Polisi yazuia Operation Sangara ya CHADEMA Morogoro kisa hakuna Askari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yazuia Operation Sangara ya CHADEMA Morogoro kisa hakuna Askari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Aug 3, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Polisi katika manispaa ya mji wa Morogoro wamezuia operation sangara ya CHADEMA kwa sababu za kuwa hakuna askari wa kutosha kusimamia mikutano yao katika mkoa wa Morogoro.

  Lakini pamoja na makatazo hayo CDM wamedai wao wataendelea na mikutano yao kama kawaida kwa sababu haisuani na fujo wala vurugu na siku zote Polisi huwa hawawasaidii kwa lolote.

  Concern

  Jeshi la PolisiCCM liko kwa ajili ya kuzuia CDM sio kulinda
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Polisi wakusimamia hawapo, lakini mkutano ukifanywa, polisi wakuwasambaratisha wapo. Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Sasa utaona kituko.. Polisi wa kuvunja mkutano huo wa kukaidi agizo la polisi kuwa hawatoshi watakuwa wengi mno!
   
 4. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Polisi watatangaza mikutano ni batili. Hawataisogelea, lakini wananchi wataogopa kwenda, mahudhurio yatakuwa pungufu. Azma yao itakuwa imetimia. Usalama wa Taifa unafanya kazi yake waliotumwa.
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Chadema hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya hizo operation mbuzi?
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama hawatoshi wakalale. Hawana umuhimu katika mikutano ya CDM. CDM hawana fujo, ila wanapochokozwa na Policts.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Si ndo hapo... Wakifanya mkutano utaona defender tatu zinaletwa zote zimejaa polisi hii nchi bana
   
 8. p

  pembe JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Cdm tunaomba bendera kwani ni alama tosha ya utambulisho wa uwepo wenu. Operesheni zikipita bila kucha alama wananchi tunawasahau kila tunapoona kijani kinapepea!
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135

  Acha uzushi...ni Operation Sangara sio mbuzi.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwani wewe ulichokusudia ni kutujuza agizo la polisi au ktoa concern yako?
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nadhani yuko sahihi kuuliza hinvyo, is too much. Wakumbuke kibaya Chajitembeza na kizuri chajiuza.
   
 12. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  All of the above..
   
 13. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama una uhakika povu la nini??
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CDM Mshughulikie Morogoro mpaka kieleweke, Hata vile viwanda vilivyobinafsishwa kwa wakubwa vinafugiwa mbuzi. huu mkoa unahitaji ukombozi wa jumla.
   
 15. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  that wy DHAIFU alisema chama cha msimu..kazi ya chama cha siasa ni kuzungumza na wanachama.ulitaka wakeshe baa?
   
 16. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  na zitawanyoosha hivyohivyo pamoja na umbuzi wake!
   
 17. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  hebu toa mapendekezo yako kwamba wafanye kazi gani tofauti na iyo, izo ni opereshen sangara tu, sangara akiwa mkubwa kama mbuzi wewe utazikwa ukiwa hai:A S-baby:
   
 18. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] MKUTANO WAO WAPIGWA MARUFUKU,WENYEWE WASEMA LAZIMA UFANYIKE
  Joseph Zablon
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeingia tena katika mzozo na Jeshi la Polisi nchini, baada ya mkutano wake uliopangwa kufanyika mjini Morogoro kuzuiwa kwa maelezo kwamba, hakuna askari wa kutosha wa kuuwekea ulinzi.

  Pamoja na zuio hilo, Chadema wanasema lazima mkutano huo ufanyike kwa maelezo kwamba sababu zilizotolewa na polisi siyo za msingi na zina ajenda ya kuhujumu kampeni yao waliyoiita ‘vua gamba, vaa gwanda'.

  Mvutano huo unatishia amani mji wa Morogoro na viunga vyake, ikiwa Chadema wataendelea na msimamo wao huo, hali polisi wakitumia nguvu kuzuia mkutano huo na mingine midogo katika kata 28 iliyoombwa isifanyike.

  Chadema kiliwahi kuingia katika mvutano na polisi katika baadhi ya matukio makubwa ambayo ni pamoja na katika miji ya Mwanza huku mapambano ya jijini Arusha yakisababisha mauaji.

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa wamepokea taarifa ya polisi ya kuwataka wasifanye mkutano huo, lakini wao kama chama hawatarudi nyuma.

  "Mkutano wetu upo palepale na utahudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa, wakiwamo wabunge wetu wote na utafunguliwa na Mwenyekiti wa wetu wa Taifa, Freeman Mbowe," alisema Kigaila.

  Kigaila alisema mikutano hiyo ni ya kukiimarisha chama na inaratibiwa na chama na sio polisi hivyo, kwa jeshi hilo walikuwa wanatoa taarifa na kuomba ulinzi na sio kulitaka liwapangie utekelezaji wake.

