Polisi wawakamata watu watatu kwa kujifanya maofisa wa Serikali na utapeli viongozi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Henry Mwaibambe.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Henry Mwaibambe

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa Serikali na kutapeli viongozi wa Serikali wakiwamo wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Henry Mwaibambe amesema mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Emanuel John (38) anashikiliwa kwa madai ya kujitambulisha kuwa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na kutapeli wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

Amewataja watuhumiwa wengine kuwa Stanley George (34) mbeba mizigo mkazi wa Temeke na Musa Nasoro (35) dereva mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Wawili hao pia wanakabiliwa na tuhuma za kujifanya maofisa wa Serikali na kutapeli viongozi.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo lilianza kuwafuatilia baada ya kufanya mawasiliano na viongozi mbalimbali na kufuatilia mawasiliano ya watuhumiwa na kugundua kuwa wahusika walikuwa Dar es Salaam.

Jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata kwa kushirikiana na polisi mkoani Dar es Salaam.

Amesema watuhumiwa wamekutwa na simu na laini nyingi zikiwa na majina ya viongozi waandamizi wa Serikali.

Mwaibambe amesema Emanuel amekuwa akipiga simu kwa viongozi akiwapa sifa kuonyesha Rais anaridhishwa na utendaji kazi wao, huku akiwataka waendelee kuwa karibu nae kwa kuwa yupo ofisi ya Rais.

Kamanda amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati upelelezi utakapokamilika.
 
Pamoja na kwamba taratibu za ajira zinajulikana kitendo cha hawa viongozi kutapelika inaonekana nafasi nyingi ni za mchongo "raisi anaridhishwa na wewe ".
Lakini pia Jeshi la polisi japo tunajua haiwezekani lakini lijaribu kuwa fair; hatukatai masela wamezingua ila hawa viongozi ndio wale kipindi flani uliwekwa uzi humu wametoa rushwa ku "secure " hizo nafasi za mchongo ko na wao wachukuliwe hatua pia kama watoa rushwa na hawafai kua viongozi. Jeshi la polisi lisiegemee upande mmoja.
 
Kwahyo tumekubaliana sio watu wa kanda ya ziwa tu ni washamba kumbe hadi viongozi wao ni washamba zaidi, imagine mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama anaingizwa mjini kizembe
 
Wamepigwa kindezi mno

Amewataja watuhumiwa wengine kuwa Stanley George (34) mbeba mizigo mkazi wa Temeke na Musa Nasoro (35) dereva mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam.
Sijui wamepigwa kiasi gani, wangepigwa zaidi ili akili ziwakae vizuri.

Wana Mavieitee, maposho, marupurupu, sijui ma pa diem ila bado maroho hivyo.
 
Tufanye hao mateepee wasingewatapeli bado yaonekana huo mchezo wa kuchukua rushwa kwa watumishi ili wapande vyeo upo.Wametapeliwa kwa sababu ni kama walikuwa wanacheza bahati nasibu.Hii michezo ipo.
 
Nafasi za juu maana yake ni ukuu wa mkoa na katibu mkuu wizara.dah,kama ni mimi sijitambulishi kuwa nimetapeliwa,nanyamaza tu kimya nimejaribu basi.
 
Back
Top Bottom