Polisi wamtoboa macho kijana wa vijibweni-kigamboni

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Nimesikitika sana kutazama kipindi kilichorushwa na channel 10 - mimi na Tanzania.kijana anadai alibambikizwa kesi ya kuvunja na kuiba. But according 2 yeye ni kwamba alikuwa na uhasama na askari aliyekuwa akimtuhumu kutembea na mkewe.Kama jambo hili ni lakweli, inabidi hatua za haraka zichukuliwe kusafisha jeshi letu la polisi. Kila siku tunasikia habari za polisi kuua na kujeruhi, hii itakwisha lini?Kwa sasa Suala lake linashughulikiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu.
 
Kitendo huyo polisi alichomfanyia ni bora angemuua kuliko kumpa adhabu kama hiyo aliyompatia
 
Jana nami nimeangalia kipindi hicho, jamani inasikitisha kweli yaani macho yametolewa, amekuwa kipofu ghafla bila kutegemea, na kasema hao polisi anawajua! hebu sheria ichukue mkondo wake jamani
 
Ndiyo nchi yetu, polisi wanauwa, wanaacha watu na vilema vya maisha, nchi haina mkemeaji wala msemaji. Hiyo ndiyo TZ yetu.
 
polisi loool unaingizwa mule kwa kosa la kuiba kuku lakini unajikuta unapewa ya mauwaji huku muuwaji mwenyewe anatorokea nje ya nji jamaniii
 
Aiseee polisi wetu wana mambo ya ajabu sana ila iko siku watajua hasira tulizonazo juu ya matendo yao.
 
Haya mambo polisi wamezoea sana tatizo huwa hawachukuliwi sheria wala nini ndio maana haya matatizo yanajirudia kila kukicha.
 
Back
Top Bottom