Polisi yazuia Operation Sangara ya CHADEMA Morogoro kisa hakuna Askari

hata alichokifinya jana kamanda wa polisi Morogoro bado ni wa kikoloni hakuna jipya hapo hata angekuwa na master ya sheria bado anatumikia polissm
 
mi nadhani police wanaakili za kutosha lakini mwajili wao yani bosi wao hakuna kitu upepo mtupu kwa kifupi ni abunuasi
 
jAMAA ALIKUWA HAYUKO SERIOUS IWEJE ASEMA KUWA HAKUNA POLISI WA KUTOSHA KULINDA MKUTANO ILA TUMEKUJA KUONA KUNA POLISI WA KUTOSHA KATIKA KUZUIA MAANDAMANO.nA KAMA HAKUTUMIA BUSARA MORO INGEJEUKA KUWA KAMA MBEYA AU ARUSHA,vIVA CHADEMA TUTAFIKA TU KWA JAMBO HILI WANANCHI PIA WAKO NYUMA YENU
 
Eti hakuna polisi wa kutosha kulinda mkutano. Wakat hao polisi waliomwagwa jana wapo zaidi ya mia. Hakuna kitu hapo walewale.
 
Chadema yakwama kufanya mkutano Send to a friend
Sunday, 05 August 2012 00:15


00000000001akinacha.jpg
MKUU wa Operasheni wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Singo Benson, akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho katika ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa maandamano na mkutano wa chama hicho uliokuwa ufanyike jana mjini Morogoro . Picha na Juma Mtanda

VIONGOZI, POLISI WAKUBALIANA UFANYIKE AGOSTI 8 KILOSA, FFU WAMWAGWA MITAANI KUDHIBITI WAFUASI
Venance George, Morogoro
BAADA ya mvutano wa siku mbili baina ya Jeshi la Polisi na Chadema kilichopanga kufanya mkutano mjini Morogoro jana, pande hizo mbili zilikubaliana kuwa mkutano wa kwanza ufanyike Agosti 8, mwaka huu Mikumi, wilayani Kilosa.Makubaliano haya yanakuja kufuatia mazungumzo baina ya viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro na wale wa Chadema kuwa, kwa vile maonyesho ya Nanenane mkutano huo usongezwe mbele na ufanyike wilayani Kilosa Agosti 8, mwaka huu.
Awali Jeshi la polisi lilizuia kwa madai kutokana na kuwapo mgomo wa walimu nchini ambao ulisitishwa kwa amri ya mahakama Alhamisi iliyopita pamoja na kwamba, jeshi hilo halitakuwa askari wa kutosha na kusimamia matukio hayo.
Hata hivyo, kabla ya kufikiwa makubaliano jana hayo askari wengi wakiwagwa mitaani kudhibiti wafuasi wa Chadema kuandamana na kufanya mkutano wa hadhara.
Wakiwa na mabomu ya kutoa machozi, magari yenye maji ya kuwasha, silaha za moto na virungu, vikosi hivyo vilikabiliana na baadhi wafuasi hao kwenye mitaa mbalimbali mjini hapa na kufanikiwa kuwatia nguvuni baadhi yao.
Hali hiyo ilitokana na wafuasi hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini hapa kwa ajili ya kuandaa maandamano hadi kwenye Viwanja ambavyo walitarajia kufanyia mkutano wa hadhara.
Wafuasi hao wa Chadema pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali walishiriki kwenye vuguvugu hilo ambalo chama kimelipa jina Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), licha polisi kutoa onyo kuwa wasithubutu kufanya maandamano na mikutano hiyo, kwa kile walichodai ni kutokuwa na askari wa kutosha wa kutoa ulinzi.
Jana asubuhi, Jeshi la polisi lilitawanya askari wake kwenye mitaa mbalimbali ya Mji wa Morogoro na barabara zote za kuingia na kutoka katika mji huo.
Magari yenye maji ya kuwasha pamoja na yale yaliyopakia askari wa FFU, yalionekana yaranda randa katika mitaa ya Mji wa Morogoro huku yakipeperusha bendera za rangi nyekundu kuashiria hali ya hatari.
Taarifa zilizopatikana mjini hapa zilidai kuwa vikosi hivyo vya askari zaidi ya 200 waliletwa hapa kutoka mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam na kuungana na wenzao wa Morogoro.
Hata hivyo, hali hiyo haikuwaogofya wafuasi na wapenzi wa Chadema, kwani walionekana wakiendelea na maandalizi ya kujikusanya huku wengi wao wakiwa wamevaa sare na kubeba bendera za chama hicho.

