Polisi Yawaonya Wanaokula Hadharani mwezi wa Ramadhani

Status
Not open for further replies.

Pepombili

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
439
58
POLISI Mkoa wa Kusini Pemba, limewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kuvumiliana kidini na kuheshimu imani za wengine, kwa kuepuka kula hadharani katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii.

Jeshi hilo limesema limejipanga kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani kama vile uvaaji wa mavazi yasioendana na maadili ya kiislamu na kuhakikisha linakabiliana na uhalifu na wahalifu.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Saleh Mohammed Saleh, alitoa onyo hilo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizo ofisini kwake Madungu -Chake Chake Pemba.

"Tumejipanga vyema kufanya doria na oparesheni mbali mbali za kuwasaka wahalifu wote ili kuona wananchi wa mkoa wa Kusini wanatekeleza ibada yao kwa salama na amani," alisema.

Aliwatanabahisha wananchi wote kuwa macho wakati wa kufutari kwani muda kama huo ni mwanya kwa wahalifu kufanya makosa kwa kuvunja nyumba na kuiba kwa vile wanajua watu wako katika harakati za futari.

Alisema katika kipindi cha Ramadhani, wahalifu hutumia mwanya huo kufanya wizi wa mazao zikiwemo karafuu, ndizi, muhogo na nazi, hivyo ni lazima wawe waangalifu na kudumisha ulinzi shirikishi katika maeneo yao.

Aidha amewataka madereva kutii sheria za barabarani, hususani nyakati za kufutari kwa kuepuka kwenda mwendo wa kasi na kupakia abiria kupindukia uwezo wa gari.

Zanzinews
 
mh! na kwaresma pia huwa wanafanya hivyo hivyo? au wakristu hawana noma na walaji wakati wa kwaresma? au pemba hakuna wakristu?
 
"kuvumiliana kidini na kuheshimu imani za watu wengine" maana yake nini? Nitabaki na msimamo wangu kwamba Waislam wanatumia nguvu nyingi za kimwili kulazimisha dini yao na wanafunga kimwili na si kiroho. Kuna maeneo ya wakatoliki zaidi ya nusu na hawa hufunga Kwaresma, je amri hii nayo iwekwe?
 
POLISI Mkoa wa Kusini Pemba, limewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kuvumiliana kidini na kuheshimu imani za wengine, kwa kuepuka kula hadharani katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii.
Jeshi hilo limesema limejipanga kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani kama vile uvaaji wa mavazi yasioendana na maadili ya kiislamu na kuhakikisha linakabiliana na uhalifu na wahalifu.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Saleh Mohammed Saleh, alitoa onyo hilo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizo ofisini kwake Madungu -Chake Chake Pemba.
“Tumejipanga vyema kufanya doria na oparesheni mbali mbali za kuwasaka wahalifu wote ili kuona wananchi wa mkoa wa Kusini wanatekeleza ibada yao kwa salama na amani,” alisema.
Aliwatanabahisha wananchi wote kuwa macho wakati wa kufutari kwani muda kama huo ni mwanya kwa wahalifu kufanya makosa kwa kuvunja nyumba na kuiba kwa vile wanajua watu wako katika harakati za futari.
Alisema katika kipindi cha Ramadhani, wahalifu hutumia mwanya huo kufanya wizi wa mazao zikiwemo karafuu, ndizi, muhogo na nazi, hivyo ni lazima wawe waangalifu na kudumisha ulinzi shirikishi katika maeneo yao.
Aidha amewataka madereva kutii sheria za barabarani, hususani nyakati za kufutari kwa kuepuka kwenda mwendo wa kasi na kupakia abiria kupindukia uwezo wa gari.
Zanzinews

ndo kwanza namaliza kupiga mpunga hadharani.
 
kwa idadi ya waislamu pemba, sidhani kama tangazo hili lina ubaya. kwa miji mingine yenye mchanganyiko mkubwa wa watu wa dini tofauti, tangazo hili halifai
 
Mhnnn..policcm ni janga la Taifa. Mambo yalianza taratibu sasa tumefikia huko. Amani wanayoisema ccm ndo ipi? amani inayokidhi matakwa yao ya kiutawala na kidini huku haki za wengi zikimezwa na wao. Huu ni upuuzi mwingine ktk nchi hii. Mode funga huu uzi maana unamlengo wa kidini?? Unaatarisha amani ya nchi???
 
HIvi kwanini wAislamU jambo lao binafsi wanpend kuwabugudhi na watu wa dini nyingine
 
kwa idadi ya waislamu pemba, sidhani kama tangazo hili lina ubaya. kwa miji mingine yenye mchanganyiko mkubwa wa watu wa dini tofauti, tangazo hili halifai

Hata angekuwa anaishi mmoja Pemba, tangazo hili kwa Mwanvuri wa muhungano Tanganyika na Zanzibar halina maana.
 
mh! na kwaresma pia huwa wanafanya hivyo hivyo? au wakristu hawana noma na walaji wakati wa kwaresma? au pemba hakuna wakristu?

Na atakaye kaidi atapigwa .... na mimi nasema muwapige tu maana tumechoka sasa.....! by Private Message of Tzzzz ...!
 
Huko waendelee tu wasilete sharia Tanganyika

Tusio waislamu aah

iftar-meal1.jpg
 
Hivi hii Zenji ni nchi ya KIISALAM?? Maana inaonekana inaendeshwa kisharia zaidi-mfano: kuzuia WASIOFUNGA kula hadharani; mara club za pombe kuvunjwa..nk!! Sasa si watangaze tuu tujue kuwa ni nchi inayoendeshwa kwa sharia TUJUE MIPAKA YETU YA MATENDO....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom