Pombe imesambaratisha familia, nahitaji ushauri

Pombe imesambaratisha familia, nahitaji ushauri

Hafai achana nae. We lea watoto tuu, alikua anakutukana wakati wa shida, leo umefanikiwa, anakubali kurudi. Kesho ukiwa na shida atakukimbia tena. Mpotezee kabisa!

Soma tena na tena uzi wa mleta Uzi...kuwa walianza maisha duni sana na mpaka wakafanikiwa na jamaa akabadilika ...so usiwe unashauri kabla ya kuelewa mkuu.
 
Tafadhali sana bwana ntule rudiana na mkeo mlee familia yenu kwani tangu unatafuta maisha ulikuwa na huyo mkeo nampaka kufanikiwa ulikuwa naye huyo mkeo na chanzo cha kuachana na mkeo tatizo ulikuwa ni wewe mwenyewe,kwa hiyo mimi hapo sioni tatizo mkeo ni mkeo tu hakuondoka kwao kwa kutaka yeye ila kwa ajili ya pombe zako,unajua sometimes wanawake huwa wanachoka na tabia zetu sisi wanaume hebu jaribu kuwasihi wazazi wako tena na tena ili uweze kurudiana na mkeo
Mi nimeshuhudia juzi hapa ninapo ishi ndoa iliyovunjika kwa mda wa miaka kumi na minne mke na mume wamerudiana tena so nachokusihi piga magoti uombe kwa mungu leo kuhusu ilo swala lako na kisha wafuate wazazi tena uongee nao kwa Mungu akishindikani kitu kaka ntule
Kama kweli huyo mwanamke anakuja kwa heli au shali Mungu atakupa majibu mtegemee mungu wakati wote.
Ninayekuambia hivi nimeona mengi kupitia yeye onja uone fanya hivyo usiku wa leo zungumza naye hata kwa sekunde moja kisha wafuate wazazi wako usikie watakuambia nin kuwa na imani
 
Tuache ushauri mbaya msimshauri bwana ntule kuto mrudia mkeo tafadhali fuata ubavu wako huyo ni mkeo tu
 
mwanaume UNGURUME wewe , sio UNGURUMIWE,
wazazi wako hawapaswi kuwa na maamuzi yeyote juu yako, kwao unaomba ushauri tu ambao waweza kuukataa au kuukubali, vinginevyo hawana maamuzi yeyote juu ya maisha yako, unless bado wewe ni kula kulala kwao.
 
Sijui kama ulishafanya maamuzi, lakini mimi nina ushauri. Kwanza Hongera kwa kubadilika, ikiwa umebadilika kweli, sababu wengi wakienda njia hiyo huwa hawarudi, mgogoro uliokuwa nao ni sababu na pombe na hilo unalijua mara nyingi wazazi wetu huwa biased kwenye maamuzi ya ndoa za watoto wao na hii inatokana na upendo. Lakini kubadilike na kuishi na familia ni bora. Hasa baada ya kikao kitakachodhihirisha mkeo naye amebadilika.
 
Back
Top Bottom