Polisi wauaji kasulu hatimaye watoroka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wauaji kasulu hatimaye watoroka

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mwandiga, Mar 6, 2012.

 1. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Hii habari niliisikia kama tetesi siku ya ijumaa tarehe 2/3/2012 kwa kuwa nilikuwa nadai vihela vyangu huko Kasulu na niliahidiwa kuzipata Jumatatu nilifunga safari Ijumaa na kufika jioni na kufanya ufukunyunyu wa kujua ukweli wa hii habari. niliyobaini ni kama ifuatavyo.
  Wale askari kama tisa hivi walioua mwananchi maeneo ya Rungwe Mpya mwaka jana walitoka lock up na kuwa mtaani, baadaye walipata uhamisho wa kwenda Kigoma na Kibondo lakini baada ya Mbunge wa Kasulu Mjini mwalimu Machari na Mhe. Mkosamali kukomalia hawa wauaji wachukuliwe hatua na sio kuhamishwa, uhamisho wao ukasitishwa mara moja ila waliohama kituo cha kasulu ni OCD, OCID NA OCS na tayari wengine wapya wamekuja wawili kati yao nilikuwa nao hapa town kigoma. Baada ya uhamisho huo kusitishwa hawa polisi wakawa mtaani tu ila wakapata habari kutoka Kigoma kuwa wanatakiwa wakamatwe. Kilichotokea ni wote kutoroka usiku wa manane wengine wakiondoka na wake zao na wengine wakiwaacha. Wake zao nimeonyeshwa walipo sehemu zao za biashara kwa wale waliobaki.
  Hivi kweli hapa kulikuwa na dhamira ya dhati kuwaadhibu hawa polisi? Ndio maana kila siku wanaua raia na hawachukuliwi hatua wanachofanya ni kulindana tu. Hongera polisi Tabora kwa kuonyesha mfano mzuri wa kuwafunza tabia polisi wenye tabia za kuua ovyo raia
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu hii ndiyo Tanzania.

  Kulindana kila sehemu kwani hapa aliyeua ni Polisi na anayekwenda kumkamata mhalifu ni Polisi. Hapa haki haiwezi kupatikana.

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Inauma? nini inauma? Mnakaa kama maboga mnasema inauma? Na itawawauma kwelikweli japo haina meno. Mmezidi undondocha enyi watanzania. Nafuu ya pundamilia kule manyara wanapigania haki zao kuliko watanzania. Mpaka mtakapojua umuhimu wa kuwafurumusha Kikwete Pinda na genge lao, hata kwa mawe ikipidi, mtaendelea kukiona kilichomnyoa kanga manyoya ya shingo
   
 4. kinganola

  kinganola Senior Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We si mtanzania?,unakichaa kweli wewe,kama hujui kujenga hoja acha kutuchefua na maneno ya kwenye taarabu...
   
 5. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hatua zaidi zichukuliwe kwa wengine wanaohusika
   
 6. s

  sugi JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Na kweli,watanzania wamezidi ukunguruu,acha wakomeshwe
   
 7. k

  kajunju JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hawa askari kweli wametoroka. Nilikuwa bar ya hawa maaskari inaitwa mkoromboko.wametoroka awapo na haijulikani wameenda wapi. Ninaowajua ni musa,shamsi, bonge. Mauaji haya ni kweli yanahusu raia wa rungwe.haijajulikana siri ilivuja vp had wakasepa.
   
 8. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mimi huwa nawaambia, siku JWtz,watakapochukua nchi hii,Polisi wote watavaa kanga mitaani,na itakuwa kiama kwao, maana wanajifanya miungu watu,wanaua raia kama kuku,
   
 9. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Achen kukurupuka hakuna m2 alotoroka
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  Hilo halipo mkuu wangu! Pengine hujui miundo ya majeshi yetu! Uasi unaweza kutokea lakini utazua vita tu na hiyo itashirikisha majeshi yote kwa mfumo tulionao!
   
