Pombe imesambaratisha familia, nahitaji ushauri

hadithi nzuri! Shigongo anaweza kuajiri.
 
Mimi ni kijana nina miaka 33 ni baba wa familia ya watoto watatu ila ni familia iliyo sambaratika mwaka mmoja uliopita, nilioa mke wangu mwaka 2005 katika kuanza tulianza maisha ya hali duni nikisema hali duni kwa mtanzania inaeleweka.

Maisha yakawa yanabadilika nakuwa maisha mazuri kulingana na juhudi zetu japo mke wangu alikuwa mama wa nyumbani baada ya muda miaka kama mitatu mpaka mitano nikawa nimetengeneza maisha mazuri ya kuweza kukidhi mahitji ya familia yangu na kula kile tunacho kitaka. Basi huku maisha yakiendelea vizuri mimi baba wa familia nikawa na marafiki wengi kulingana na kazi yangu.

Nilikuwa napenda kunywa pombe weekend sasa hali ikawa tofauti marafiki wakawa ni kunipitia kila siku tukanywe. Muda ulivyozidi kwenda bia zikawa hazinileweshi, nikahamia kunywa konyagi za chupa (bapa). Hizo nazo nikawa sipati ulevi wa kutosha nikaingia kwenye Viroba.

Sasa hapo ndipo mambo yakawa mwendo mdundo. Kila nikirudi nyumbani ni vurugu kati ya mimi na mke wangu akinisihi niache pombe mimi kiukweli nilikuwa na mamuahidi naacha kesho. Ila pakikucha tu laizma nikazimue na kuendelea. Ugomvi ukazidi na kipato nacho kikaanza kupungua.

Tumegombana sana nikawa nikija nimelewa ni vurugu sasa kwa kuwa niko chakari najikuta nazidiwa nguvu na mke hivyo mara nyingine napokea kipigo cha ukweli mpaka kesho yake kazini hakuendeki. Naumwa mwili mzima kwa kipigo cha wife alichonipa. Lakini mke wangu akawa ananiambia amechoka na ulevi wangu hivyo atanikimbia na kuniacha siku ikifika.

Basi mwaka jana mwezi wa nane nilirudi nyumbani nikiwa sijalewa sana tukakosana kidogo tu ikatokea ugomvi mkubwa sana mpaka mke wangu akakimbilia jikoni kuchukua kisu aje anichome nife. Kweli akaja na kisu katika purukushani za kujihami ili asiniue nikawa nimepata kile kisu na kumshida nguvu. Lakini kisu kikanikata kiganjani na kuumia sana nikafanikiwa kutoka ndani na kukimbilia nje. Baada ya kutoka nje nikakimbia mpaka police na kupewa barua ya kwenda hospitali kwa matibabu. Nikaenda hospitali na nikawa nimeshonwa nyuzi 9.

Ukweli niliumia sana usiku huo sikurudi nyumbani kwangu nililala dukan kwngu huko mjin. Asubuhi nikapanga safari ya kurudi kijijin kwa wazazi wangu, nilipofika nyumbani wazazi wakanipokea nikahudumiwa mpaka nikapona. Baada ya kupona wazazi wangu wakanikataza kurudi tena kule. Basi nikaondoka nyumban nikaenda mkoa mwingine kuanza maisha upya. Mke wangu na yeye akawa amerudi kwao na watoto. Baada ya muda wazazi wangu wakaenda kwao na mke wangu kujua nini hatima ya ndoa yetu.

Kikao kikafanyika mke wangu akawambia wazazi wangu kuwa hawezi tena kurudia matapishi yaani kurudiana na mimi. Basi wazazi wakanifkishia ujumbe huo kuwa mkeo hatarudiana na wewe tena. Nioe mke mwingine na mimi ikaniuma sana nikampigia simu nikamwambia kuwa nimeacha pombe na nahitaji kuishi pamoja na familia yangu. Akagoma kabisa huku matusi mabaya akinitukana. Nikawa sina la kusema tena maana pia nikiangalia maisha niliyo nayo ni ya shida sana. Sasa imepita mwaka mmoja na miezi miwili nimepambana na maisha mpaka yamekaa vizuri. Nina miezi miwili nawasiliana na mke wangu namtumia picha mbali mbali kwa njia ya whatsap jinsi nilivyo badilika nimekuwa mwanaume bora kabisa.

