Safi sana mkuu kwa kuliona hilo, Always Critical thinkers have similar way of seeing things.Kama kuna watu wana mambo ya kijinga hapa Tanzania basi CUF wanaongoza. Wamepanga haya maandamano yao siku hizo makusudi wakijua kuna ugeni. Sasa kama utajiuliza kwa nini, jibu ni kwamba, wamefanya hivyo ili mume wao atakaposema wasiandamane basi ionekane wana adabu tofauti na CDM ambao hugomeaga sababu za kike-kike kama hizo.
Kama kweli CUF nia yao ya kufanya maandamano ni ili wasikike, basi hawana haja ya kurudi nyuma, huu ndio wakati muafaka kwani hicho wanachotaka kudai ndio wakati wake. Wenzetu husubiri ujio wa wageni ndio waandamane, basi kama kweli wanayo madai huu ndio wakati na wala sio akishaondoka.
Eti CUF wanataka kuandamana kipindi ambacho Obama anakuja Dar tena maandamano yataelekea Ikulu!!! CUF hawana mpango wowote wa kuandamana na walijua fika Polisi hawataruhusu maandamano yao.
Malengo ya CUF ni hata:
1/To draw attention za watu ili CUF ionekane nayo ipo.
2/Ili kuonyesha wao ni watii kwa jeshi la Polisi, lengo lionekane wasiotii Polisi kwenye mambo ya maandamano ni wakorofi.