  "Mkutano ni makubaliano ya ndani ya chama na ajenda yetu ni kuwahamasisha Watanzania kujiunga na chama na ni sehemu ya operesheni Sangara," alisema Kigaila na kuongeza kuwa, maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika.

  Zuio la mkutano
  Kigaila alisema zuio la mkutano huo limetokana na barua yenye kumbukumbu Namba MRG/SO.7/2/A/219, ya Agosti Mosi mwaka huu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Morogoro kwenda kwa Katibu Chadema wilaya.

  Kigaila alisema baada ya kujitokeza hali hiyo aliwasiliana na kamanda wa polisi na walimuomba wafanyie mkutano wao eneo la Mvomero ombi ambalo pia lilikataliwa kwa madai kuwa haiwezekani kutokana na mgomo wa walimu.

  "Mara waseme kuna Nane nane, CCM nao wana mkutano Morogoro hivyo haiwezekani, tunapomwambia tukafanyie Mvomero anadai kuna mgomo wa walimu sasa hoja yake ipi hapa tunashindwa kumuelewa," alisema Kigaila.

  Alidai ni wazi jeshi hilo linatumika kwa manufaa ya kisiasa kwani yeye anavyofahamu ni kwamba ikiwa kuna vyama viwili vinavyotaka kufanya mikutano yake, basi hupangiwa maeneo tofauti.

  "Kama wengine wakipanga eneo fulani basi sheria inataka chama kingine kifanye mkutano wake mita 500 kutoka walipo wenzao," alisema.

  Kigaila alisema mkutano wao huo utafuatiwa na mingine katika kata 28 za mji huo kabla ya kuelekea katika miji ya Iringa, Dodoma, Manyara na Singida na awamu inayofuata itahusisha mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mwanza.

  Operesheni hiyo itaendelea katika miji ya Mara, Kagera na Geita kabla ya kurudi kumalizia mikoa iliyokuwa imesalia Kusini na ni operesheni ya kawaida ya kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho

  Taarifa ya polisi
  Kulingana na taarifa hiyo (ambayo Mwananchi limeona nakala yake), sehemu yake inasomeka: "Rejea barua yako ya Julai 30, 2012 ya kutoa taarifa na kuomba ulinzi kwa ajili ya maandamano na mikutano ya hadhara mliyokusudia kufanya K/Ndege Agosti 4, 2012 na Agosti 5 kwa Kata 28".

  "Katika tarehe zilizoainishwa hapo juu Chama cha Mapinduzi (CCM), wamekusudia kufanya mikutano ya hadhara ya wanachama, wapenzi na makada wao katika maeneo hayo hayo," inasema taarifa hiyo.

  Inaongeza kuwa Agosti mosi hadi 10 mwaka huu, maadhimisho ya sherehe za Nane Nane yanaendelea katika Mkoa huo na kama vile haitoshi, katika tarehe zilizoanishwa, mgomo wa walimu wa shule za msingi na sekondari unaendelea nchi nzima.

  Sehemu ya taarifa hiyo iliongeza kwamba, kutokana na sababu hizo shughuli zote zinahitaji ulinzi na usalama ambao utasimamiwa na polisi, hivyo kutokana na mgawanyo uliopo wa askari itakuwa vigumu kusimamia shughuli zote kwa wakati mmoja.

  "Kwa mantiki hiyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro amesitisha mikutano ya hadhara na maandamano hayo kwa mujibu wa kifungu namba 43 (1-6) cha sheria za Polisi na polisi wasaidizi sura 322 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002," inabainisha barua hiyo.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: modifydate"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 19. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimesoma habari kuwa polisi wamekataza mkutano wa CDM Morogoro kisa na sababu hawana polisa wa kutosha kulinda mkutano huo. Hadi hapa ninaelewa. Nisipoelewa ni pale polisi wanaposema watatumia nguvu kuzuia mkutano huo. Ina maana kama CDM watakusanyika polisi watawatawanya na kuwasambaratisha.

  Nisichokielewa - kama hawana polisi wa kutosha kulinda amani, hao wa kusambaratisha watawatoa wapi? Kipi kinahitaji nguvu zaidi baina ya kusimamia amani na kutuliza amani?

  Nielekezeni wenye kujua mambo hayo
   
 20. r

  rugo Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu zilizotolewa na jeshi la polisi kuzuia mkutano wa CHADEMA huko Morogoro, je zina mashiko? Sababu zenyewe ni kwamba; walivyotaka kufanyia Moro mjini wakaambiwa CCM pia wana mkutano, wakaomba kwenda kufanyia Mvomero, wakaambiwa haiwezekani kwa sababu kuna mgomo wa walimu. Sasa kama kuna mgomo wa walimu, ina maana mkutano wa CCM hautaathiriwa na mgomo wa walimu, au mgomo wa walimu upo Mvomero tu?

  Nawasilisha.
   
Loading...