Nimembembeleza aje huku nilipo ili tuishi wote tena na watoto nimeshawatafutia international school. Mke wangu amekubali kuja kuishi na mimi tena. Upande wa pili wazazi wangu nimewaambia kuwa mke wangu amekubali kurudiana na mimi tena wamekuwa wamegoma wamekuwa wakali kama mbogo. Kauli ya mama yangu hatutaki urudiane na huyo muuaji. Alikukataa kipindi cha shida ameona umefanikiwa ndio arudi, sitaki kumsikia huyo mwanamke na ukilaaimisha kurudiana naye ujue mimi sio mama yako niliye kuzaa. Sasa nimeshindwa nichukue uamuzi upi. Mke sijamwambia juu ya kauli ya wazazi wangu na ndugu wengine nao hawamtaki kabisa na mimi mke wangu nampenda na nilisha msamehe nahitaji kulea watoto wangu na kuwapatia elimu bora. Nisaidieni nna mawazo sana

NB: Pombe nilishaacha toka siku ya kuchomwa na kisu. Wana JF naombeni ushauri wenu.. By Ntule

Kaka usithubutu kurudiana na huyo mwanamke.Kitakukuta kikubwa zaidi ya hicho.
 
Pamoja na kutounga mkono kitendo chake alichokifanya cha kuchukua kisu na labda kutaka kukuchoma nacho kukujeruhi au hata kukuua, wewe ndiye uliyekua chanzo cha matatizo ndani ya ndoa yenu. Waambie wazazi wako kwamba usingependa kuona watoto wenu wanalelewa bila ya kuwa na baba yao na mama yao pamoja ili kuwapa malezi na upendo wanaostahili kutoka kwenu. Waambie wazazi wako kwamba mmesamaheana kwa makosa yenu na bado mnapendana sana na hivyo kutaka kuendelea kuishi pamoja kama mke na mume. Wazazi kama wataweka ngumu basi akili mkichwa na kipaumbele kiwe kwa watoto wenu na familia yenu. Kila la heri na hongera kwa kuacha ulevi. Tujulishe kitakachojiri katika jitihada zako za kuirudisha familia yako iwe pamoja.

ok nitawajulisha kwa maana ushauri wenu ni nguzo mpya ya kujenga familia yangu upya endapo tutaungana tena
 
Umefanya kosa kushirikisha wazazi ugomvi wenu! Sasa utakoma!
 
Wazazi wako nao hawafikirii....Wanataka tuu kuletea watoto matatizo ya kuja kulelewa na mama mwingine...Kuchanganya wake ni mbaya sana..unakaribisha uovu nyumbani kwako kwani huyo mke mpya aweza asiwe mzuri kwa watoto wako ndipo itakuwa chanzo cha ugomvi...We ishi na mkeo aliyekuzalia watoto wako...Mungu atawabariki

Mimi ni kijana nina miaka 33 ni baba wa familia ya watoto watatu ila ni familia iliyo sambaratika mwaka mmoja uliopita, nilioa mke wangu mwaka 2005 katika kuanza tulianza maisha ya hali duni nikisema hali duni kwa mtanzania inaeleweka.

Maisha yakawa yanabadilika nakuwa maisha mazuri kulingana na juhudi zetu japo mke wangu alikuwa mama wa nyumbani baada ya muda miaka kama mitatu mpaka mitano nikawa nimetengeneza maisha mazuri ya kuweza kukidhi mahitji ya familia yangu na kula kile tunacho kitaka. Basi huku maisha yakiendelea vizuri mimi baba wa familia nikawa na marafiki wengi kulingana na kazi yangu.

Nilikuwa napenda kunywa pombe weekend sasa hali ikawa tofauti marafiki wakawa ni kunipitia kila siku tukanywe. Muda ulivyozidi kwenda bia zikawa hazinileweshi, nikahamia kunywa konyagi za chupa (bapa). Hizo nazo nikawa sipati ulevi wa kutosha nikaingia kwenye Viroba.

Sasa hapo ndipo mambo yakawa mwendo mdundo. Kila nikirudi nyumbani ni vurugu kati ya mimi na mke wangu akinisihi niache pombe mimi kiukweli nilikuwa na mamuahidi naacha kesho. Ila pakikucha tu laizma nikazimue na kuendelea. Ugomvi ukazidi na kipato nacho kikaanza kupungua.

Tumegombana sana nikawa nikija nimelewa ni vurugu sasa kwa kuwa niko chakari najikuta nazidiwa nguvu na mke hivyo mara nyingine napokea kipigo cha ukweli mpaka kesho yake kazini hakuendeki. Naumwa mwili mzima kwa kipigo cha wife alichonipa. Lakini mke wangu akawa ananiambia amechoka na ulevi wangu hivyo atanikimbia na kuniacha siku ikifika.

