Polisi, Zimamoto, Magereza, Uhamiaji na Waziri mmeshindwaji kupandisha Askari vyeo Kama Rais alivyoagiza?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kupitia ukurasa wa Instagram Malisa ameeleza mianya iliyopo kwenye jeshi la Polisi kuhusu vyeo. Amefafanua namna ambavyo kukosekana kwa baadhi ya vyeo ndani ya jeshi Hilo kunashusha heshima ya jeshi nakupelekea ugumu katika kuongoza.

Baada ya kusoma makala ile nilijaribu kufanya utafiti Kwanza kujua vyeo vya polisi vinapanda kwa utaratibu gani na kwa sheria ipi. Hivyo nilijaribu kuwatafuta wanaofanya kazi kwenye vyombo hivi kuona ni kweli tatizo lipo na kama lipo limesababishwa na Nini? Matokeo ya uchambuzi wangu kwenye hoja hii hayatapishana sana na hoja ya malisa ila yatapanua wigo kidogo.

1. Sheria na utaratibu wa upandaji vyeo
Sheria inayosimamia upandaji vyeo kwa jeshi la Polisi imeweka masharti ya upandaji vyeo yanayofanana kwa vyombo vilivyomo wizara ya mambo ya mambo ya ndani ambavyo ni Pilisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto.

2. Kwa mujibu wa sheria hiyo vyeo vinafanana kwa majeshi haya yote na upandaji wake upo Kama ifuatavyo;

Constabo hadi S/Sajini ni vyeo vinavyopandishwa na mkuu wa chombo husika ambaye ni IGP, CGP,CGI,CGF

Mkaguzi msaidizi au nyota moja hadi Kamishna msaidizi upandishwa na Kamisheni ambayo wajumbe wake ni wakuu wa vyombo na Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ni Mwenyekiti.

Kamishna Mwandamizi hadi Hadi mkuu wa Chombo (IGP, CGP....) Wanapandishwa na Mhe. Rais.

Kwa kundi la Kwanza na la pili wameweka kigezo kikuu kuwa Ni kukaa na cheo kimoja kwa muda wa miaka mitatu lakini kwa kundi linalosubiri uteuzi wa Mhe. Rais mamlaka hii haifungwi na kigezo Cha miaka kwenye vyeo.

2. Hali ilivyo kwa Sasa
Baada ya Mhe. Rais kutoa maelekezo ya watu kupanda vyeo ni Kama katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani pamoja na wakuu wa vyombo walishtukizwa. Walikuwa hawana data za Nani anapanda na Nani apandi na hivyo kupelekea mkwamo kwenye kutekeleza amri hii ya amri jeshi mkuu.

Changamoto ya Kwanza kubwa iliyotokea ni wakuu wa vyombo kutosoma na kuelewa vyema Organization structure zao, hii imepelekea hadi sasa ndani ya jeshi la Polisi ,Zimamoto,Magereza na Uhamiaji kuwepo kwa nafasi nyingi sana za vyeo vya Mrakibu, Mrakibu Mwandamizi Kamishna Msaidizi ambazo zipo wazi au zinakaliwa na watu wenye vyeo vya chini.

Vyeo hivi vyote vipo mikononi mwa wakuu wa vyombo na Katibu mkuu wa Wizara lakini pamoja na kukaa kwenye vikao ,pamoja na kuwa na Watendaji wenye sifa za kieleimu wakupandishwa kuziba nafasi hizi vyombo hivi vimeshindwa kujisimamia kwa miaka Sasa na kupelekea hoja ya malisa ya kukosekana kwa baadhi ya watendaji kwenye vyeo flani kutokea. Lakini changamoto hii pia inaelezwa kuwa imesababishwa na kuwepo kwa maafisa rasilimali watu wasiotimiza wajibu wao ndani ya Wizara na ndani ya vyombo.

Hivyo kwa mantiki hii ni kweli pamoja na Waziri kutangaza Askari wengi kupandishwa vyeo lakini mianya haikuzibwa, organization structure haikufuatwa na hata Sasa bado yapo malalamiko ya watu kutopandishwa vyeo.

Lakini pia ipo changamoto ya pili ambayo ni wizara na ofisi ya katibu mkuu kiongozi, taarifa zinadai upo mkanganyiko wa kanuni na sheria katika hoja ya malisa ambapo vigezo vinakinzana na hata mapendekezo yanayopelkwa kwa muda mrefu hayafanyiwi kazi Kama inavyotakiwa.

Hivyo kwa mujibu wa malisa na kwa mujibu wa watendaji lipo tatizo la Askari kutopandishwa vyeo. Chakushangaza zipo pia taarifa ambazo zinadai idadi aliyotaja Mhe. Waziri siyo idadi iliyopandishwa vyeo Bali baadhi ya vyombo Wana idadi pungufu na hivyo walimdanganya Waziri kuwa wamepandisha watu wengi lakini waliopandishwa Ni wachache,. Hii unatokana na kuwa na nidhamu ya woga kwenye vyombo.

Kuhusu wateule wa Mhe. Rais yaani Kamishna Mwandamizi hadi makamishna napo kunaelezwa Kuna nafasi nyingi zipo wazi Kama alivyoelekeza Malisa. Lakini Kama ilivyo kwa makundi mengine, Katibu mkuu baada ya kushauriana na wakuu wa vyombo ndiye upeleka mapendekezo yakuziba maianya pale maafisa wanapostaafu au kufariki au kupangiwa majukumu mengine. Si jukumu la Rais kwenda kuangalia mapungufu ya vyeo Magereza wala Fire.

Ni jukumu la wakuu wa vyombo hivyo malalamiko yanaelekezwa kwa wakuu wa vyombo kwamba wanaamini wakipata seneor officers Kama muundo unavyotaka na kuwaweka kwenye nafasi zao wataonekana na kutishia nafasi zao. Hi inaelezwa ipo sana, unamkuta afisa mdogo yupo makao makuu na maafisa wakubwa kivyeo wapo mikoani si kwa bahati mbaya Bali nimakusudi. Hivyo naamini endapo wakuu wa vyombo watataka kuzibwa kwa nafasi hizi Basi watapendekeza kwa mamlaka husika lakini wakiendelea na mgomo baridi siku zote changamoto ya vyeo Jeshini haitokoma.

Mwisho niwaombe maaskari kujifunza kujitetea mbele ya wanna siasa, kuacha uungu mtu pale wanapopanda wao wakaona walio chini yao hawaruhusiwi kupanda na mwisho wapendane. Ni vigumu kutafita na kusimamia haki ya jamii Kama wewe tu mwenyewe uwezi kudai na kusimamia haki yako
 
Unapanda cheo na mshahara unapanda.

Hao askari wapo wastaafu hawajalipwa stahiki zao.

Leo unamlaumu katibu wa wizara,anajua kibuyu hakiruhusu
 
Sawa hao wengine wote wapandishwe lakini kwa aina ya utendaji kazi wa zimamoto hapana aseeee
 
Back
Top Bottom