Pombe imesambaratisha familia, nahitaji ushauri

Pombe imesambaratisha familia, nahitaji ushauri

ntule

Senior Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
104
Reaction score
29
Mimi ni kijana nina miaka 33 ni baba wa familia ya watoto watatu ila ni familia iliyo sambaratika mwaka mmoja uliopita, nilioa mke wangu mwaka 2005 katika kuanza tulianza maisha ya hali duni nikisema hali duni kwa mtanzania inaeleweka.

Maisha yakawa yanabadilika nakuwa maisha mazuri kulingana na juhudi zetu japo mke wangu alikuwa mama wa nyumbani baada ya muda miaka kama mitatu mpaka mitano nikawa nimetengeneza maisha mazuri ya kuweza kukidhi mahitji ya familia yangu na kula kile tunacho kitaka. Basi huku maisha yakiendelea vizuri mimi baba wa familia nikawa na marafiki wengi kulingana na kazi yangu.

Nilikuwa napenda kunywa pombe weekend sasa hali ikawa tofauti marafiki wakawa ni kunipitia kila siku tukanywe. Muda ulivyozidi kwenda bia zikawa hazinileweshi, nikahamia kunywa konyagi za chupa (bapa). Hizo nazo nikawa sipati ulevi wa kutosha nikaingia kwenye Viroba.

Sasa hapo ndipo mambo yakawa mwendo mdundo. Kila nikirudi nyumbani ni vurugu kati ya mimi na mke wangu akinisihi niache pombe mimi kiukweli nilikuwa na mamuahidi naacha kesho. Ila pakikucha tu laizma nikazimue na kuendelea. Ugomvi ukazidi na kipato nacho kikaanza kupungua.

Tumegombana sana nikawa nikija nimelewa ni vurugu sasa kwa kuwa niko chakari najikuta nazidiwa nguvu na mke hivyo mara nyingine napokea kipigo cha ukweli mpaka kesho yake kazini hakuendeki. Naumwa mwili mzima kwa kipigo cha wife alichonipa. Lakini mke wangu akawa ananiambia amechoka na ulevi wangu hivyo atanikimbia na kuniacha siku ikifika.

Basi mwaka jana mwezi wa nane nilirudi nyumbani nikiwa sijalewa sana tukakosana kidogo tu ikatokea ugomvi mkubwa sana mpaka mke wangu akakimbilia jikoni kuchukua kisu aje anichome nife. Kweli akaja na kisu katika purukushani za kujihami ili asiniue nikawa nimepata kile kisu na kumshida nguvu. Lakini kisu kikanikata kiganjani na kuumia sana nikafanikiwa kutoka ndani na kukimbilia nje. Baada ya kutoka nje nikakimbia mpaka police na kupewa barua ya kwenda hospitali kwa matibabu. Nikaenda hospitali na nikawa nimeshonwa nyuzi 9.

Ukweli niliumia sana usiku huo sikurudi nyumbani kwangu nililala dukan kwngu huko mjin. Asubuhi nikapanga safari ya kurudi kijijin kwa wazazi wangu, nilipofika nyumbani wazazi wakanipokea nikahudumiwa mpaka nikapona. Baada ya kupona wazazi wangu wakanikataza kurudi tena kule. Basi nikaondoka nyumban nikaenda mkoa mwingine kuanza maisha upya. Mke wangu na yeye akawa amerudi kwao na watoto. Baada ya muda wazazi wangu wakaenda kwao na mke wangu kujua nini hatima ya ndoa yetu.

Kikao kikafanyika mke wangu akawambia wazazi wangu kuwa hawezi tena kurudia matapishi yaani kurudiana na mimi. Basi wazazi wakanifkishia ujumbe huo kuwa mkeo hatarudiana na wewe tena. Nioe mke mwingine na mimi ikaniuma sana nikampigia simu nikamwambia kuwa nimeacha pombe na nahitaji kuishi pamoja na familia yangu. Akagoma kabisa huku matusi mabaya akinitukana. Nikawa sina la kusema tena maana pia nikiangalia maisha niliyo nayo ni ya shida sana. Sasa imepita mwaka mmoja na miezi miwili nimepambana na maisha mpaka yamekaa vizuri. Nina miezi miwili nawasiliana na mke wangu namtumia picha mbali mbali kwa njia ya whatsap jinsi nilivyo badilika nimekuwa mwanaume bora kabisa.

Nimembembeleza aje huku nilipo ili tuishi wote tena na watoto nimeshawatafutia international school. Mke wangu amekubali kuja kuishi na mimi tena. Upande wa pili wazazi wangu nimewaambia kuwa mke wangu amekubali kurudiana na mimi tena wamekuwa wamegoma wamekuwa wakali kama mbogo. Kauli ya mama yangu hatutaki urudiane na huyo muuaji. Alikukataa kipindi cha shida ameona umefanikiwa ndio arudi, sitaki kumsikia huyo mwanamke na ukilaaimisha kurudiana naye ujue mimi sio mama yako niliye kuzaa. Sasa nimeshindwa nichukue uamuzi upi. Mke sijamwambia juu ya kauli ya wazazi wangu na ndugu wengine nao hawamtaki kabisa na mimi mke wangu nampenda na nilisha msamehe nahitaji kulea watoto wangu na kuwapatia elimu bora. Nisaidieni nna mawazo sana

NB: Pombe nilishaacha toka siku ya kuchomwa na kisu. Wana JF naombeni ushauri wenu.. By Ntule
 
hii ndo ile asiesikia la mkuu......pole sana..ungekubali kuacha pombe byvthen....yasingekukuta haya.
 
asante kaka buti hujanisaidi mawazo
 
Fata moyo wako unachokipenda na kukitaka,itisha kikao cha wanafamilia wakiwamo wazazi wako uwaeleze sababu za ww kukatwa mkono kwa kisu na kwa nini uligombana na mke wako kiasi cha kuachana,waambie ww ndio ulifanya makosa kwa kuendekeza pombe na kumsumbua mkeo..hii itasaidia kumsafisha mkeo..wasipoelewa basi mrudie na Mungu atakusimamia sababu ndoa yako ni takatifu na moyo wako umemsamehe mkeo...utabarikiwa na ndugu wataelewa tu siku moja.

Usiniwaze kama huwezi kujiwaza.
 
Fata moyo wako unachokipenda na kukitaka,itisha kikao cha wanafamilia wakiwamo wazazi wako uwaeleze sababu za ww kukatwa mkono kwa kisu na kwa nini uligombana na mke wako kiasi cha kuachana,waambie ww ndio ulifanya makosa kwa kuendekeza pombe na kumsumbua mkeo..hii itasaidia kumsafisha mkeo..wasipoelewa basi mrudie na Mungu atakusimamia sababu ndoa yako ni takatifu na moyo wako umemsamehe mkeo...utabarikiwa na ndugu wataelewa tu siku moja.

Usiniwaze kama huwezi kujiwaza.

nilisha waeleza kuwa mm ndio chazo cha yote na mipombe yangu ndio sababu but sijaona kunielewa lawama ni kwa mke wangu tu kuwa hanifai .asnt broo
 
Hafai achana nae. We lea watoto tuu, alikua anakutukana wakati wa shida, leo umefanikiwa, anakubali kurudi. Kesho ukiwa na shida atakukimbia tena. Mpotezee kabisa!
 
Hafai achana nae. We lea watoto tuu, alikua anakutukana wakati wa shida, leo umefanikiwa, anakubali kurudi. Kesho ukiwa na shida atakukimbia tena. Mpotezee kabisa!

watoto anao yeye huko .mm nipo single now
 
wewe mrudie mkeo hiyo mambo ya mama kusema yeye siyo mama yako ni nambo ya kidunia ila kwa Mungu huyo ni mama yako we mrudishe mkeo ukae nae muda umshauri aende kwa wazee aombe radhi kwa yaliyotokea
 
Vitabu vya dini vinasema mwanaume atamuacha baba na mama yake,na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.
Akili kichwani.. Wapi unapata furaha ya moyo?? Coz Joy of the heart is that all matters!!
 
Pole sn, kwanza kabisa wewe ni pure an alcoholic na kitaalum kabisa ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) HAUNA TIBA (RESEARCH BY World Health Organization (W.H.O) SINCE 1949) pia lazima ufahamu kuwa ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) una hatua kuu tatu (YA AWALI, KATI NA YA MWISHO) kwa maelezo yako ww umefikia hatua ya mwisho yaani LATE STAGE ambayo hakuna jinsi yyt unaweza kunywa pombe na kubaki salama as a social drinker, njia pekee ya kukusaidia jaribu kutafuta kitu ALCOHOLICS ANOYMNOUS (A.A) MEETING katika eneo lako au waweza kuwasiliana nami kwa +255 789 78 05 29 kwa msaada zaidi.
 
Pole sn, kwanza kabisa wewe ni pure an alcoholic na kitaalum kabisa ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) HAUNA TIBA (RESEARCH BY World Health Organization (W.H.O) SINCE 1949) pia lazima ufahamu kuwa ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) una hatua kuu tatu (YA AWALI, KATI NA YA MWISHO) kwa maelezo yako ww umefikia hatua ya mwisho yaani LATE STAGE ambayo hakuna jinsi yyt unaweza kunywa pombe na kubaki salama as a social drinker, njia pekee ya kukusaidia jaribu kutafuta kitu ALCOHOLICS ANOYMNOUS (A.A) MEETING katika eneo lako au waweza kuwasiliana nami kwa +255 789 78 05 29 kwa msaada zaidi.
 
Hapa mkeo hakua na kosa kuondoka kwako!
Kosa lake 1 kubwa lilikua ni kukushikia kisu .
Ni kosa kubwa, hata hivyo linastahili kusamehewa incase limeombewa msamaha wa kina na dhati .

Mkosaji nambarione ni wewe !
Kwani ndiye uliyekua creater wa msambaratiko wa nyumba through mipombe yako.
Bytheway makosa yako nayo pia yanasameheka pindipo umeyaombea radhi ya udhati na kina .

Kaa na familia yako uwape ushauri wa kina umuhimu wa kurejeana na mkeo, wao sio mawe ni binadamu wanaweza badili msimamo wakakupa baraka.
Aidha usichukue hatua ya kumrejea mkeo pasipo ridhaa ya mamio .
 
Ukome ila endelea kumsihi moyo ulimchafuka kabisa ujue wanawake mioyo yetu inachukua muda kuchafuka lakin SKU mwanamke akichukia hata kuua anaona sawa tu vumilia manake umeharibu mwenyewe na mamako anaona mwanamke wako muuwaji kivipi kwann usione wewe ndo muuwaji
Ulevi wako ungewexa kumpa maradhi ya ukimwi.
Presha
Msongo w mawazo na kuuwa sasa we kukatw kiganja anaona hatareee
 
Rudiana na Mkeo kwa Maelezo yako wewe mume ndiyo ulikuwa tatizo kwenye familia yako.

safi sana mkuu,tatizo wazazi wake wanapaangalia kwa hasira alipoangukia mtoto wao badala ya kukikabili kisiki kilichomwangusha. ulevi wake ndio chanzo cha matatizo,alichofanya mkewe ni matokeo ya ulevi wake....

Itisha kikao cha wazazi wa pande zote uwaeleze kuwa tatizo ulikuwa ni wewe na si mkeo,kitendo cha mkeo kukukata na kisu alikuwa akijihami dhidi ya fujo zako za ulevi. Nakutakia mafanikio mema
 
Kikubwa ni kuwasikiliza wazazi wako ,hata vitabu vya mungu vinasema hivyo ,endapo hawataridhiwa na wwe ujue shida itarydi tena kwa njia yeyote ile kka ,huyo mwanamke wazazi wako wanamjua ndomana wakatoa ushauri huo ,
 
Binafsi nakubaliana na wazazi wako,
Ila si juu ya kwamba mkeo baada ya kukuona uko well off ndio ataka rudi kwako.
Isipokuwa ni mkeo kuwa na fikra za kuua pindi anapokwazika,
Kimsingi kila binadamu hupatwa hasira pale anapoudhiwa na tunatofautiana the way we respond to such a situation, sasa kama yeye kukuua ndio anaona ni best response, hiyo hatari.
Huenda next time mkaja kukwaruzana kwa sababu zingine mbali na ulevi akakuua.
 
Back
Top Bottom