Basi mwaka jana mwezi wa nane nilirudi nyumbani nikiwa sijalewa sana tukakosana kidogo tu ikatokea ugomvi mkubwa sana mpaka mke wangu akakimbilia jikoni kuchukua kisu aje anichome nife. Kweli akaja na kisu katika purukushani za kujihami ili asiniue nikawa nimepata kile kisu na kumshida nguvu. Lakini kisu kikanikata kiganjani na kuumia sana nikafanikiwa kutoka ndani na kukimbilia nje. Baada ya kutoka nje nikakimbia mpaka police na kupewa barua ya kwenda hospitali kwa matibabu. Nikaenda hospitali na nikawa nimeshonwa nyuzi 9.

Ukweli niliumia sana usiku huo sikurudi nyumbani kwangu nililala dukan kwngu huko mjin. Asubuhi nikapanga safari ya kurudi kijijin kwa wazazi wangu, nilipofika nyumbani wazazi wakanipokea nikahudumiwa mpaka nikapona. Baada ya kupona wazazi wangu wakanikataza kurudi tena kule. Basi nikaondoka nyumban nikaenda mkoa mwingine kuanza maisha upya. Mke wangu na yeye akawa amerudi kwao na watoto. Baada ya muda wazazi wangu wakaenda kwao na mke wangu kujua nini hatima ya ndoa yetu.

Kikao kikafanyika mke wangu akawambia wazazi wangu kuwa hawezi tena kurudia matapishi yaani kurudiana na mimi. Basi wazazi wakanifkishia ujumbe huo kuwa mkeo hatarudiana na wewe tena. Nioe mke mwingine na mimi ikaniuma sana nikampigia simu nikamwambia kuwa nimeacha pombe na nahitaji kuishi pamoja na familia yangu. Akagoma kabisa huku matusi mabaya akinitukana. Nikawa sina la kusema tena maana pia nikiangalia maisha niliyo nayo ni ya shida sana. Sasa imepita mwaka mmoja na miezi miwili nimepambana na maisha mpaka yamekaa vizuri. Nina miezi miwili nawasiliana na mke wangu namtumia picha mbali mbali kwa njia ya whatsap jinsi nilivyo badilika nimekuwa mwanaume bora kabisa.

Nimembembeleza aje huku nilipo ili tuishi wote tena na watoto nimeshawatafutia international school. Mke wangu amekubali kuja kuishi na mimi tena. Upande wa pili wazazi wangu nimewaambia kuwa mke wangu amekubali kurudiana na mimi tena wamekuwa wamegoma wamekuwa wakali kama mbogo. Kauli ya mama yangu hatutaki urudiane na huyo muuaji. Alikukataa kipindi cha shida ameona umefanikiwa ndio arudi, sitaki kumsikia huyo mwanamke na ukilaaimisha kurudiana naye ujue mimi sio mama yako niliye kuzaa. Sasa nimeshindwa nichukue uamuzi upi. Mke sijamwambia juu ya kauli ya wazazi wangu na ndugu wengine nao hawamtaki kabisa na mimi mke wangu nampenda na nilisha msamehe nahitaji kulea watoto wangu na kuwapatia elimu bora. Nisaidieni nna mawazo sana

NB: Pombe nilishaacha toka siku ya kuchomwa na kisu. Wana JF naombeni ushauri wenu.. By Ntule
 
Mimi ni kijana nina miaka 33 ni baba wa familia ya watoto watatu ila ni familia iliyo sambaratika mwaka mmoja uliopita, nilioa mke wangu mwaka 2005 katika kuanza tulianza maisha ya hali duni nikisema hali duni kwa mtanzania inaeleweka.

Maisha yakawa yanabadilika nakuwa maisha mazuri kulingana na juhudi zetu japo mke wangu alikuwa mama wa nyumbani baada ya muda miaka kama mitatu mpaka mitano nikawa nimetengeneza maisha mazuri ya kuweza kukidhi mahitji ya familia yangu na kula kile tunacho kitaka. Basi huku maisha yakiendelea vizuri mimi baba wa familia nikawa na marafiki wengi kulingana na kazi yangu.

Nilikuwa napenda kunywa pombe weekend sasa hali ikawa tofauti marafiki wakawa ni kunipitia kila siku tukanywe. Muda ulivyozidi kwenda bia zikawa hazinileweshi, nikahamia kunywa konyagi za chupa (bapa). Hizo nazo nikawa sipati ulevi wa kutosha nikaingia kwenye Viroba.

