Polisi yatembeza mabomu kwa wananchi Arusha

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
Kuna milio ya mabomu karibu na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Bado haijaeleweka ni nini kimetokea, habari kamili nitawaletea
 
Polisi imetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chadema waliokuwa wanatoka mahakamani kwa mguu kurudi makwao
 
Kuna mabomu yanapigwa hapa jirani na kituo cha kimataifa Arusha na watu wanaonekana kukimbia ovyo. inaonekana ni kuwatawanya watu waliokuwa wamekusanyika mahakamani leo Asubuhi kufuatia kesi inayowakabili viongozi wa chadema.
 
Polisi wawapiga mabomu kuwatawanya watu waliokua wakitoka mahakamani na Mbunge Lema, na watu walikua katika amani na hata hawakuwa wengi... inakua kama polisi wanafanya majaribio
 
jamani jamani... wana mabomu mengi sana nini? hivi bomu moja la machozi bei gani?
 
Muda mfupi uliopita kama dakika tano hivi, polisi mjini Arusha wamezuia kundi la waandamaji waliokuwa wakiandamana karibu na manispaa kuelekea Boma Road. Polisi hao waliwafuata waandamaji hao na kufyetua bomu la machozi. Waandamaji hao wapatao kama mia hivi walikuwa wakiimba wakisema hawamtambui Meya wa Arusha. Habari zingine baadae.
 
Wananchi wakishayazoea sijui wataanza kutumia risasi za moto? Vitu vingine havina sababu ya kufanyika, I did not expect this
 
Leo ilikuwa ni siku ya kesi ya chadema. Baada ya kesi kutajwa na kuahirishwa mahakamani wana CDM Wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Lema walitembea kwa maandamano wakiwa wanaimba "hatumtaki meya" na walipofika karibu na ofisi za manispaa polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi.
 
Kitaeleweka tu! Hapa mimi nalia kwa mabomu haya mawili yaliopigwa, kulikua hakuna sababu ya kupiga mabomu haya wakati watu walikua kwenye hali ya utulivu!
 
Hii ni aibu kwani hapa ofisi za kilimo mkoa na kwa mkuu wa Wilaya watu wenye pressure lazima wakimbizwe hospitalini kwa sababu from nowhere mabomu yamerindima bila watu kuwa na taarifa na hii imeleta mtafaruku wa watu kukimbia ovyo. Sijui kwa nini polisi Arusha wamedhamiria kuvuruga amani kwani nasikia watu walikuwa wanamsindikiza tu mbunge wao ofisini Polisi wakaingilia na kupiga mabomu.
 
Leo ilikuwa ni siku ya kesi ya chadema. Baada ya kesi kutajwa na kuahirishwa mahakamani wana CDM Wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Lema walitembea kwa maandamano wakiwa wanaimba "hatumtaki meya" na walipofika karibu na ofisi za manispaa polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi.

Heshima kwako Wikiliki,

Sidhani kama Mheshimiwa mbunge alitumia busara ?.
 
Nyepesi nyepesi kwa wana JF! Kuna hali ya uvunjifu wa amani Ausha. Silaha za machozi zimepigwa maeneo ya karibu na ofisi ya Mkuu wa mkoa jirani na Manispaa ya Arusha. Jamani tunataka amani Arusha. Hali si shwari.
 
Back
Top Bottom