba hatutaweza kuishi bila lami, kwa sasa serikali ya CCM inatuona kwamba sisi ni watu wa daraja la tatu, kipindi hicho tutaitwa waheshimiwa. Kwa sasa Serikali inatuona labda tukishika hela tutaota ukoma, kipindi hicho watakuwa wamebaini kwamba ni dhambi kubwa mtu wa huku kuishi bila kumiliki hela.
 
Wajinga ndio waliwao. Hilo daraja limekuwa ni mtego wa kura kwa CCM. Hata Rostam Aziz alitumia hilo hilo daraja kutega kura mwaka jana.
Katika watu ambao kidogo nilikuwa nawakubali ni Magufuli ila kwa jana igunga kuna asilimia zimeshuka kumwamini amejidhalilisha
 
Wajinga ndio waliwao. Hilo daraja limekuwa ni mtego wa kura kwa CCM. Hata Rostam Aziz alitumia hilo hilo daraja kutega kura mwaka jana.

Jana nimepita kwa taabu sana, hakuna kilichofanyika zaidi ya hayo mafungu mawili ya mawe ya kutoka Mwanzugi, kweli CCM ni Kimeta




 

Attachments

  • Photo0027.jpg
    Photo0027.jpg
    150.2 KB · Views: 51
  • Photo0029.jpg
    Photo0029.jpg
    204.3 KB · Views: 46
  • Photo0013.jpg
    Photo0013.jpg
    144.4 KB · Views: 39
Back
Top Bottom