Sasa hapo ndipo mambo yakawa mwendo mdundo. Kila nikirudi nyumbani ni vurugu kati ya mimi na mke wangu akinisihi niache pombe mimi kiukweli nilikuwa na mamuahidi naacha kesho. Ila pakikucha tu laizma nikazimue na kuendelea. Ugomvi ukazidi na kipato nacho kikaanza kupungua.

Tumegombana sana nikawa nikija nimelewa ni vurugu sasa kwa kuwa niko chakari najikuta nazidiwa nguvu na mke hivyo mara nyingine napokea kipigo cha ukweli mpaka kesho yake kazini hakuendeki. Naumwa mwili mzima kwa kipigo cha wife alichonipa. Lakini mke wangu akawa ananiambia amechoka na ulevi wangu hivyo atanikimbia na kuniacha siku ikifika.

Basi mwaka jana mwezi wa nane nilirudi nyumbani nikiwa sijalewa sana tukakosana kidogo tu ikatokea ugomvi mkubwa sana mpaka mke wangu akakimbilia jikoni kuchukua kisu aje anichome nife. Kweli akaja na kisu katika purukushani za kujihami ili asiniue nikawa nimepata kile kisu na kumshida nguvu. Lakini kisu kikanikata kiganjani na kuumia sana nikafanikiwa kutoka ndani na kukimbilia nje. Baada ya kutoka nje nikakimbia mpaka police na kupewa barua ya kwenda hospitali kwa matibabu. Nikaenda hospitali na nikawa nimeshonwa nyuzi 9.

Ukweli niliumia sana usiku huo sikurudi nyumbani kwangu nililala dukan kwngu huko mjin. Asubuhi nikapanga safari ya kurudi kijijin kwa wazazi wangu, nilipofika nyumbani wazazi wakanipokea nikahudumiwa mpaka nikapona. Baada ya kupona wazazi wangu wakanikataza kurudi tena kule. Basi nikaondoka nyumban nikaenda mkoa mwingine kuanza maisha upya. Mke wangu na yeye akawa amerudi kwao na watoto. Baada ya muda wazazi wangu wakaenda kwao na mke wangu kujua nini hatima ya ndoa yetu.

Kikao kikafanyika mke wangu akawambia wazazi wangu kuwa hawezi tena kurudia matapishi yaani kurudiana na mimi. Basi wazazi wakanifkishia ujumbe huo kuwa mkeo hatarudiana na wewe tena. Nioe mke mwingine na mimi ikaniuma sana nikampigia simu nikamwambia kuwa nimeacha pombe na nahitaji kuishi pamoja na familia yangu. Akagoma kabisa huku matusi mabaya akinitukana. Nikawa sina la kusema tena maana pia nikiangalia maisha niliyo nayo ni ya shida sana. Sasa imepita mwaka mmoja na miezi miwili nimepambana na maisha mpaka yamekaa vizuri. Nina miezi miwili nawasiliana na mke wangu namtumia picha mbali mbali kwa njia ya whatsap jinsi nilivyo badilika nimekuwa mwanaume bora kabisa.

Nimembembeleza aje huku nilipo ili tuishi wote tena na watoto nimeshawatafutia international school. Mke wangu amekubali kuja kuishi na mimi tena. Upande wa pili wazazi wangu nimewaambia kuwa mke wangu amekubali kurudiana na mimi tena wamekuwa wamegoma wamekuwa wakali kama mbogo. Kauli ya mama yangu hatutaki urudiane na huyo muuaji. Alikukataa kipindi cha shida ameona umefanikiwa ndio arudi, sitaki kumsikia huyo mwanamke na ukilaaimisha kurudiana naye ujue mimi sio mama yako niliye kuzaa. Sasa nimeshindwa nichukue uamuzi upi. Mke sijamwambia juu ya kauli ya wazazi wangu na ndugu wengine nao hawamtaki kabisa na mimi mke wangu nampenda na nilisha msamehe nahitaji kulea watoto wangu na kuwapatia elimu bora. Nisaidieni nna mawazo sana

NB: Pombe nilishaacha toka siku ya kuchomwa na kisu. Wana JF naombeni ushauri wenu.. By Ntule

Wewe siyo mkweli pombe huwa haiachwi kiivyo,huo ni uongo.
 