Wafuasi hao walionekana wakiwa katika makundi kwa makundi wakielekea kwenye ofisi za wilaya za Chadema zilizoko Mtaa wa Kingo.
Hali hiyo iliwafanya baadhi ya polisi waliokuwa katika mitaa mbalimbali kuanza kuwakamata baadhi yao hususan pale walipoonekana kuwa katika makundi makubwa.
Kitendo hicho kiliibua jazba na kuwafanya baadhi ya wafuasi kutoa maneno makali ya kulilaani jeshi hilo.
Hali hiyo ilionekana kuwatia zaidi hamasa wafuasi hao ambao waliendelea kujikusanya kwa kwenye ofisi za chama huku wakihimiza kuwa waandamane na ikiwezekana wakabiliane na yeyote atakayewazuia.
Kutokana na sakata hilo, polisi liliomba kukutana na viongozi wa Chadema wa mkoa na taifa ili kujadiliana nao.
Akizungumza na wafuasi na wanachama walifulika katika ofisi hizo baada ya majadiliano na polisi, Mkuu wa Operesheni za Chadema, Singo Benson Kigaila alisema kuwa, Jeshi la Polisi limewaomba kukubali kubadilisha ratiba na kupanga nyingine kadri chama hicho kitakavyopendekeza.
Aliongeza makubaliano yatakwenda sambamba kuwachia huru bila masharti wafuasi zaidi ya 10 walikuwa wamekamatwa pamoja na magari ya chama hicho.
Alisema Jeshi la polisi limeomba maandamano na mkutano huo uliopangwa kufanyika jana usitishwe kupisha shughuli za maonyesho ya wakulima ya Nane Nane, Kanda ya Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, mkoani hapa.

Alisema kuwa, kufuatia makubaliano hao waruhusiwa kufanya uzinduzi M4C kuanzia Jimbo la Mikumi, wilayani Kilosa Agosti 8 mwaka huu na kuendelea katika majimbo mengine tisa yaliyosalia.
Hata hivyo, Chadema imepanga kufanya mkutano mkubwa katika Jimbo la Morogoro mjini ambao utawahusisha viongozi wa kitaifa na wabunge Agosti 18, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Chadema, maandamano hayo yatapambwa na watembea kwa miguu waliobeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Yalielezewa kuwa yatasindikizwa na misafara ya baiskeli, pikipiki, magari na helikopta ya chama hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustin Shilogile alithibitisha kufikiwa kwa makubaliano hayo na kwamba, jeshi hilo litandelea kuimarisha ulinzi popote mikutano hiyo itakapofanyika.


 
Tuesday, 24 July 2012 21:03

Aidan Mhando
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni humo.

Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang'ula, Msolwa na Mkamba.

"Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama 214 kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14," alisema Kisenime.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi.

"Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge," alisema Katanduki.
 
Kanda ya kati m4c lini?ratiba ilionyesha ni leo,ila sioni dalili yeyote.msiwatenge wana makao jamani.
 
ndugu yangu hapa ni sehemu ya kutoa habari na kupata taarifa. Kwahyo acha umbumbu wako.

Wewe sio mbumbumbu tu ila ni imbecile huwa sipendi matusi and I never argue with stupid, silly people like you tafuta size yako uwatukane, kite wewe!!
 
Back
Top Bottom