 11. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Wewe ndio unakurupuka au ni mhusika a.k.a muuaji? Unataka niwataje majina kisha uniambie wako wapi? Ila nimesikia tetesi wapo 2 waliorudi wakanaswa wapo ndani lock up. Nimeambiwa mke wa mmojawapo waliotoroka wote yupo Kasulu tena mjamzito, bado sijajua ukweli wa hili ila nitarudi hapa na taarifa kamili
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Simple tu mkuu,wakati mlikuwa mnawaona jalada lilikuwa limepelekwa kwa DPP, aliporejesha majibu kwamba wakamatwe na kushtakiwa kwa murder mlolongo ambao umeanzia makao makuu Polisi Dar,walishastuliwa na ndo maana wakasepa,kimsingi hakuna cha kusepa maana taarifa zao zajulikana,ni kulindana tu
   
 13. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Umenena mkuu, japo kuna mmoja alisema nimekurupuka hawa jamaa hawajatoroka. Nikufahamishe kidogo hiyo baa imeshauzwa na mmiliki sasa hivi ni askari polisi wa hapa kigoma mjini ila nadhani kuna watakaokuwa wanamsaidia kusimamia huko Ksl.
   
 14. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Ulisema tunakurupuka sasa hapa mkurupakaji atajulikana ni nani, Hizi ni updates nzuri sana na zimenifurahisha japo kidogo. Soma kwa makini hapa chini nilivyokurupuka tena


  Na. Pardon Mbwate na Felister Elias wa Jeshi la Polisi Kigoma
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya amesema sambamba na hayo askari polisi saba wameweza kufikishwa mahakama ya hakimu mkaazi wa kigoma wakikabiliwa na mashitaka mauaji. maelezo ya matukio hayo ni kama ifuatavyo-
  Kamanda huyo amesema Askari wame kufikishwa mahakamani kwa tuhuma ya mauaji tarehe 16/03/2012 Askari saba wa Wilaya ya Kasulu walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa kigoma wakikabiliwa na tuhuma za mauaji.Askari hao wanatuhumiwa Kusababisha kifo cha Festo Stephano Sekaino mkazi wa Kijiji cha runwempya Wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma ,tukio ambalo linalodaiwa kutokea mnamo tarehe 06/08/2011. askari waliofikishwa mahakamani ni: Baraka Hongoli mkaguzi, D 9200 cpl Mawazo Mohamed, F.8252 d/cpl Swahibu Kalaghe, E.9409 pc Charles Weleka, F5276 d/c Shamsi Lung'uno, G. 1659 pc Jerry Dawson, G, 2699 pc Amrani Rajabu. pia kuna askari wawili ambao ni F.6677 d/c Musa Wilfred na G.2663 d/c Adili Mshana. hawajapatikana na juhudi za kuwatafuta zinaendelea.
  Hawa wawili hawakurudi kabisa, hao walionaswa walidanganywa mambo yameisha wakajileta kama serikali ni yao wakanaswa, Gooooooooooooood!!!!!!!!
   
 15. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,348
  Likes Received: 2,984
  Trophy Points: 280
  Mkuu hujakurupuka nadhani huyo bwana alikuwa na,lake japo.Alikuwa kamtumwa lakini ajue wazi watu wanayajua mambo zaidi anavyodhani.
   
 16. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo umenena, ukiwa mwana JF huwezi kukurupuka, unajipanga hasa ndio unaingia. Kwa kuwa alitumwa hajarudi hadi sasa au unawezekana ni mmoja wa walinaswa na hapa bangwe hawapewi muda wa kuzurura nje kama walivyokuwa kule kasulu. Narudi KGM next wk nitakuwa mahakamani kila siku, Dar washkaji wanafurahi sana jamaa wamenaswa
   
 17. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  xo mbona unakurupuka na unaongea habri ambzo hazna kichwa wala miguu achen majungu...'we co msemaj we 2lia maneno maneno by queen drne
   
 18. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  xo m naamin wenyewe wanaakil zaid yako...''2lia man acha pyepyepyepye..'
   
 19. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Sijakurupuka joe...'na wala cna llte jambo bur mda mwingne 2we 2nafikiria..'nn maana ya m2 kupelekwa mahakaman..,'achen mambo ya kizaman bana..'nyie ndo mnaomdic lulu kammaliz the great..'
   
 20. M

  Majamba Jr Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is unnecessary panic of the people who use to leave in past rather than the present.@Mtazamo,kama polisi watavaa khanga jiulize wewe itakuwaje?Uczungumzie tu jeshi kuchukua nchi ukadhan polisi itawacost. Angalia Mali pale nani inamcost.
   
Loading...