Kila la heri Mkuu, pamoja na kuwa Wazazi ni Mungu wa dunia unachotaka kukifanya wewe na mkeo ni kitu kizuri cha kuhakikisha familia yenu inaendelea kuwa pamoja na kuyaweka yote yaliyotokea na kusababisha kusambaratika kwa familia yenu pembeni. Hivyo wewe na mkeo ndio wenye sauti ya mwisho katika hili. Wazazi walikuruhusu uoe mke mwngine lakini kwa mapenzi uliyokuwa nayo kwa mama watoto wako hukutaka kufanya hivyo.

ok nitawajulisha kwa maana ushauri wenu ni nguzo mpya ya kujenga familia yangu upya endapo tutaungana tena
 
Uzuri unajua ni nani hasa alikuwa mkosaji.
Rudiana na mkeo mkajenge familia..hao wengine wote ni third parties.

Mapenzi ni baina yako na mkeo.
 
Wewe na mkeo mmeishakuwa mwili mmoja.mmeunganishwa tayari na watoto.wazazi wana nafas yao kama wazazi kwa ushauri tu.mwamuzi wa mwisho ni wewe na mkeo.tunza familia yako.
 
Ushauri usilete huku watakukatisha tamaa broo chakufanya yule ni mkeo na mnafamilia tayari kwanza nikuulize umeoana kihalalali?kama ni kihalali nakuhakikishia mweleze mungu tuu wala usifikiri ukiita vikao vya familia itasaidia itia jina na yesu pekee yeye ndie ataweka kila kitu sawa
 
Unajua kuna kitu kimoja binadamu tunachokosea sana, inapotokea ugomvi kama huu basi wazazi wa upande mmoja utasimama imara kutetea na kufunika makosa ya mtoto wao hali kadhalika upande wa pili. Hili ni kosa kubwa sana endapo wasuluhishi hao watalenga kuirudisha familia katika misingi imara.
Wewe jamaa unajua nini ulifanya mpaka mkeo akapata hasira. Pengine nae kitendo cha kushika kisu kinamsuta mpaka muda huu. Hiyo ni hali ya kiwa provoked.
Waambie wazazi wako hali halisi. Wapi ulikosea na nani alikuwa mkosaji kwenye huo ugomvi. Naimani watakuelewa...

hahahahaaaa bora huyo kakushikia kisu, mie nanunuaga mabomu, ukileta mambo yako tu, nakulipua kwa suprise...
 
Vitabu vya dini vinasema mwanaume atamuacha baba na mama yake,na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.
Akili kichwani.. Wapi unapata furaha ya moyo?? Coz Joy of the heart is that all matters!!

Sio vitabu vya dini ni Biblia takatifu pekee ndio inayosema hivyo. Hata hivyo huu ni ushauri mzuri, kama mk.muamini
 
Fata moyo wako
unachokipenda na kukitaka,itisha kikao cha wanafamilia wakiwamo wazazi
wako uwaeleze sababu za ww kukatwa mkono kwa kisu na kwa nini uligombana
na mke wako kiasi cha kuachana,waambie ww ndio ulifanya makosa kwa
kuendekeza pombe na kumsumbua mkeo..hii itasaidia kumsafisha
mkeo..wasipoelewa basi mrudie na Mungu atakusimamia sababu ndoa yako ni
takatifu na moyo wako umemsamehe mkeo...utabarikiwa na ndugu wataelewa
tu siku moja.

Usiniwaze kama huwezi kujiwaza.

Ndugu, hakuna laana ndani ya msamaha na upendo. Arudiane na mkewe kwa faida yao (mke na mume) na watoto. Amen!
 
Inaonekana unampenda sana mke wako na ulishaamua utamrudia sema ulitaka kuhajkikihsiwa na mwawazo mbalimbali. Nami naona ni vema ukarudiana na mke wako lakini pamoja na kuwa wewe ulikuwa mkosaji zaidi lazima mke wako pia aelewe alikosea kabisa kukushikia kisu. Aidha aelewe pia kuna kusita kidogo kwa upande wafamiia yako na sababu ni hicho hicho kisu! Mapenzi na pande mbili ili mzani uwezeku-balance.
 
kisa chako kinaonyesha wewe ndo ulikuwa chanzo cha matatizo yote ulikuwa ukitoka kunywa pombe unaanzisha ugomvi ambao mke alichoka.kosa alilolifanya mkeo ni kutaka kukuchoma kisu inawezekana alipata hasira ghafura akashindwa kutafasiri madhara ya kuchukua kisu kwamba anaweza kuua.nakushauri kabisa mrudie mkeo mlee watoto wenu.kama kweli umeacha pombe ndoa yenu itakuwa ya amani kweli.
kuhusu wazazi wanasehemu katika maamuzi yetu lakini katika ndoa maamuzi ya mwisho ni ya wanandoa wenyewe,kama ninyi mmesameheana rudianeni msimsikilize mtu
 
Back
Top Bottom